Nini kinachotuongoza? Sheria na Katiba au hila na fadhila za Rais?

Nini kinachotuongoza? Sheria na Katiba au hila na fadhila za Rais?

Hii nchi bwana!! Eti ikimpendeza rais! Mtu wa kwanza kuongozwa na katiba na sheria ni lazima awe rais.
Sasa sheria na katibas ni lazima viwe na misingi imara kwa sasag hili ndilo tatizo!
Ndo maana waimba pambio husema, ikompendeza rais, kama vile ni Mungu.
Hii nchi rais Ni wa pili baada ya mwenyezi mungu...
 
Tumejawa na watu tunaopenda hisani siyo haki, watu haki zetu za msingi tunahisi tunapaswa kuwabembeleza wakubwa watupatie.

Cha kushangaza tunafurahia hili jambo na ajabu zaidi ukionekana unadai haki Watanzania wenzako huanza kukusuta na unaonekana huitakii mema nchi yako.
 
Ko cha msingi mkuu unashauri wakae kimya tuu wasifanye chochote.?
Waongee kwa hekima na staha! Kutumia lugha kali za vitisho havijawahi kurahisisha mchakato wa kupata unachotaka toka kwa mtu mwenye mamlaka ya kukuzidi. Kama huamini mshurutishe boss wako hapo ofisini juu ya malipo yako yaliochelewa kisha uone utadumu muda gani katika hiko kiti!
 
Tanzania sheria na taratibu zipo.

Ila suala la utekelezaji ni maamuzi ya Rais.

Hata wewe unaweza ukakamatwa tu ukawekwa jela na hakuna kitu utafanya.

Waulize masheikh wa uamsho.

Watu pekee wanaoweza kuishurutisha serikali ni wananchi kwa umoja wao, ila hapa kwetu watu hawajawa na utayari kwa hilo.

Kila mtu bado anapenda maisha yake.

In short, kwa nchi kama yetu ukipata Rais anawasikiliza watu hata kidogo ni kushukuru Mungu.

Maana anaweza asimsikilize mtu yeyote na hakuna kitu tutafanya.
Nimeipenda hiyo " hakuna kitu tutafanya". Ukweli ulio perfect
 
Waongee kwa hekima na staha! Kutumia lugha kali za vitisho havijawahi kurahisisha mchakato wa kupata unachotaka toka kwa mtu mwenye mamlaka ya kukuzidi. Kama huamini mshurutishe boss wako hapo ofisini juu ya malipo yako yaliochelewa kisha uone utadumu muda gani katika hiko kiti!
Tumejawa na watu tunaopenda hisani siyo haki, watu haki zetu za msingi tunahisi tunapaswa kuwabembeleza wakubwa watupatie.

Cha kushangaza tunafurahia hili jambo na ajabu zaidi ukionekana unadai haki Watanzania wenzako huanza kukusuta na unaonekana huitakii mema nchi yako.
 
Tumejawa na watu tunaopenda hisani siyo haki, watu haki zetu za msingi tunahisi tunapaswa kuwabembeleza wakubwa watupatie.

Cha kushangaza tunafurahia hili jambo na ajabu zaidi ukionekana unadai haki Watanzania wenzako huanza kukusuta na unaonekana huitakii mema nchi yako.
True.
 
ukifuatilia kwa umakini mtiririko wa matukio yaliokwishatokea nchini utagundua ya kwamba Tanzania ya sasa inaongozwa zaidi kwa kutumia zaidi Ihsani kuliko sheria, hata haki na wajibu kwa mtanzania yamemezwa na hisani.
  1. mtanzania kupewa kitambulisho cha mtanzania au passport limekuwa ni jambo la hisani
  2. mtanzania kuchagua kiongozi amtakaye ni hisani
  3. mtanzania kulipa kodi imekuwa ni hisani kwake, wanaolipa kodi hawafiki millioni 3
  4. bunge na mahakama vinaendeshwa kwa Ihsani ya raisi
  5. mfanyakazi wa taasisi za kiserikali kukupa huduma ya haraka ni hisani kwake
  6. mkopo wa elimu ya juu ni hisani kwa mwanafunzi
 
01: Kiuhalisia hakuna usawa na uhuru kati ya mihimili yetu ya Serikali, Bunge na Mahakama kama Katiba inavyohitaji.

02: Hakuna matashi mema ya watu na taasisi zetu kusimamia haki na wajibu kama inavyostahili.

03: Tuna ubinafsi mwingi na kila mmoja anaangalia masilahi yake binafsi na siyo masilahi mapana ya nchi.

04: Hatuna uzalendo kama tunavyotaka tuonekane.

05: Suluhisho ya yote haya tuwe wazalendo wa kweli, sote wananchi na viongozi, tuachane na huu unafiki. Lest tutaendelea kuongozwa na hila na fadhila za Rais.
 
