Nini story au kisa nyuma ya username yako na avatar yako hapa JF

Nini story au kisa nyuma ya username yako na avatar yako hapa JF

Sante sana ndugu mwaipopo, umenikumbusha nilipokuwa Alevel pale Swilla High School, mbeya. Nilikuwa kwenye darasa ambalo zaidi ya asilimia 90 ya wafunzi wenzetu walikuwa na ubini unaoamziwa na MWA😱😱
twamasiku mwanafafyale wa swilla
 
Am back sizzya007;

Jina la TRANSCEND;

Mimi nilikuwa napenda sana mambo ya IT na Technology Development issues, though nikiwa chuo sikusoma hii fani ila nilikuwa mtundu sana kwenye mambo ya Computers na electronics devices zingine.....

Computer za wenzangu zikiwa na matatizo ndo nilikuwa nawasaidia na vitu vingine kama hivyo, sasa kuna aina ya flash inaitwa TRANSCEND ( najua wengine mnazijua) , ndo aina ya flash nilikuwaga Natumia na ilikuwa na 32Gb ndani ikiwa na setups za software's na mautundu-utundu mengine ya computers.... So watu wakawa wanajua flash yangu na kwa waliokuwa wanataka kununua flash niliwashauri wanunue TRANSCEND kwa kuw niliipenda sana hiyo brand ya flash disk.

Nakumbuka kuna Lecturer mmoja ambaye computer yake iliingiaga shortcut virus , lecturer akawa anahaha...kazi haifunguki ! Then nikamsaidia kwa kumwekea shortcut remover software .....so akija class ananiulizia ""Yule kijana wangu mwenye flash ya TRANSCEND 32Gb yuko wapi?""
From that day nikawa naitwa TRANSCEND


Kuhusu Avatar:

Huyo ni Blair Underwood , American actor... Kuna mdada alinipendaga tukiwa Olevel-seminary flani hivi Arusha....akawa ananiambia umekaa-kaa kama Blair hivi.....so she was calling me Blair ! Blair ! Nadhani alivurugwaga na hair styles yangu.....! Namshimu sana huyo dada....

Am out, hivyo yaani.

Rodger that captain TRANSEND 32GB😎
 
Napenda sana uigizaji wa Robert De Niro...
kuna movie inaitwa...Analyze this ..
aliulizwa na daktari 'what do you do for a living?'
akajibu 'i am the boss' 'i don't do anything'..
sijawahi isahau hiyo scene....
Nimeipenda hii
 
Id chanzo kuna scania 113 tank fupi rangi ya majivu huko tanga kwenye kioo cha mbele imeandikwa NGAMIANI TRUCK ilikuwa nakutana nayo sana barabarani ilikuwa ina turbo basi ikifika sehemu yenye mkusanyiko wa watu dereva anafanya manjonjo basi sisi vijana tulikuwa tunafurahi sana jamaa alikuwa mtundu sana hata akiwa mbali basi huwa tunajua jamaa anakuja kutokana na mlio wa gari na ubadilishaji wake wa gia...avatar huyo ni christopher brown (chris brown) ni rnb singer tangu anaanza kuimba hadi leo nimekuwa fan wake wa kutupwa napenda nyimbo zake, life style yake ingawaje vingne siwez iga kwake like matuminzi ya drugs ni hayo mafupi
 
Back
Top Bottom