Nini kinaendelea kuhusu mechi ys Simba na Yanga ambayo iliahirishwa katika mazingira ya utatanishi baada ya Simba kugoma kufika uwanjani?

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
52,828
Reaction score
165,667
Habari wadau!

Mpaka sasa, tumesikia na kusoma mengi kuhusu hii mechi ambayo haikuchezwa baada ya Bodi ya ligi kuiahirisha huku Yanga wakifika uwanjani na Simba kutofika kama walivyokuwa wamepanga.

Je, ni kweli jambo hili sssa liko huko CAS kwa ajili ya usuluhishi na maamuzi?

Na kama kweli jambo jilo liko CAS kama tulivyosoma kwenye mitandao na kuona zile nyaraka, hukumu ni lini?

Kama haliko huko CAS, nini kinaendelea kuhusu hatima ya mchezo huo?

Kwa kifupi, nini kinaendelea na nini inaweza kuwa ni madhara ya hukumu hiyo kwa Simba inayoshiriki michuano ya CAF?
 
Hili ni suala la kisheria:
1: Kama kesi iko CAS, Yanga walipewa siku 10 kuwasilisha madai yao ya kisheria ILI wadaiwa TFF na Simba wapewe siku 20 kujibu madai.

2: Yanga wasipopeleka/ kuwasilisha malalamiko yao ndani ya siku 10 kesi inajifuta. Je wamewasilisha na vielelezo?

3: Vielelezo ni pamoja na maamzi ya TFF juu ya jambo la msingi, Je kesi lilishaamliwa au yale yalikuwa majibu ya barua/yatokanayo?

4: Je sheria za CAS zinasemaje kwa suala ambalo bado ni bichi/halijatolewa maamzi ya mwisho na chombo husika/ kwenye nchi kupelekwa kule?

5: Nani ataathirika, inategemea na nani kavunja sheria gani na inahusika kwa nafasi ipi kwa kiasi gani(ni nyumbani au kimataifa).

NB: Kuna sintofahamu nyingi ila zote zitafata sheria za vyombo husika juu ya jambo husika na jinsi lilivyojikunjakunja.
 
Hizo sintofahamu zote zinatokana na Simba na Yanga kuendeshwa na wanasiasa wa CCM.

Mwisho wa siku kitakachoamuliwa kitaangalia nini kitaifadisha CCM. Hapo maslahi ya CCM ndiyo yatakayozingatiwa.
 
Habari wadau!

Mpaka sasa, tumesikia na kusoma mengi kuhusu hii mechi ambayo haikuchezwa baada ya Bodi ya ligi kuiahirisha huku Yanga wakifika uwanjani na Simba kutofika kama walivyokuwa wamepanga.

Je, ni kweli jambo hili sssa liko huko CAS kwa ajili ya usuluhishi na maamuzi?

Na kama kweli jambo jilo liko CAS kama tulivyosoma kwenye mitandao na kuona zile nyaraka, hukumu ni lini?

Kama haliko huko CAS, nini kinaendelea kuhusu hatima ya mchezo huo?

Kwa kifupi, nini kinaendelea na nini inaweza kuwa ni madhara ya hukumu hiyo kwa Simba inayoshiriki michuano ya CAF?
hii mechi bora ipangwe iwe mechi ya mwisho ya msimu!
 
Hili ni suala la kisheria:
1: Kama kesi iko CAS, Yanga walipewa siku 10 kuwasilisha madai yao ya kisheria ILI wadaiwa TFF na Simba wapewe siku 20 kujibu madai.

2: Yanga wasipopeleka/ kuwasilisha malalamiko yao ndani ya siku 10 kesi inajifuta. Je wamewasilisha na vielelezo?

3: Vielelezo ni pamoja na maamzi ya TFF juu ya jambo la msingi, Je kesi lilishaamliwa au yale yalikuwa majibu ya barua/yatokanayo?

4: Je sheria za CAS zinasemaje kwa suala ambalo bado ni bichi/halijatolewa maamzi ya mwisho na chombo husika/ kwenye nchi kupelekwa kule?

5: Nani ataathirika, inategemea na nani kavunja sheria gani na inahusika kwa nafasi ipi kwa kiasi gani(ni nyumbani au kimataifa).

NB: Kuna sintofahamu nyingi ila zote zitafata sheria za vyombo husika juu ya jambo husika na jinsi lilivyojikunjakunja.
Hiyo namba 1 & 2 naomba kujua wapi Yanga waliambiwa wapeleke malalamiko na vielelezo ndani ya siku 10? Nachojua Yanga ndio alipeleka malalamiko CAS kwa maana hiyo aliwasilisha vielelezo vya malalamiko yake. Sasa kwanini yeye ndio apewe siku kumi za kuwasilisha malalamiko?

