Rais anafurahia sana ujinga wa wananchi, maana hata kilicho chao wanaenda kumwomba Rais.
Kuna siku tutaenda kumwulizavRais, kama tuvae suruali au misuli!
Huu utukufu wa Rais, ni sisi ndio tunampa kutokana na uwoga, ujinga, na unafiki wetu. Katiba inasema vyama vina haki ya kufanya siasa wakati wowote, svyama vinasubiri mpaka Rais aseme, nendeni mkafanye siasa.
Mbowe alikuwa sahihi sana kusema wataanza kufanya mikutano ya hadhara. Hakuwa hata na haja ya kumtaja Rais. Alitakiwa tu kutoa maelekezo kwa viongozi na wanachama, maana ni haki ya kikatiba. Tutamshangaa atakayezuia, tutamwuliza ni kwa sheria ipi anazuia.