Nini Sababu: Mume amehama ghafla na kwenda kupanga bila ugomvi wala maelezo yoyote

Kuna point hapo, kiukweli jamaa ni mkavu Kama Hana kilichotokea, juz TU hapa katoka kuwalipia wanae wote ada bila wasiwasi kabisa.
Achaa afanye kile kwake anachoona ni sahihi Kwa wakatii huu ,mpk pale atakapokaa sawaa 😄
 
Huwezi linganisha ndoa na tabia za watoto, ndoa zina mambo magumu sana mtu akiongea utashangaa huyu si huwa yupo happy muda wote , kumbe huko ndani kwake ni sarakasi za kutosha
 
Ujue umenifumbua kitu flani hivi, na mchepuko wangu mmoja hivi, kipind nnachokua nmegombana nae Kila mtu kivyake, ndo kipind Ile miradi viporo niliyoitelekeza napata Ela na akili ya kuifufua. Na kweli Huwa inafufuka.

Tukirudiana TU, naanza upya kutelekeza miradi
 
Pigia mstar pale alipopigiwa simu na askofu akamtukana!!!

Haihitaji kwenda cuba
Kwamba askofu kamla mkewe, mbn Kama haiingii akilini mkuu, MKE WA jamaa mlokole na anajiheshim Sana yule.
 
Akili mtu wangu. Haya mambo haya bwana we acha tu
 
Huwezi linganisha ndoa na tabia za watoto, ndoa zina mambo magumu sana mtu akiongea utashangaa huyu si huwa yupo happy muda wote , kumbe huko ndani kwake ni sarakasi za kutosha
Nimeweka mfano wa watoto alama ya nafsi isiyoridhika baada ya kukosa udhibiti.......

Wale walioamua au kuchagua kuishi na mwenza sio kama wamefungwa matamanio bali wamefanikiwa kuyadhibiti matamanio
 
Kwamba askofu kamla mkewe, mbn Kama haiingii akilini mkuu, MKE WA jamaa mlokole na anajiheshim Sana yule.
Hao hao wanaojiheshimu behind the scene utakimbia

Trust me hapo pana ishu kubwa sana ya usaliti,si kawaida kwa mwanaume kufanya maamuzi magumu kiasi hicho

Kama ukitaka kujua ukweli wa hilo,mwambie mkeo afanye kazi ya ziada aongee na mwanamke mwenzake ukweli utajulikana tu
 

Kwa red hapo.......
Labda anafanya mipango ahamie upande wa pili...
 
Binafsi nachoona kwanza Jamaa ni wale watu wasiri sana, wenye hulka ya upole na ukimya. Mtu wa aina hyo sio rahisi kufungua kifua chake kujua aloyaficha.
Kikubwa inakubidi kwanza ww msuluhishi uwe na uwezo wa kusoma Saikolojia ya mtu, unamuhoji na kuongea naye je unavyomuona anayoongea yanatoka moyoni (ya ukweli)?, au anaongea ili tuu uridhike mada iishe? Ukizingatia hilo utajua nn kinaendelea.
*
Mke angekuwa muelewa na mvumilivu angekausha asubiri huo muda ambao jamaa kasema atarudi akimalza mambo yake, ikiwa jamaa haachi kupeleka matumizi home basi bdo anaipenda familia yke, angekuwa hawataki asingepokea simu na mawasiliano na wala matumizi asingepeleka home. Mke huenda anapanik kwa kukosa haki yke ya ndoa, basi angefnya utaratibu na mumewe awe hta anaenda kupeana huko jamaa alipo, huku mke akisubiri muda wa jamaa kurejea home.
*
Tumia njia ya kufanya mawasiliano na wazaz wake kuwachimba kiundan lazma kawaambia lengo lake ama yale yanayomsibu, ila ww anashndwa kukweleza Coz ww n rafiki tuu na upo karibu na mkewe huenda siri yke itafika asipotaka ifike.
*
Mtumie mkeo kumdadisi kiundan mke w jamaa, huenda kuna dalili jamaa aliziona kwa mkewe (kiusaliti, shirikina n.k) ambazo jamaa hajazipenda na kwakuwa dini yke haimtaki kuachana mpaka kifo anaona hyo ndo njia sahih ya kukaa mbali na mkewe.
*
Mwisho; ukiona ktk hayo bdo hupati muelekeo, kaa kimya usiendelee kumuuliza jamaa kuhusu hilo suala maana huenda ukawa wamkera na baadae mkaja kutia dosari urafiki wenu.
 
Huyo jamaa ni kama mimi tu, siwezi kumwambia mtu yoyote upuuzi wa mke wangu, nikishasema tu sioni sababu ya kuendelea kuishi nae na nikisha achana na wife sioni bababu ya kuongea chochote.

Huyo mwanamke anajua sababu kwanini hadi kaachwa ila hataki kusema yeye anataka eti aliyekuwa mume wake ndo aseme.
 
Ameamua kujipa likizo kwa muda ila nadhani mkewe atakua anajua ndio maana anapata presha presha za hapa na pale, kama alichat na akasahau kufuta now kimemramba... Wengine hawana muda na drama za mapenzi.
 
Pia, KUISHI NA MKE WA MTU NYUMBANI KWANGU, KIUKWELI binafsi nijistukia kua kimaadili HAIKAI VIZURI kabisa.

Mpeleke kwa wazazi wake au ndugu zake. Siku akitokewa na mengine huku labda pia ndio muda wa kutolewa kafwalwa basi yatakukuta wewe msamaria mwema, jirani mwema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…