Nini status ya Baraza la Mawaziri la Magufuli sasa na baada ya Samia Suluhu Hassan kuapishwa?

Nini status ya Baraza la Mawaziri la Magufuli sasa na baada ya Samia Suluhu Hassan kuapishwa?

Samia awe makini tu kwenye ushauri maana kuna ushauri akipokea utampekeka shimoni kama Magufuli. Alipokea ushauri mwingi uliomgombanisha na wananchi
 
Kuna haja ya kumstaafisha mara moja field Martial wa afya ili kuinusuru wizara nyeti ya afya unless otherwise wizara inakoelekea siko kabisa
Huyo waziri wa afya hafai afukuzwe mara moja kashindwa kuhimiza watanzania kuvaa barakoa kunawa mikono kupaka vitakasa mikono kuzuia salam za kushikana mikono
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Kutakuwa na mabadilko makubwa tu Mama akishakabidhiwa ngao na mkuki, mawaziri waliopo watakaopenya ni wachache sana maana wengi walikuwa loyal kwa mwendazake na hivyo hawawezi kumsaidia mpya

Kwa hiyo kujibu mada kwa nionavyo itabidi alivunje ili aanze upya, tutegemee ngwe hii kuwa na viongozi wengi wataotoka jinsi ya HAWA kuanzia kwenye baraza mpk chini.

Lakini pia tutarajie misuguano sana hasa bungeni maana pataibuka kambi za kutosha na kucharuana sana kwa wabunge
 
Samia awe makini tu kwenye ushauri maana kuna ushauri akipokea utampekeka shimoni kama Magufuli. Alipokea ushauri mwingi uliomgombanisha na wananchi
Ushauri wa Hatari ni ushauri wa kuwabambikia kesi watu mbalimbali task force kuwabambikia kodi kubwa wafanyabiashara kuwafungia Account zao biashara zao na uonevu unyanyasaji mwingi
 
Ww huelewi! Magu alifanya uteuzi wakiwa na Samia! Kimsingi, mie namuona Magufuli akifufuka kwa nguvu kupia mama Samia ambaye watu hawataamini ushupavu wake na kimsingi watapata shinikizo la moyo baada ya kukosa matamanio yao ya 'kuiba na business as usual!'

Mama Samia anakwenda kuweka 'bar' ya aina yake isiyokumbatia ufisadi, ubwanyeye, uzembe, ushoga, upanya book wa majaribio, utegemezi nk!

Hivyo basi kaeni mkao wa kunyolewa! Mliozoea kuchezea masharubu ya Magu, nawapa pole, Mama Samia atapita nanyi mkimletea mazoea hayo!

I can see an 'Iron lady' of our time!
Samia ni 🔥🔥 tunasema mwenzako akinyolewa wewe tia maji ila Suluhu yeye ananyoa bila maji💣
Oooh wasiomjua huyu mama tukutani kwenye huu uzi December kama tutajaliwa uzima

Mungu ibariki Tanzania Mungu mbariki mheshimiwa Samia Suluhu Hassan na viongozi wetu wote

Rest well John Pombe Magufuli 🙏
 
Kuirudisha Nchi kwenye umoja itapendeza sana kuwaweka hata Mawaziri watano toka upinzani. Kama Visiwani wameweza kuwa na Mawaziri wa upinzani sioni sababu ya hili kushindikana Bara.
January
Rizwan
Nape..
Hawa wote ndani ya cabinet
 
Haifai kuvunja bali mabadiliko kidogo kidogo ni muhimu hasa zile sekta nyeti inabidi uweke watu watiifu kwako. Mfano waziri wa majeshi,fedha,katibu mkuu,katiba na sheria etc
 
Hivi wale na wale walihamia ccm kutokeza upinzani "kuunga mkono juhudi", itakuwaje
 
Kuirudisha Nchi kwenye umoja itapendeza sana kuwaweka hata Mawaziri watano toka upinzani. Kama Visiwani wameweza kuwa na Mawaziri wa upinzani sioni sababu ya hili kushindikana Bara.
Tutajie hao wabunge wa upinzani bwashee!
 
Asipofanya hivyo basi ajiandae kushindwa mapema kabisa kabla ya wakati wa hukumu (2025) kufika.

Yule mama usimchukulie poa, ni kichwa, na inaonekana yuko karibu na Mungu. Hivyo anajitambua,

Chadema yote + mwenyekiti wenu=Mama samia
 
Back
Top Bottom