Nini status ya Baraza la Mawaziri la Magufuli sasa na baada ya Samia Suluhu Hassan kuapishwa?

Mama kama anataka kweli ajijengee imani kwa Watanzania wengi, alivunje tu hilo Baraza lililojaa wanafiki, wachumia tumbo na waimba mapambio.

Na Majaliwa asiachwe kuendeleza uongo wake! Naye abakie tu na Ubunge wake.
Kumbe na ubunge wenyewe ulipatikana kwa mbinde!

Watu wanajiharibia sifa zao kijingajinga tu.

Nilimheshimu huyu jamaa, kumbe na yeye ni 'bogus'?
 
Viongozi wote wakuu lazima wale kiapo mbele ya rais.
Hawa waliopo waliapa mbele ya Magu na sio mama Samia. Hivyo lazima baraza lipigwe chini. Hiyo itashuka hivyo hadi kwa ma Rc, IGP, CDF, TISS..... Hivyo....
Samia akitaka ajiondolee lawama na visingizio, ni lazima apange safu yake upya kabisa!

Hii haina maana atawatupa wote waliokuwemo kwenye serikali ya Magufuli.
 
Mama Samia anamalizia ngwe waliyoanza na John Pombe Magufuli

Yeye ataanza ngwe yake kamili kwake 2025-2035

Mungu wa mbunguni amtunze
Hapana, miaka ikizidi mitatu katika muhula umeutumikia kama Naibu, huhesabika umeutumikia mihula mzima wa miaka mitano.
 
Lazima tuanze upya!

Ila punguzeni expectations kwa huyu Mama..

Kumbukeni CCM ni ile ile kama usemavyo wimbo wao ule wa kampeni
Akiendeleza upumbavu ulio kuwepo, na yeye atadharauliwa na kuombewa mabaya. Simshauri kuchagua njia hiyo mbaya ya kuwasikiliza zaidi wanafiki na wachumia tumbo.
 
Afadhali alivunje ili tuanze upya
 
Naunga mkono
Mama kama anataka kweli ajijengee imani kwa Watanzania wengi, alivunje tu hilo Baraza lililojaa wanafiki, wachumia tumbo na waimba mapambio.

Na Majaliwa asiachwe kuendeleza uongo wake! Naye abakie tu na Ubunge wake.
hoja hili baraza la akina Palamagamba halitufai, baraza la watu waoga na comedians
 
Mama kama anataka kweli ajijengee imani kwa Watanzania wengi, alivunje tu hilo Baraza lililojaa wanafiki, wachumia tumbo na waimba mapambio.

Na Majaliwa asiachwe kuendeleza uongo wake! Naye abakie tu na Ubunge wake.
Hapo mama atakuwa amejisafishia njia kuwakwepa wanafiki kumkwamisha
 
Endapo kiti cha Rais kitakuwa wazi kutokana na Rais
kufariki dunia, kujiuzulu, kupoteza sifa za uchaguzi au kutomudu
kazi zake kutokana na maradhi ya mwili au kushindwa
kutekeleza kazi na shughuli za Rais, basi Makamu wa Rais
ataapishwa na atakuwa Rais kwa muda uliobaki katika kipindi
cha miaka mitano na kwa masharti yaliyoelezwa katika ibara ya
40, kisha baada ya kushauriana na chama cha siasa anachotoka
Rais atapendekeza jina la mtu atakae kuwa Makamu wa Rais na
uteuzi huo utathibitishwa na Bunge kwa kura zisizopungua
asilimia hamsini ya Wabunge wote.

Lakini kuhusu awamu au kugombea tena katiba iko wazi kabisa
Endapo makamu wa raisi atakaa madarakani kwa muda wa miaka chini ya mitatu anaruhusiwa kugombea anaruhusiwa kugombea mara mbili lakini endapo atashika kwa zaidi ya miaka zaidi ya mitatu ataruhusiwa kugombea mara moja tu.
 
Nakuhakikishia ana uwezo wa kulivunja na kuunda lingine maana yeye ndiye mkuu wa nchi.

Utake usitake hilo baraza linavunjwa
 
Lakini halikula kiapo chini yake.
 
Akiendeleza upumbavu ulio kuwepo, na yeye atadharauliwa na kuombewa mabaya. Simshauri kuchagua njia hiyo mbaya ya kuwasikiliza zaidi wanafiki na wachumia tumbo.

Samia ni 🔥🔥🔥🔥🔥
Na Samia ni mwanamke📏na jembe kwelikweli
Mungu amtunze tuu maana mwendo ni uleule💣💥
 
Viongozi wote wakuu lazima wale kiapo mbele ya rais.
Hawa waliopo waliapa mbele ya Magu na sio mama Samia. Hivyo lazima baraza lipigwe chini. Hiyo itashuka hivyo hadi kwa ma Rc, IGP, CDF, TISS..... Hivyo....
Katiba ndiyo inasema hivyo? siku zote wakati wa uapisho makamu uwepo kwenye ukumbi au hiyo sio kula kiapo mbele yake?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…