Katiba na sheria zipi hizi zinazowazuia watu kufanya shughuli za kisiasa nchini?
Nyani Ngabu katika ubora wake. Umegonga kule ambako mashabiki wengi wa siasa za Tanzania hawataki. Kwa mfano hili la Mdude nimeshangaa kusikia hata wanasiasa na wasomi makini wakisema hana shukrani kwa rais aliyemtoa jela. Kumbe ametolewa ili aonyeshe shukrani hata kama hakubaliani na kinachofanywa na rais! Observation yako wala usiwe na mashaka nayo. Nchi ya Tanzania rais ni kila kitu. Anaweza kuamua nani afungwe, nani afanye mkutano na vyama vya siasa vipewe au visipelewe haki haki. Hii ni kwa sababu vyombo vya dola na mihimili yote ya serikali iko chini yake na inafuata matakwa yake. Ndiyo maana wengi wanasema bila kuwa na katiba mpya ni bure. Hili la msemo wa kiswahili ''kuuliza siyo ujinga'', ni msemo mzuri sana na hauna mushkeli wowote. Kama ilivyo misemo mingi katika jamii, huendana na tamaduni na tabia za jamii. Huu msemo una-encourage watu kuuliza bila kuwa na aibu wakidhani watachekwa kwa sababu ya kuonekana ni wajinga. Ndiyo maana wakasema ''kuuliza siyo ujinga bali ni kutaka kujua''. Yaani ukiona mtu anauliza jambo fulani basi huyo mtu ni mwerevu kwani anataka kujua zaidi/kuchokonoa zaidi kuhusu lile jambo. Mfano hai: wewe haya yote uliyouliza yanaonyesha hakika wewe siyo mjinga!
 
Tumejawa na watu tunaopenda hisani siyo haki, watu haki zetu za msingi tunahisi tunapaswa kuwabembeleza wakubwa watupatie.

Cha kushangaza tunafurahia hili jambo na ajabu zaidi ukionekana unadai haki Watanzania wenzako huanza kukusuta na unaonekana huitakii mema nchi yako.
Sawa haki sio hisani naelewa ila kuna namna ya kuidai hio haki! Angalia nani anapaswa akupatie hio haki? Personality traits zake zikoje? Kuna watu wanataka kuwa pleased ili upate unachotaka na ambao ndio wengi kuliko wale ambao wanajua kukupatia haki ni wajibu wao so hutenda bila kuombwa!

Shida ya hawa ndugu zetu wao wanataka haki kwa kupush kauli za kibabe! Ukikutana na mtu mwenye roho ngumu anakufyekelea mbali and the rest is history! Tuwe na adabu kidogo...tunadai haki ila tuwe na adabu kidogo huwezi kuvunja vipengele vya katiba kwa makusudi hii ni nchi yenye utawala wa sheria sio kijiwe cha kahawa kwamba lugha za chooni ni ruksa kwa yeyote yule!

Ombeni kibali fateni taratibu mkinyimwa lalamikeni na mtoe hoja zenu mama personality yake ni rahisi kusikiliza watu. She is not a harsh person kama mtangulizi wake so mambo yanaweza kwenda smooth watu wakitumia akili vizuri. Wakitaka ubabe vijana wenye kazi ya kuwatuliza wapo!

Ningependa hao wanaojitia wana uchungu sana na katiba wapeleke matumbo yao mbele na familia zao kisha wakifanikiwa kwenye hio vurugu watanzania wengine watafuata!

Mie nimesema ntashiriki mchakato wa hio katiba mpya kama kutakuwa na kipengele cha wananchi kupewa hela ya maendeleo 5M cash kwenye account zao kila mwanzo wa mwaka mpya wa serikali. Kama hilo litakuwepo ntawaunga mkono ila kama ni lile la kuwaingiza akina Mbowe Ikulu tu basi sihusiki na shughuli hio!
 
Rais anafurahia sana ujinga wa wananchi, maana hata kilicho chao wanaenda kumwomba Rais.

Kuna siku tutaenda kumwulizavRais, kama tuvae suruali au misuli!

Huu utukufu wa Rais, ni sisi ndio tunampa kutokana na uwoga, ujinga, na unafiki wetu. Katiba inasema vyama vina haki ya kufanya siasa wakati wowote, svyama vinasubiri mpaka Rais aseme, nendeni mkafanye siasa.

Mbowe alikuwa sahihi sana kusema wataanza kufanya mikutano ya hadhara. Hakuwa hata na haja ya kumtaja Rais. Alitakiwa tu kutoa maelekezo kwa viongozi na wanachama, maana ni haki ya kikatiba. Tutamshangaa atakayezuia, tutamwuliza ni kwa sheria ipi anazuia.
 
Waongee kwa hekima na staha! Kutumia lugha kali za vitisho havijawahi kurahisisha mchakato wa kupata unachotaka toka kwa mtu mwenye mamlaka ya kukuzidi. Kama huamini mshurutishe boss wako hapo ofisini juu ya malipo yako yaliochelewa kisha uone utadumu muda gani katika hiko kiti!
Mkuu umejikita katika kulinda maslahi ya muda mfupi na yanayo umiza. Kudai haki yako siyo kumshurutisha mtu ni kitu ambacho unadeserve kupata siyo kuwa unahurumiwa.

Harafu ukidai haki yako kwa huyo boss hata usipodumu katika hiyo kazi naamini siyo vibaya cha msingi hujataka haki yako kusiginwa.

| tunapalilia dhuluma hivyo uvinjifu wa haki unamea na kustawi katika jamii zetu|
 
Back
Top Bottom