Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 63,730
- 111,542
Katiba na Sheria!
Kwa hii katiba ilivyo mbovu rais yuko juu ya katiba na sheria. Na kiuhalisia rais ndio anaendesha sheria za nchi, na sio nchi kuendeshwa kwa sheria. Yote haya rais anafanikiwa kuyafanya maana katiba imempa nguvu ya kuamrisha vyombo vya dola kufanya atakavyo, bila kuulizwa na yoyote, na hawezi kushitakiwa kwa makosa yoyote atakayofanya akiwa madarakani au ametoka. Iwapo katiba itarekebishwa kwenye madaraka ya urais, inatakiwa rais akitoa maagizo aweke kwa maandishi, huku akiweka wazi vifungu vilivyovunjwa, na vifungu vinavyomruhusu kutoa amri hiyo. Hii itaaondoa sheria iliyo na nguvu kabisa kuliko zote iitwayo amri kutoka juu. Amri kutoka juu asili yake kubwa huwa inatokana na madaraka makubwa ya urais yanayotumika vibaya.