Vizee vya kule hatariKwa mtu asiefahamu Mtwara pananuka ulozi..
Mimi kwa mara ya kwanza nilishindana na Nguvu za giza nikiwa Mtwara, huko ndipo nilijua Mapambano katika ulimwengu wa roho yapoje..
Nimeishi Kusini wakati flani.. kwa kweli ni Sehemu Salama sana. Wenyeji wako poa hawana Ubaguzi wala Tatizo na Mgeni wa hali yoyote ile kiuchumi.Nazungumzia Lindi na Mtwara haswa!
1. Kule husikii albino amechinjwa
2. Kule husikii wenye macho mekundu wameuawa kisa ni wachawi,
3. Kule husikii wenye upanja wamepigwa nondo ili zikatumike buchani
4. Kule husikii mtu amechunwa ngozi
5. Kule ni nadra kusikia wazazi, sijui mama, kutolewa uhai ili kuleta utajiri
6. Kule ni nadra kusikia makabila au koo wamepigana na kutoana uhai (ingawa kuna makabila mengi tu na yanapishana wakati mwingine),
7. Kule ni nadra kusikia mauaji ya kinyama kwa kisa cha mapenzi au kudaiana fedha
8. Kule ni nadra kusikia babu sijui mjomba amembaka mjuu/mpwa,
9. Kule ni nadra kusikia visa vya mabinti kutupa watoto chooni,
10. kule ni nadra kusikia binadamu ananyofolewa viungo ili vikauzwe vilete utajiri
11. Kule ni kawaida mgeni ukapokelewa na kuishi kama wananchi wengine bila wasiwasi n.k.
Wakati hali ikiwa hivyo, maeneo mengine kuna utofuti sana.
-Mauaji. JF kwa siku karibia nne au tano leo zimejaa thread za mauaji tu kwa visa vya mapenzi n.k. kisa cha hivi karibuni kuripotiwa ni hicho kilichotokea Tabora
-Ubakaji
-Utupaji wa watoto
-Ushirikina, kuna maeneo wazee eti wanakaa kabisa na kufanya tambiko ambapo mgeni anauawa kama kafara (mwalimu mmoja wa sekondari alikutana na dhahama hii sehemu fulani, galifuatwa akauawa na mwili wake kuchukuliwa kwenda kufanyiwa tambiko). pia, maeneo mengine tunaona na kusikia jinsi makaburi yanavyoenda kufukuliwa na maiti kutolewa na kurudishwa ilikotoka.....wafiwa wanaamka asubuhi wanakuta wamewekewa maiti ya ndugu yao waliomzika jana uwanjani.
na vingine vingi
Wajuzi/wafuatiliaji/ wasomi; sababu kubwa haswa ya hali hii ni nini? dini au?
Karibuni kwa uelimishaji.
Mbeya wana Majungu sana na Unafiki. Mnyakyusa mtu mnafiki sanaa. Anakuchekea usoni kumbe moyoni hataki hata kukuona. Mbeya ni kwetu nalielewa hilo jambo haswaaUmeisahau na Mbeya.
Hamna hayo mambo.
Mmmmh kama kuna ukweli hivi!!AWa
Watu wa kusini wamejawa na maadili ya Dini hiyo ndo sababu Kuu,na ukimuona Katili basi huyo ni wale waliovuka kutoka kwa mreno
OMG wapi huko, nimeshtuka mno bro!Kitaya wanajeshi wetu walipokatwa vichwa unapajua??
Kuna kaukweli kiasi bt ushirikina ,uchawi ndo home huku...misukule na chuma uletee ndo penyewe.Nazungumzia Lindi na Mtwara haswa!
