Nini kinachotuongoza? Sheria na Katiba au hila na fadhila za Rais?

Nini kinachotuongoza? Sheria na Katiba au hila na fadhila za Rais?

Katiba mpya ina umuhimu wa kipekee
E5tTtHJWEAAuzmp.jpeg
 
Kwa wanaofikiri kwa kutumia ubongo ni muhimu. Ila kwa wale wenye kufikiri kwa kutumia makalio na tumbo sio muhimu.

Kwangu mimi kama mtanzania katiba ni muhimu sana
 
Kwanza wananchi ni haki yao kupewa elimu na kabla ya kupata katiba mpya ni lazima kuimarisha taasisi zetu kutoa maamuzi kutoka taasisi moja kwenda taasisi nyingine.

Maana kuna nchi zina katiba iliyo bora lkn hakuna nguvu ya katiba. Suala la katiba mpya halipaswi kuwa ni la The Big Vegetables au taasisi fulani ni la wananchi wenyewe.
 
Hii kitu imelipasua taifa kwa muda wa siku kadhaa. Baadhi ya wananchi kupitia vyama vyao wanadai ni lazima wapate katiba mpya. Sababu ile ha mwaka 1977 imekuwa outdated. Na haikidhi mahitaji ya kutatua kero za wananchi.

Waliomadarakani wametoa sababu kuwa nao wanatambua kuwa katiba ya sasa imepwaya. Ila wanataka wawatumikie wananchi kwa kuwaletea maendeleo kwanza. Maendeleo yakipatikana ndio wataleta katiba mpya.

Kidhaaa kimezuka baaada ya baadhi ya wananchi kudai kuwa patachimbika kama watawala hataweka mezani mchakato wa kupata katiba mpya.

Sasa je kupata katiba mpya ni mpaka watawala watake au ni pale wananchi wanapohitaji?
 
Serikali ni chombo chenye mamlaka na madaraka na ushawishi mkubwa mno dhid ya raia. Raia ni kama mtoto yatima ambaye mali za urithi amekabithiwa baba mkubwa. Hapo ndin atajua hzo ni zake au vipi!?
 
Hii kitu imelipasua taifa kwa muda wa siku kadhaa. Baadhi ya wananchi kupitia vyama vyao wanadai ni lazima wapate katiba mpya. Sababu ile ha mwaka 1977 imekuwa outdated. Na haikidhi mahitaji ya kutatua kero za wananchi.

Waliomadarakani wametoa sababu kuwa nao wanatambua kuwa katiba ya sasa imepwaya. Ila wanataka wawatumikie wananchi kwa kuwaletea maendeleo kwanza. Maendeleo yakipatikana ndio wataleta katiba mpya.
Walio madarakani ni CCM, Serikali ni ya CCM halafu majibu yale yalikuwa ya fedhea ya tungojee, kwanza tupate maendeleo halafu yakipatikana ndio iwekwe mezani? CCM inaogopa nini? na sisemi hivyo kama CCM ni waoga, hawa sio waoga, angalia siku hizo mia moja wamepiga nyuzi 180 bila woga, sasa hili la Katiba ni nini linalowaogopesha?
Kidhaaa kimezuka baaada ya baadhi ya wananchi kudai kuwa patachimbika kama watawala hataweka mezani mchakato wa kupata katiba mpya.

Sasa je kupata katiba mpya ni mpaka watawala watake au ni pale wananchi wanapohitaji?
Wananchi wameshazungumza na wangependa kupata Katiba mpya, wananchi hawa wanawakilishwa mezani na Wabunge wao, wabunge, CCM! kuna mkongano hapa kama mashauri yao hayapewi kipaumble na Wabunge wao, mbadala wake uwe kuwachagua Wabunge wenye kujali Wananchi na matakwa yao ya Katiba, ya Kikatiba pamoja na kuilinda Katiba hiyo.
Watawala ni CCM na bila woga wananchi, wanapohitaji, kwenye chaguzi zijazo waanze kuwang'oa hawa kutoka kwenye utawala. Pataeleweka tu.
 
Hii kitu imelipasua taifa kwa muda wa siku kadhaa. Baadhi ya wananchi kupitia vyama vyao wanadai ni lazima wapate katiba mpya. Sababu ile ha mwaka 1977 imekuwa outdated. Na haikidhi mahitaji ya kutatua kero za wananchi...
Hivi kweli Kikwete angaliruhusu katiba mpya si angekuwa lupango na familia yake? Je, faida ya katiba mpya kwa watawala unaijua? Hii hapa katika picha na baada ya kuziona ndipo ufanye tafakuri ya swali lako.

50983F03-4136-49F0-AE28-57AD363F413D.jpeg
75517F3F-7B3B-4EC9-ACF2-569E5836E2F8.jpeg
94053D9D-A566-41E1-AA8F-A5701FE7E6F5.jpeg
810CDAC4-E654-4019-AFD1-FCDE1CBC0FAE.jpeg
 
Katiba na sheria zipi hizi zinazowazuia watu kufanya shughuli za kisiasa nchini?
Hakuna sheria wala Katiba haizuii shughuli za kisiasa za vyama isipokuwa CCM ndiyo wanawazuia Watanzania kufanya siasa.
Pia ni CCM hiyo hiyo iliyoharibu uchumi wa Tanzania kwa kutumia vibaya Katiba mbovu wanadai ili Watanzania kupata Katiba ya Wananchi tusubiri waimarishe kwanza uchumi.Je,kilichoangusha uchumi wetu na kudumaza maendeleo yetu ni Katiba Bora(Ya Wananchi)?
Je,mchakato wa Katiba Mpya ulianzishwa wakati uchumi wa Tanzania ukiwa katika Haki gani 2011-2015?Vipi kuhusu fedha za umma zilizoteketezwa wakati ile?Nani atatulipà?
 
"kauli ya rais ni sheria" nchi zenye ustawi huwezi kuta huu ujinga upo Tanzania tu
Huo ni ubovu mojawapo wa Katiba tuliyonayo,kuna kauli hazifai kuwa Sheria maana zinakiuka misingi ya Haki.Hizo nazo ziwe Sheria?Hayo ni mawazo ya kiimla na hayana Tina kwa dunia ya sasa.Stand for your Rights,wakeup!
 
Back
Top Bottom