Nazungumzia Lindi na Mtwara haswa!
1. Kule husikii albino amechinjwa
2. Kule husikii wenye macho mekundu wameuawa kisa ni wachawi,
3. Kule husikii wenye upanja wamepigwa nondo ili zikatumike buchani
4. Kule husikii mtu amechunwa ngozi
5. Kule ni nadra kusikia wazazi, sijui mama, kutolewa uhai ili kuleta utajiri
6. Kule ni nadra kusikia makabila au koo wamepigana na kutoana uhai (ingawa kuna makabila mengi tu na yanapishana wakati mwingine),
7. Kule ni nadra kusikia mauaji ya kinyama kwa kisa cha mapenzi au kudaiana fedha
8. Kule ni nadra kusikia babu sijui mjomba amembaka mjuu/mpwa,
9. Kule ni nadra kusikia visa vya mabinti kutupa watoto chooni,
10. kule ni nadra kusikia binadamu ananyofolewa viungo ili vikauzwe vilete utajiri
11. Kule ni kawaida mgeni ukapokelewa na kuishi kama wananchi wengine bila wasiwasi n.k.
Wakati hali ikiwa hivyo, maeneo mengine kuna utofuti sana.
-Mauaji. JF kwa siku karibia nne au tano leo zimejaa thread za mauaji tu kwa visa vya mapenzi n.k. kisa cha hivi karibuni kuripotiwa ni hicho kilichotokea Tabora
-Ubakaji
-Utupaji wa watoto
-Ushirikina, kuna maeneo wazee eti wanakaa kabisa na kufanya tambiko ambapo mgeni anauawa kama kafara (mwalimu mmoja wa sekondari alikutana na dhahama hii sehemu fulani, alifuatwa akauawa na mwili wake kuchukuliwa kwenda kufanyiwa tambiko). pia, maeneo mengine tunaona na kusikia jinsi makaburi yanavyoenda kufukuliwa na maiti kutolewa na kurudishwa ilikotoka.....wafiwa wanaamka asubuhi wanakuta wamewekewa maiti ya ndugu yao waliomzika jana uwanjani.
na vingine vingi
Wajuzi/wafuatiliaji/ wasomi; sababu kubwa haswa ya hali hii ni nini? dini au?
Karibuni kwa uelimishaji.