Nini kinakuogopesha kufungua au kufanya biashara?

Sawa mwamba
 
Tatizo kubwa ni majambazi wa TRA na pia ni UPORAJI wa pesa za wafanya biashara uliokuwa unafanyika nchini tangu 2015. Hivyo ni bora watu wafunge biashara zao au kuhamia nchi za jirani kufanya biashara.
 
Changamoto ni kupata watu sahihi ambao ndio wazalishaji au watendaji (technical skill) hasa kwenye biashara ya teknolojia. Kwenye hizi biashara zingine changamoto kubwa ni masoko
 
Tuwekane wazi tu unavyoanza biashara unahitaji kuwa na moyo wa chuma yaani uvumilivu wa hali ya juu kupitiliza,akili na muda wako lazima viwe kwenye biashara pia jiandae kupoteza pesa nyingi sana ndio maana wengi wanashauri usiweke pesa yote kwenye biashara sababu ili kupata faida hiyo biashara uliyoanzisha itahitaji marekebisha mengi sana na shida kuna vitu vingi kuvijua kwenye biashara mpaka uingie ndio utavigundua na pesa itahitajika kuweka sawa ila jinsi muda unavyokwenda mambo yanafunguka na biashara inakuwa nyepesi na faida unaiona hata kama ni kidogo.
 
Mimi naona bora hiyo nyumba uigeuze guest tu kidoogo upepo unasoma vizuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…