Nini kitatokea baada ya Magufuli kustaafu Urais?

Nini kitatokea baada ya Magufuli kustaafu Urais?

Na mimi huwa najiuliza je, waliokuwa wanamsifia kama kina pole×2 wataendelea kumsifia? Na je kwakuwa watu wamefungwa midomo kwa kuogopa utawala wake je kama akitoka madarakani (sina uhakika) atakuwa na uvumilivu wa kupigwa spana ?[emoji4][emoji4]. NA JE WABUNGE WALIOPITA BILA KUPINGWA JE WATAPATA MTU WAKUWAPA FAVOUR AU LIFT YA KUPITA BILA KUPINGWA? haya ni maswali huwa najiuliza sana mara kwa mara.
 
Mkuu, mi nadhani umeipaka bendera yetu rangi nzuri kuliko uhalisia wenyewe. Twende taratibu kidogo kidogo, pengine tutafika huko tunakokupenda sote hatua kwa hatua.
Sema jambo mkuu wangu 'tindo', maanake jahazi hili ni letu sote. Linapozama, sote tunakunywa maji.

cc: tindo
 
Habari wadau wa JF siasa.

Nimekuwa nikiwaza Sana sura ya nchi na hali ya nchi hii baada ya Rais Magufuli kumaliza mihula yake miwili. Je nchi itakuwaje kirushwa na kifisadi, kiuchumi, kisiasa, kimaendeleo nk?

Ajaye atakuwaje na atatupeleka wapi na jamii ya Kitanzania kipindi hicho kitakuwaje?
Uwanja wa chato kuota nyasi na mbuga ya buriji kuwa zoo ya mtu binafsi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona tupo pamoja mkuu, au hukuelewa nilichoandika hapo?

Nashukuru wewe umepata muda mzuri wa kufafanua mkakati mzima. Huyu hana mpango wa kutoka hapo alipo kwa hiari yake.
sitaki kukulisha maneno ila lisemwalo lipo
tuweke akiba ya maneno, na tujiandae kisaikolojia
1612082993579.png
 
sitaki kukulisha maneno ila lisemwalo lipo
tuweke akiba ya maneno, na tujiandae kisaikolojia
View attachment 1690638
Kwa bahati nzuri au mbaya mkuu, hili halinishtui kabisa kwani nalitarajia siku yoyote litokee.

Kitakachonishangaza ni sababu zipi waanze na hako ka miaka saba? Au wanamwachia mwenyewe afanye 'testing' kwanza kabla ya kuamua 'full blast' ya akina Kagame na M7?
 
Nchi itakuwa kwenye madeni makubwa
Nchi itakuwa kwenye umasikini.
Magufuli anaua uwekezaji, anaua ajira nchini kwa sababu zisizo na kichwa wala miguu.
Hivi huyu mwekezaji hapa chini kosa lake ni nini?

View attachment 1690196
Afanye hivyo kwa walimu na vyuo na shule binafsi ili tujue kama yeye ni mzalendo kweli
 
Sijui kama umeuliza hili swali ukitaka kupata jibu!

Wewe unadhani ni nani anayo madaraka ya kumwamulia. Huyo mtu anazo bunduki na mabomu na mapolisi?
Wananchi kupitia Katiba,kama hii katiba haiwezi kufanya hivyo kuna haja ya kuandika nyingine maana huo ndiyo msingi wa nchi.
 
Habari wadau wa JF siasa.

Nimekuwa nikiwaza Sana sura ya nchi na hali ya nchi hii baada ya Rais Magufuli kumaliza mihula yake miwili. Je nchi itakuwaje kirushwa na kifisadi, kiuchumi, kisiasa, kimaendeleo nk?

Ajaye atakuwaje na atatupeleka wapi na jamii ya Kitanzania kipindi hicho kitakuwaje?
Katiba ya nchi inayo majibu
 
Wewe ndiye huwajui kabisa ccm! Zanzibar waligwaya Kamando alipotaka kubadilisha katiba aendelee. Jahazi likaokolewa na baba wa taifa.

2015 ccm unayozungumzia ilizikwa rasmi na Twende kupiga kura asiyetaka na abaki. Ccm ambayo haijasema kilichomtokea Mangula hadi leo! Wako pamoja wote hawako wote pamoja! Dhana ya chukua chako mapema ni sasa. Ccm ya watu sio watu wa ccm. Inatumiwa tu kwa maslahi. Hakuna mfia ccm tena.
Mi ninachojua huyu jamaa harudi kamwe akimaliza muhula wake...
 
Habari wadau wa JF siasa.

Nimekuwa nikiwaza Sana sura ya nchi na hali ya nchi hii baada ya Rais Magufuli kumaliza mihula yake miwili. Je nchi itakuwaje kirushwa na kifisadi, kiuchumi, kisiasa, kimaendeleo nk?

Ajaye atakuwaje na atatupeleka wapi na jamii ya Kitanzania kipindi hicho kitakuwaje?
Cha kwanza ni kumtupa rupango DAB kwa kutumia vyeti feki
 
Nchi itakuwa kwenye madeni makubwa
Nchi itakuwa kwenye umasikini.
Magufuli anaua uwekezaji, anaua ajira nchini kwa sababu zisizo na kichwa wala miguu.
Hivi huyu mwekezaji hapa chini kosa lake ni nini?

View attachment 1690196
Tutaanza chato tunaondoa taa zote za barabarani,tutafunga maofisi yote, chato airport italimwa mbogamboga
 
Wananchi kupitia Katiba,kama hii katiba haiwezi kufanya hivyo kuna haja ya kuandika nyingine maana huo ndiyo msingi wa nchi.
LOoo, mkuu Gellangi, umenimaliza nguvu kabisa na haya mawazo yako hapa.

Naona wewe mwenzetu unaishi nchi tofauti kabisa na hii tunayoishi wenzio.

Huko kwenu naona mnao uhuru kamili wa kuyafanya hayo unayoyasema. Hapa tulipo maamuzi ni ya mtu mmoja tu. Kila anachotaka yeye ndicho hicho tutakachopata. Sijui tutamshawishi vipi aweze kuruhusu mambo kama ya huko kwenu hapa kwetu.

Huko kwenu huo mchakato wa katiba mpya mtauanza lini mkuu?

Uzuri wa JF ni kwamba unakutana na watu wenye ufahamu mwingine kabisa usiotegemea kuwa bado wapo wanaoamini wanayoyaandika.
 
Hahaaaa!!!huyu bwana kunanga wenzake anapenda sana ngoja zamu yake ifike
Atagombana na mrithi wake kwa kuwa hana kifua cha kuvumilia vijembe vya Wapambe wa Rais ajae.

Cyprian Musiba wa Awamu ya 6 atakuwa anam provoke nae 'atajaaa'.

JK alitumia busara na subira ya hali ya juu sana kukwepa kuchonganishwa na Mrithi wake, sijui kama Yeye atakuwa na hicho kifua kama cha Jk
 
Back
Top Bottom