Nini Sababu: Mume amehama ghafla na kwenda kupanga bila ugomvi wala maelezo yoyote

Mwanamke anatabia ambazo hazimpendezi mume japo mume kaamua kuzistiri ila mwanamke amelikuza hadi ustawi wa jamii hapa njia pekee ya kumrudisha ni MSAMAHA wa dhati na kubadilika
 
Hapo kuna mambo mawili ninavyohisi

1. Kamchoka mkewe, inawezekana ikawa huyo mkewe hajamkosea bali yeye tu kamchoka, sometimes distance inasaidia wamuache tu wasimsumbue huko kumshitaki ndio kunaharibu kabisa

2. Labda ana mambo ya kishirikina, huwezi jua anachofanya usiku huko alipo au labda kuna mambo mganga kampa maelekezo. Labda hataki mtu ajue siri zake.

Moyo wa mtu kichaka, huyo mkewe mwambie arudi kwake tu akubaliane na hali halisi na muombe asikushirikishe tena wewe mambo yao
 
Mwanaume kama mwanaume hawezi kukurupuka bila sababu ya msingi akimbie familia, Huyo mwanamke kuna kosa kalifanya na analijua kosa lake vizuri ila tatizo lao wanawake hawakubali hata siku moja kama wao ndio chanzo cha tatizo zaidi ya kuplay victim.

Jamaa anaweza kurudi kama ana moyo wa kusamehe lakini pia anaweza kutokomea mazima ikabaki anatunza familia kwa hiyo pesa ya matumizi.


Tukatae ndoa tu.
 
Huyo sio mzima,mwanayme kamili hawezi kumaliza miezi sita bila kula mzigo
 
Hii kali mkuu!
Ebu tusubiri tuone. Yawezekana mke anampa stress.
Na hataki kusema.
 
Ndugu wakigombana,nenda ukalime,wakipatana chukua kapu ukavune
 
Mwanamke kalegezewa sana kwenye jamii kwa sasa....

Mambo ya haki sawa yanawafanya wanawake waone kama maisha ya ndoa ni sehemu ya luxury, kumbe ndoa ina majukumu mengi sana.
Wanawaza kuwatapeli Tu waume Zao ndio maana sisi wengine KATAA NDOA NI UTAPELI
 
Huyo sio mzima,mwanayme kamili hawezi kumaliza miezi sita bila kula mzigo
Haya maswala ya changamoto za ndoa ukiya tizama unaweza sema wanayo wakuta ni wajinga, ila ukiingia deep unaweza ukauta mwamba kaamua kujipa muda.Kuna kitu kinaitwa mental health huwezi jua jamaa ndio anakipitia, hivi vitu husimkejeli mtu maana havijakukuta.
 
Mimi yalishanikuta mara mbili.mke wa kwanza alikuwa mzungu,wapilimchaga,huyu nchaga kidogo niue mtu aliyekuwa akimpa kiburi,niliondoka na nguo zangu tuna kuanza upya,ila ili kujifariji niligeuka playboy,malaya pro max
 
Hii ni hali ngumu sana, na inaonyesha kwamba mume huyo ana jambo zito anapitia, lakini hataki kulieleza kwa mtu yeyote.

Kama ameweza hata kumtukana askofu na kukaidi wazazi, huenda hakuna mtu ambaye anamheshimu vya kutosha kumshauri.

Tafuta mtu mmoja ambaye unahisi anaweza kumvuta sikio na kusikilizwa (rafiki wa karibu, mkubwa wake kazini, au mtu anayeaminiwa sana na familia yake

Kama ameanza ujenzi wa nyumba mpya, huenda ameshaamua kuanza maisha mapya mbali na familia yake.

Badala ya kumlazimisha kurudi, jaribu kumpa nafasi ya kueleza nia yake halisi kwa njia isiyo ya kumshinikiza.

Kuhusu kukaa na mke wa mtu

Umefanya jambo la utu kwa kumsaidia mke wa jirani yako, lakini kwa upande wa maadili, ni vyema kutafuta njia mbadala ili asikae kwako kwa muda mrefu. Pengine washirikishe ndugu wa karibu wa mkewe ili wamsaidie kwenye kipindi hiki kigumu.

Mkewe anaonekana kuwa kwenye hali mbaya ya msongo wa mawazo. Tafuta namna ya kumshauri akapate ushauri wa kitaalamu kwa sababu hali hii inaweza kuathiri afya yake kwa kiwango kikubwa.

MWISHO JAPO SI KWA UMUHIMU HUYO MWANAMKE ANAJUA KWANINI MUME WAKE HAATKI KURUDI NYUMBANI, AU KAMA HAJUI HUYO MWANUME HUENDA KUNA MAAGANO AMEINGIA YA KISHETANI HIVYO AKATAKIWA ASIKAE NA MWANAMKE
 
Mimi yalishanikuta mara mbili.mke wa kwanza alikuwa mzungu,wapilimchaga,huyu nchaga kidogo niue mtu aliyekuwa akimpa kiburi,niliondoka na nguo zangu tuna kuanza upya,ila ili kujifariji niligeuka playboy,malaya pro max
Kuna watu wengine may be wapo hivyo sababu ya dini.
 
Tulishauriana na wife amsihi aende kwao, hataki kabisa, pia kumforce akarudi kwake inakua Kama tunamfukuza kisa ana matatzo, kitu ambayo Kama haisound vzuri
Hapa kuna tatizo. Tafuta ndugu zake wamchukue. Hatujui siku ya kufa, lakini ghafla amefia hapo kwako unaweza kupata changamoto ya kuhusika na upelelezi
 
Aise hata mm npo radhi nimuachie mwanamke na watoto nyumbaa nikaanze upya .....huyu jamaaa yupo sahihi kabisa
 
Watoto wanne kabisa, Tena wakubwa, WA mwisho Yuko darasa la nne
basi hapo ndo kwenye shida ndio maana mwanaume kaona akae kando ili asije akafanya jambo kubwa likawashangaza. Mungu amsaidie.
 
Kuna mengi sana wanandoa wanapitia,pande zote mbili,kuna +ve na -ve

Kuna kitu kwa sasa kinavunja sana ndoa,saaana yaaani..

Wake zetu hawa wanao okoka ama kutumia muda mwingi kanisani.....kuna kosa moja kubwa sana wanafanya ila hawajui,wanajenga ukaribu sana na kuwaamini hawa wachungaji,watumishi,walimu,pasta,padri etc kuliko mumewe ndani kiasi kwamba analeta nyumbani yale anayo ambiwa huko na anaanza kumwamwini mchungaji wake kuliko mumewe,kinachotokea kwa mume ni kuona anashushwa thamani yake kama baba ndani nafasi hiyo anachukua mtu flan na hili linawala sana wanaume moyoni.
Kuna case moja nawatolea mfano..

Kuna mshikaji mkewe anasali haya makanisa ya kiroho,anashughuli zake halali akimaliza anazama kanisani kwa pasta,kuna wakati jamaa akapata changamoto kidogo,kapiga mchepuko akafanya yake akirudi kwa mama ngoma(dushe) inasua sua kusimama,mke akaja na ushauri kaongea na mchungaji kuhusu hilo swala kwa hiyo mumuwe aende wakaongee kiume na mchungaji....nnavyoandika hapa ndo ili ingia kwenye misukosuko balaa,mwamba anaamin mke analiwa na mchungaji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…