Nini kinachotuongoza? Sheria na Katiba au hila na fadhila za Rais?

Nini kinachotuongoza? Sheria na Katiba au hila na fadhila za Rais?

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
94,296
Reaction score
122,540
Wanasema eti kuuliza si ujinga! Wakati ujinga ni hali ya kutojua kitu au jambo fulani.

Sasa kama kitu unakijua au jambo unalijua, unauliza ili iweje sasa?

Baadhi ya hii misemo ya Kiswahili ukiichambua kwa undani utabaini haina mantiki kabisa.

Ah! Hayo ya misemo ya Kiswahili tuyaache kwa leo maana nina ujinga wa mambo kadha wa kadha na ningependa niufute.

Haya twende kazi:

Hivi, hili suala la katiba mpya ni suala la fadhila ya Rais aliyepo madarakani au?

Nauliza hivyo kwa sababu tokea hili vuguvugu lianze tena baada ya kifo cha Rais Magufuli, kumekuwepo na maombi kwa Rais Samia kuwa aurejeshe tena mchakato wa katiba mpya.

Mara kadhaa sasa yeye Rais Samia keshasema suala hilo lisubiri [kidogo/ kwanza] maana anataka aisimamishe kwanza nchi kiuchumi.

Ni kama sielewi elewi vile inakuwaje suala muhimu kama hilo kuhusu mustabali wa taifa liwe ni suala la hisani ya mtu mmoja ilhali taifa linakadiriwa kuwa idadi ya watu takriban milioni 60.

Jingine ambalo silielewi elewi ni hili suala la huyu jamaa wa CHADEMA aitwaye Mdude Nyagali.

Hivi hilo ‘Mdude’ ni jina lake kweli? 🤔

Baada ya kutoa kauli yake ya hivi karibuni kwamba kimsingi ataendelea kuanzia palepale alipoishia kabla ya kwenda jela kipindi Rais Magufuli akiwa hai, kumekuwepo na maneno maneno ya kwamba auchunge mdomo wake kuhusu anayoyasema dhidi ya Rais Samia kwa sababu yeye Mama Samia ndo kamtoa huko jela alikokuwa.

Ina maana Tanzania mtu kuwa jela au kuwa huru kunaweza kutegemea hila ama fadhila za Rais aliyepo madarakani na si sheria za nchi?

Madai ni kwamba Mdude alibambikiwa kesi na utawala wa Magufuli. Lakini utawala wa Samia umeamua kumwachia huru 🤦‍♂️.

Rais Magufuli alipiga marufuku wanasiasa kufanya shughuli za kisiasa nchini. Akasema eti wanaruhusiwa tu kufanya shughuli hizo kwenye majimbo yao.

Ajabu kweli kweli maana Tanzania ni nchi iliyo huru na nijuavyo Mtanzania yeyote yule ana haki ya kufanya kazi sehemu yoyote iliyo nchini mwake.

Kaja Rais Samia naye anaendelea na uamuzi huo huo wa kupiga marufuku shughuli za kisiasa kwa wanasiasa nje ya majimbo yao isipokuwa kwa CCM tu.

Ni wazi kabisa kuwa hii amri ni ukiukwaji wa katiba maana shughuli za kisiasa ni haki kwa mujibu wa katiba.

Sielewi kwa nini wanasiasa wa upinzani hawaikaidi hiyo amri maana sheria ipo upande wao.

Kwani kwa mfano wakiamua kuzifanya hizo shughuli za kisiasa nchi nzima, nini kitawatokea?

Watakamatwa na polisi na kufungwa jela? Watashitakiwa na serikali kwa kosa/ makosa gani?

Watafikishwa mahakamani na kushitakiwa kutenda kosa/ makosa gani?

Kama wanachokifanya ni haki yao kikatiba, ni mahakama gani itayowapata na hatia ya kuitumia haki yao ya kikatiba?

Hii nchi bana…imejaa watu wa ajabu kweli!
 
Wapumbavu hudhani tunaongozwa na kudra za rais. Hii ni kwa sababu ya wananchi hawajawahi kuandika katiba

Bado tunatumia katiba ya watawala.

Ni wakati sasa tukapata katiba ya wananchi ili kuleta utulivu na kukuza uchumi wetu.

Kwa katiba hii hata wezi viongozi wakiiba hazina ya nchi, inawalinda wasishtakiwe kisa tu nafasi wanazohodhi!

Nchi haiwezi kuendelea kwa ujinga huu!
 
Tanzania sheria na taratibu zipo.

Ila suala la utekelezaji ni maamuzi ya Rais.

Hata wewe unaweza ukakamatwa tu ukawekwa jela na hakuna kitu utafanya.

Waulize masheikh wa uamsho.

Watu pekee wanaoweza kuishurutisha serikali ni wananchi kwa umoja wao, ila hapa kwetu watu hawajawa na utayari kwa hilo.

Kila mtu bado anapenda maisha yake.

In short, kwa nchi kama yetu ukipata Rais anawasikiliza watu hata kidogo ni kushukuru Mungu.

Maana anaweza asimsikilize mtu yeyote na hakuna kitu tutafanya.
 
Nyani Ngabu:Hii nchi kiukweli Ina watu wajinga Sana bado ,iwe upande wa upinzani na hata upande wa CCM.Ndo Mana haki inaonekana hisani kwa hiyo basi nchi hii haitakaa ipate MAENDELEO hadi kwanza ujinga na upumbavu uishe,Uliona wapi nchi yenye majority ambao ni mazuzu na wakati huo ikawa na MAENDELEO?
 
Hii nchi bwana!! Eti ikimpendeza rais! Mtu wa kwanza kuongozwa na katiba na sheria ni lazima awe rais.
Sasa sheria na katibas ni lazima viwe na misingi imara kwa sasa hili ndilo tatizo!
Ndo maana waimba pambio husema, ikompendeza rais, kama vile ni Mungu.
 
Back
Top Bottom