1. Kule husikii albino amechinjwa
2. Kule husikii wenye macho mekundu wameuawa kisa ni wachawi,
3. Kule husikii wenye upanja wamepigwa nondo ili zikatumike buchani
4. Kule husikii mtu amechunwa ngozi
5. Kule ni nadra kusikia wazazi, sijui mama, kutolewa uhai ili kuleta utajiri
6. Kule ni nadra kusikia makabila au koo wamepigana na kutoana uhai (ingawa kuna makabila mengi tu na yanapishana wakati mwingine),
7. Kule ni nadra kusikia mauaji ya kinyama kwa kisa cha mapenzi au kudaiana fedha
8. Kule ni nadra kusikia babu sijui mjomba amembaka mjuu/mpwa,
9. Kule ni nadra kusikia visa vya mabinti kutupa watoto chooni,
10. kule ni nadra kusikia binadamu ananyofolewa viungo ili vikauzwe vilete utajiri
11. Kule ni kawaida mgeni ukapokelewa na kuishi kama wananchi wengine bila wasiwasi n.k.
Wakati hali ikiwa hivyo, maeneo mengine kuna utofuti sana.
-Mauaji. JF kwa siku karibia nne au tano leo zimejaa thread za mauaji tu kwa visa vya mapenzi n.k. kisa cha hivi karibuni kuripotiwa ni hicho kilichotokea Tabora
-Ubakaji
-Utupaji wa watoto
-Ushirikina, kuna maeneo wazee eti wanakaa kabisa na kufanya tambiko ambapo mgeni anauawa kama kafara (mwalimu mmoja wa sekondari alikutana na dhahama hii sehemu fulani, alifuatwa akauawa na mwili wake kuchukuliwa kwenda kufanyiwa tambiko). pia, maeneo mengine tunaona na kusikia jinsi makaburi yanavyoenda kufukuliwa na maiti kutolewa na kurudishwa ilikotoka.....wafiwa wanaamka asubuhi wanakuta wamewekewa maiti ya ndugu yao waliomzika jana uwanjani.
na vingine vingi
Wajuzi/wafuatiliaji/ wasomi; sababu kubwa haswa ya hali hii ni nini? dini au?
Karibuni kwa uelimishaji.
SIO KWELI KABISA NILIWAHI FIKA NACHINGWEA NIKAPOKELEWA NA KWA UKARIMU WA AJABU SANA,HAKIKA KUSINI KUNA UKARIMU WA AJABU SANA./SEREKALI ITUPIE JICHO HUKO KIMAENDELEO KUWEKWE MSUKUMO MAALUMWanauana kishirikina kuna sehemu imaitwa ngende
Inawezekana pia hali siyo shwari kama tunavyofikiria ila mawasialiano ndiyo yanasababisha tusipate habari nyingi za huku. Hii mikoa bado iko nyuma sana. Ila nikiri kuwa watu wa huko hawana mambo ya tamaa ya mali kama mikoa mingine. Kule mtu akipata sex na chakula anaona ameshamaliza shida zote za maisha.... sidhani kama ni dini. Maana dini hizo hizo zilizoko kusini ndio hizo hizo zilizoko maeneo mengine ya nchi. Mbona hatusikii mauwaji ya kijnga kama hayo yakitokea Ulaya?
Hii inaweza kuwa moja ya sababu.Unauhakika kuna watu wa media wa kutosha uko kama mikoa mingine kotosikia haimaanishi havitendeki nimetembelea kijiji fulani nakutana na uozo lkn hausikiki kwenye media
Maeneo ya pwani huwa yanastaarabika mapema zaidi kuliko bara kwa sababu ya muingiliano mkubwa na watu wa mataifa mengine na pia wana fursa ya muingiliano mkubwa na makabila mengine ya bara.... sidhani kama ni dini. Maana dini hizo hizo zilizoko kusini ndio hizo hizo zilizoko maeneo mengine ya nchi. Mbona hatusikii mauwaji ya kijnga kama hayo yakitokea Ulaya?
Kwani sehemu zingine hazina dini?Ustaarabu na dini imesawasaidia sana huku ukanda wa pwani
HahahahahNiliwahi kwenda huko nikiwa sina ndugu wala rafiki ila wale watu ni waungwana mno wana madhaifu mengine ila huko ni sehemu salama kuishi na kuolewa/kuoa huwezi chinjwa kikatili