Nini kipo nyuma ya Mzungu John Robert Maitland, alifungwa Tanzania miezi 6 lakini bado yuko Gerezani Segerea zaidi ya miaka 10?

Nini kipo nyuma ya Mzungu John Robert Maitland, alifungwa Tanzania miezi 6 lakini bado yuko Gerezani Segerea zaidi ya miaka 10?

Black Butterfly

Senior Member
Joined
Aug 31, 2022
Posts
130
Reaction score
368
JOHN ROBERT MAITLAND DHIDI YA JAMHURI

Mshtakiwa alishtakiwa kwa kosa la kuingia na kuwepo kinyume cha sheria ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mahakama ya Wilaya Bukoba, Kavera.

Alikutwa na hatia na kuhukumiwa kulipa faini ya Shilingi 80,000 za Kitanzania au kifungo cha miaka miwili iwapo atashindwa kulipa faini hiyo, pamoja na viboko 10.

Robert hakuridhika na uamuzi wa Mahakama alikata rufaa katika Mahakama Kuu. Mahakama Kuu ilifuta adhabu ya viboko lakini ikathibitisha hatia ya mshtakiwa.

Aidha, Mahakama Kuu ilitoa amri ya kumfukuza mshtakiwa nchini, ikamhukumu kwa kosa la kuidharau Mahakama, na kumfunga kifungo cha miezi sita bila fursa ya kulipa faini.

Mshtakiwa, akiwa hajaridhika na uamuzi wa Mahakama Kuu, alikata rufaa tena katika Mahakama ya Rufaa.

Matokeo yake akabakizwa Gerezani na kuhamishiwa Dar es Salaam katika gereza la Segerea ambapo amebaki Mahabusu bila kesi wala hukumu yoyote hadi leo.
images (1).png
 

Attachments

Back
Top Bottom