Nini msingi wa Mahabusu kujisaidia kwenye ndoo?

Nini msingi wa Mahabusu kujisaidia kwenye ndoo?

Sijui kwanini wabunge huwa hawapigii kelele mambo kama haya yanayomgusa kila Mtanzania wa chini. Hii pia ni kete nzuri mno kwa wapinzani ila hawaitumii vizuri. Sijajua kwanini.
Niombe wapinzani wa kweli kweli wawe wanasoma hili jukwaa ili sera zao zipate madini Safi kutoka humu.
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Ni hali ya kumpa adhabu mtuhumiwa.
Kwa ulimwengu huu hii ni aibu kubwa kwa taifa ambalo mahabisu zake Bado zinatumia ndoo kwenda haja.
 
Mahabusu ya kawe ina choo ila hakina mlango wala faragha yoyote, pia ni kichafu had sinki la choo limekuwa jeusi, kuna bomba ila halitoi maji, kuna dumu la lita 20 ila halina maji hata tone, hamna kopo la kunawia wanatumia chupa za maji ya kunywa kunawia na kubwa kabisa ni hicho choo kimejaa, hata ukikojoa tu mkojo wote unakuja juu hapo hujatoa haja kubwa na hapo ni kawe tu na sio mbali kilomita 1 kutoka dawasco kawe.
 
Siku hizi ni vyoo bana hakuna ile mitondoo..tena
 
Mahabusu ya kawe ina choo ila ni kichafu had sinki la choo limegeuka jeusi, kuna bomba ila halitoi maji, kuna dumu la lita 20 ila halina maji hata tone, hamna kopo la kunawia wanatumia chupa za maji ya kunywa kunawia na kubwa kabisa ni hicho choo kimejaa, hata ukikojoa tu mkojo wote unakuja juu hapo hujatoa haja kubwa na hapo ni kawe tu na sio mbali kilomita 1 kutoka dawasco kawe.
Uko sawa nlishalazwa pale ni shida kwa kweli.na milango hakuna
 
Mahabusu ya kawe ina choo ila ni kichafu had sinki la choo limegeuka jeusi, kuna bomba ila halitoi maji, kuna dumu la lita 20 ila halina maji hata tone, hamna kopo la kunawia wanatumia chupa za maji ya kunywa kunawia na kubwa kabisa ni hicho choo kimejaa, hata ukikojoa tu mkojo wote unakuja juu hapo hujatoa haja kubwa na hapo ni kawe tu na sio mbali kilomita 1 kutoka dawasco kawe.
Kibongo bongo hata majumbani hali ziko hivi.

Sasa ukizingatia kwamba watumishi wa serikali wanatoka kwenye jamii hii hii. Huwezi kushangaa ya mahabusu na jela.
Mwaka 2016 nilikutana na Jamaa aliyetaka kuzamia Ulaya kwa kupitia Somalia, Sudani hadi Mediterania. Alikamatwa hana nyaraka. Akatupwa Jela Libya.

Alinisimulia Jela za Libya kwa miaka hiyo ya 2010 ilikuwa kama Nyumbani kwa Afisa wa ngazi fulani hapa kwetu.

Kuna vyoo safi, Redio na TV.

Kuna Gym na Chakula safi. Unachonyimwa ni Uhuru wa kujumuika na jamii na kufanya shughuli zako tu.

Huduma zote za msingi za kibinadamu zinapatikana nzuri sana kuliko Mamilioni ya Watanzania ambao wako Huru na Uraini
 
UPUMBAVU WA NGOZI NYEUSI KURITHI ADHABU ZA KIKOLONI.

SHENZI KABISA.
 
Kuna Gereza Rais aliwahi kutembelea hapahapa TZ alikuta wafungwa wanalala sehemu safi, ila inasemekana yule mkuu wa Magereza aliposikia kuna ugeni wa Rais aliamua kuwawekea wafungwa magodoro mapya na net ili Rais aone kwamba wafungwa wanalala sehemu nzuri ingawa inasemekana Rais alivyoondoka tuu yale magodoro yalitolewa yakarudishwa store wafungwa wakaendelea kulala chini kwenye kunguni
 
Back
Top Bottom