Nini status ya Baraza la Mawaziri la Magufuli sasa na baada ya Samia Suluhu Hassan kuapishwa?

Nini status ya Baraza la Mawaziri la Magufuli sasa na baada ya Samia Suluhu Hassan kuapishwa?

Mama kama anataka kweli ajijengee imani kwa Watanzania wengi, alivunje tu hilo Baraza lililojaa wanafiki, wachumia tumbo na waimba mapambio.

Na Majaliwa asiachwe kuendeleza uongo wake! Naye abakie tu na Ubunge wake.

Mwambieni aanze kwa kuwauliza walio tayari kuendelea na yeye ndio atajua kuwa ngoma iliyo mbele yake sio lelemama.
 
Katiba haijasema chochote kuhusu baraza la mawaziri maana Rais akiunda Baraza huwa anamshirikisha Makamu wa Rais na Waziri mkuu kwa hiyo Baraza la mawaziri balo lipo hai.

Angalizo :Kutokana na tabia ya Bwana Mkubwa ilivyokuwa si bure asilimia 95 ya mawaziri hakumshirikisha mtu yeyote, kwa hiyo uwezekano wa Mama Samia kuanza upya ni mkubwa sana.
Hivi Makamu wa rais anaingia kwenye kikao cha Baraza la Mawaziri?
 
Kama hoja ni kuwa hakuna serikali mpya inayoingia nini logic ya Baraza kuvunjika anapojiuzuru Waziri mkuu au akijiuzuru Waziri mkuu Kuna serikali mpya inaingia?

Waziri Mkuu anashiriki katika kuunda baraza la mawaziri. Akiondoka lazima baraza livunjike. Samia akiamua kubaki na Majaliwa, hakutakuwa na haja ya kulivunja baraza la mawaziri. Reshuffle inaweza kufanyika!
 
Mpira unaendelea kocha tuu kabadilika msaidizi kashika timu so msipanic! Tusubiri tuone formula yake ya ushindi japo binafsi kocha mwanamama sipendi
 
Mama Samia anamalizia ngwe waliyoanza na John Pombe Magufuli

Yeye ataanza ngwe yake kamili kwake 2025-2035

Mungu wa mbunguni amtunze
Hii CCM yenye khofu na kutowaamini ccm wenzao kutoka Zanzibar? 2025 kama namuona ivi anaekwa pembeni
 
Kuhusu tundu kuwa raisi Naomba tusahau [emoji23][emoji23][emoji23]
Aliyekuwa mbabe na mpenda kusifiwa yuko kwenye mafriji sasa hivi. Lissu Yuko hai mbali na kupigwa risasi 16 hadharani na kunyimwa pesa ya matibabu.
 
Mama Samia anamalizia ngwe waliyoanza na John Pombe Magufuli

Yeye ataanza ngwe yake kamili kwake 2025-2035

Mungu wa mbunguni amtunze
Hawezi labda kama akiamua kubadili katiba
 
U
Katiba haijasema chochote kuhusu baraza la mawaziri maana Rais akiunda Baraza huwa anamshirikisha Makamu wa Rais na Waziri mkuu kwa hiyo Baraza la mawaziri balo lipo hai.

Angalizo :Kutokana na tabia ya Bwana Mkubwa ilivyokuwa si bure asilimia 95 ya mawaziri hakumshirikisha mtu yeyote, kwa hiyo uwezekano wa Mama Samia kuanza upya ni mkubwa sana.
Unaweza kushirikishwa lakini usiwe na maamuzi😆😆😆

Kwahiyo, kwasababu Samia Suluhu Hassan hakuwa kwenye capacity ya u-Rais na kufanya maamuzi ni lazima aanze na wa kwake ambapo itabidi amshirikishe Makamu wa Rais atakaependekezwa.

Inaweza isiwe shida kwa PM huyo anaweza akamuacha pamoja na kwamba pia inawezekana Samia hakuhusika kupendekeza jina la Waziri Mkuu.

Angekuwa ni mtu mwingine ambae anataka kuanza fresh angepeleka majina yote mawili bungeni kwa maana ya; Makamu wa Rais na Waziri Mkuu.
 
Mambo mawili yanaweza kufanyika, mosi kuvunja Baraza la Mawaziri na kuliunda upya akishirikiana na Makamu wa Rais mpya na Waziri Mkuu.

Pili, Kulifanyia mabadiliko ya msingi Baraza la Mawaziri lililopo kimuundo na kubadilisha baadhi ya mawaziri kulingana na maono yake ya kiuongozi.

Yote haya yanaweza kufanyika baada ya Rais mpya mama Samia kuapishwa hapo kesho na mazishi ya mtangulizi wake Dr Magufuli kufanyika.

Maendeleo hayana vyama
 
Back
Top Bottom