Yeah, wanasema SAUTI YA WENGI NI SAUTI YA MUNGU kwa wale wanaoamini.
Nadhani wengi wako kwenye ule umri wa kufanya makosa(16 - 28) na ama hawana muongozo sahihi au hawako tayari kuongozwa. Watakapofikia ule umri wa kuangalia nyuma na kutamani kurudi pale walipokosea ili warekebishe, inakuwa too late, wanaanza kuuishi ujinga ule kwa taaabu sana katika jamii.
Mama mmoja mtaani, ni wa heshima sana, hakuwahi kuonekana amevaa nguo ya mikono mifupi, kumbe ni mkakati wa kuficha tattoo iliyoko mkono wa kushoto, juu tu ya kiganja. Nilipoiona kwa bahati mbaya, aliniangalia kwa upole, nikaona aibu mimi, sijui kwanini. Ila naamini anajutia.
Monalisa, anasema jambo analojutia, ni kuchora tattoo begani