Nini kipo nyuma ya ukuaji na ongezeko la watu wasiokuwa na dini?

Nini kipo nyuma ya ukuaji na ongezeko la watu wasiokuwa na dini?

isajorsergio

Platinum Member
Joined
Apr 22, 2018
Posts
4,143
Reaction score
6,560
Habari 👋🏾

Nimefanya tafiti katika vipindi, nyakati na maeneo tofauti na inaonekana wazi ushawishi wa dini unapungua kwa kasi kubwa sana.

Inaonekana wengi kutokuwa na hakika katika dini mbalimbali na wengi wao bado wanajaribu kujionesha katika ngwe hiyo kwa sababu kadhaa ikiwemo kutokataliwa na jamii hizo.

Je, ni ipi sababu ya ukuaji wa kiwango hiki cha watu kutokuwa na dini kama ilivyozoeleka?
 
Makanisani siyo sehemu tena ya kupata faraja. Ila pia watu wengi wamekuwa wanareason kila kitu tofauti na zamani watu walikuwa na reasoning power ndogo so wanaona inayoendelea kule ni miyeyusho miyeyusho tu.
Unamaanisha dini ni sehemu ya watu wasiokuwa na uwezo wa reasoning? Ni yapi ambayo yamefichwa kwa watu wasiokuwa na uwezo huo?
 
Dini zipo kwa ajili ya watu wenye uwezo mdogo kufikiri!!!!Lakini kama utafikiri kwa makini utaona mkanganyiko na mianya mingi yenye utata kwenye hizo zinazoitwa Dini!!
Nimekuelewa Kwa uzuri, mfano wa mikanganyiko hiyo ni utengano na madaraja kwa binadamu. Unaweza kuongeza mikanganyiko mingine tuweze kujifunza?
 
Ushawishi umepungua maaana watu haweindi kanisani kwasbb ya uviko 19
UVIKO-19 ndio sababu ya watu kuacha kuhudhuria kanisani?

Imekaririka ikisemwa kanisani utaponywa kila maradhi na hakuna tatizo likatizalo mbele ya madhabau ya bwana kunani tena UVIKO-19 aivunje mipaka hii?
 
Nimekulewa Kwa uzuri, mfano wa mikanganyiko hiyo ni utengano na madaraja kwa binadamu. Unaweza kuongeza mikanganyiko mingine tuweze kujifunza?
Mfano wewe hapo uishi miaka 70 halafu eti umetenda dhambi ukachomwe moto milele yaani hakuna mwisho wa kuchomwa wakati wewe umejiishia miaka 70!

Wakati huo huo atakaekuchoma huo moto anahubiriwe ndie Mwenye upendo mkubwa kuliko viumbe vyote!

Halafu akamuumba malaika mmoja mkuu halafu huyo akafanywa kuwa shetani atudanganye sisi ili tukachomwe moto. HEBU FIKIRIA KWA MAKINI KAMA ITAKUINGIA AKILINI AISEH
 
Back
Top Bottom