Mkiambiwa CCM ni tatizo nambari wani Tanzania muwe mnatuelewa. Haiihitaji ubishi.
Siasa ni maisha yako/yenu. Take it very serious. Tukitaja hapa kashfa na ufisadi dhidi ya rasilimali zetu chini ya CCM, server ya JF inaweza zima!
Siasa sio ushabiki. Siasa inagusa uhai, uchumi, maisha na haki zako za msingi.
Mkiambiwa Katiba Mpya inahitajika sasa sikilizeni na muelewe; ni kwa faida yenu na vizazi vyenu na pia kwa ulinzi na unufaikakaji wa rasilimali zote Mwenyezi Mungu alizotupa.
Baada ya muda mtasahau (na wanawajua sana). Mtaletewa (wananchi) vitu vya kipuuzi, halafu mtadandia na kuachana na mambo muhimu kama hilo la bandari, kama mlivyofanya kwa ripoti ya CAG na mengine mengi.
Watawala wanalijua hilo, wanawajua maungo yenu.