Naomba kuelekezwa hapo tafadhali
 
Nenda ukasome kwa makini maelezo kwenye ile memo na uielewe, usishinikize ubongo kukatalia hayo unayosema unayaelewa.
IMG_3797.jpeg
 
Bodi ya ligi watajuta kutumiwa na simba kuahirisha ile mechi. Wakati mwingine ni bora kuweka kanuni zinazo tekelezeka.
Timu ikisusia mechi kutokana na sababu za kitoto; timu pinzani ipewe pointi 3 na magoli 3! Full stop.

Na pia ijiwekee mipaka ya kuruhusu wanansiasa kuwatumia. 2021 waliahirisha mechi ya Yanga na simba kutoka saa 11 mpaka saa 1 jioni kinyume na kanuni/utaratibu! kwa sababu tu ya kumfurahisha mwanasiasa! Na mwisho wa siku mechi haikufanyika.
 
Tatizo ni nyie utopolo kujifanya ni timu ya CCM. Mnasema timu yenu eti ilipigania uhuru wa Tanganyika😆😀😃

Mwaka 2015 nilifika klabu ya Yanga na kuona mpaka ndani kabisa ya kuta za Klabu hiyo kumebandikwa mabango ya Magufuli wakati huo akiwa ni Mgombea Urais kupitia CCM. Kwa kweli nilikereka kupita kiasi.
 
Hiyo namba 1 & 2 naomba kujua wapi Yanga waliambiwa wapeleke malalamiko na vielelezo ndani ya siku 10? Nachojua Yanga ndio alipeleka malalamiko CAS kwa maana hiyo aliwasilisha vielelezo vya malalamiko yake. Sasa kwanini yeye ndio apewe siku kumi za kuwasilisha malalamiko?

Naomba kuelekezwa hapo tafadhali
Si ndie alieshtaki,sasa unataka nani apewe siku wakati aliyekwenda CAS NI YANGA
 
Nenda ukasome kwa makini maelezo kwenye ile memo na uielewe, usishinikize ubongo kukatalia hayo unayosema unayaelewa.View attachment 3301574
Nimesema nimeomba kueleweshwa acha ushari kwa kunilisha maneno eti nashinikiza. Haya tuma document bila kuweka hayo mashading yako kwa maana nachosoma hapo ni wèwe ndio unaelewa tuma niisome yote.
 
Nimekueleza soma ukiwa na mawazo huru ili uielewe(critical reading), sababu lugha inayotumiwa pale ni ya kisheria. Wala hakuna ushari wowote juu ya hilo. Nimeweka document na nimekusaidia kuzungushia maeneo husika ambayo ni tafsiri ya kingereza kwa yale niliyoyaeleza mwanzo yakiwa kwenye andishi husika.
 
Ukienda CAS si unapeleka vielelezo vyote vya nia ya kutaka kesi ifunguliwe then washtakiwa ndio wanaambiwa walete na wao ushahidi wao.
1: Kuna kupeleka nia ya kushitaki.

2: Kupeleka shitaka rasmi na vielelezo.

3: Shitaka kupokelewa rasmi na CAS.

4: Shitaka kupelekwa kwa washtakiwa ili wapeleke utetezi wao dhidi ya mashtaka na vielelezo.

5: Kesi kuanza kusikilizwa.
 
Nimekueleza soma ukiwa na mawazo huru ili uielewe(critical reading), sababu lugha inayotumiwa pale ni ya kisheria. Wala hakuna ushari wowote juu ya hilo. Nimeweka document na nimekusaidia kuzungushia maeneo husika ambayo ni tafsiri ya kingereza kwa yale niliyoyaeleza mwanzo yakiwa kwenye andishi husika.
Kulingana na hiyo article kama ni kweli Yanga ndio kaandikiwa anatakiwa apeleke vifungu vya sheria (kanuni, sheria na miongozo ya bodi ya ligi) vinavyo mfanya asikilizwe madai yake which is simple haviwezi kuchukua hata siku mbili hiyo email inatumwa.

Japo mimi bado nahitaji document yote niisome sio hiyo iliyokua shaded.
 
Kinachoendelea ndugu Yangu ni Yanga Wameachwa Waneng'eneke weee.... Baada ya hapo Simba akishatwaa Kombe La Shirikisho aje ambutue Utopolo ambaye atalazimishwa kucheza..atake au asitake..!

Tumechoka kuongea Lugha laini laini.!
 
Kulingana na hiyo article kama ni kweli Yanga ndio kaandikiwa anatakiwa apeleke vifungu vya sheria (kanuni, sheria na miongozo ya bodi ya ligi) vinavyo mfanya asikilizwe madai yake which is simple haviwezi kuchukua hata siku mbili hiyo email inatumwa.

Japo mimi bado nahitaji document yote niisome sio hiyo iliyokua shaded.
IMG_3795.jpeg
IMG_3797 (1).jpeg
 
Back
Top Bottom