Nini tafsiri ya Megawatts 2,115 za umeme wa bwawa la Mwalimu Nyerere (Stiegler's Gorge)?

Juhudi ipi ya kukabili Climate change imeonyesha mafanikio makubwa?? Una mifano??
 
Watu wavivu utawajua tuu, hivi huna habari kwamba watu tayari wana several schemes za irrigation kwa kutumia majenereta? Unadhani vitunguu, nyanya, hoho etc zinalimwaje kama siyo irrigation za kutumia water pumps??

Off-point.
 
[emoji106][emoji106][emoji106][emoji106][emoji106][emoji122][emoji122][emoji122]
 
Kwa mlinganisho na ufahamisho tu hadi mwaka 2018, Kenya walikuwa wanazalisha 2,700 MW za umeme na wana mpango wa kuzalisha 7,200 MW za umeme kufikia mwaka 2030.
 
Hata wewe ni muongo tuu maana haujatoa any proof to backup your argument.
Unajua Megawati moja ni watt ngapi? Kwa taarifa yako Mega watt moja ni Watts 1,000,000 sasa hilo jengo la Mkapa linaweza likatumia Watts Million we unaonekana jinga kabisa.
 
Unajua Megawati moja ni watt ngapi? Kwa taarifa yako Mega watt moja ni Watts 1,000,000 sasa hilo jengo la Mkapa linaweza likatumia Watts Million we unaonekana jinga kabisa.
Umeme unapimwa kwa KWh
1,000,000/1000= 1000KWh
 
Umesahau SGR pekee itakula 700MWh itakapokamilika,
Na kwa sasa Dar - Moro imetengewa 30MWh
 
HAPANA! Nazungumzia vihoja uchwara vilivyokuwa vikitolewa na mabeberu wakati wakipinga ujenzi wa hilo Bwawa; na vihoja hivyo hivyo ndivyo anakuja navyo Lissu na wewe leo! Ndiyo maana nasema nilishawahi kusikia vihoja kama hivi hapo zamani na majibu yake yalishatoka ikiwa na hiyo ya kusema kuwa sehemu ya huo mradi wa hilo Bwawa ni less than 2% ya eneo linalopigiwa kelele la hiyo mbuga ya Selous. Hiyo ni moja ya majibu ya vihoja hivyo dhidi ya hilo Bwawa and that is what I am trying to say hapo juu ndugu siyo matusi!
 
Umesahau SGR pekee itakula 700MWh itakapokamilika,
Na kwa sasa Dar - Moro imetengewa 30MWh
Muongo leta ushahidi, train zinatumia Motor mzee na hakuna motor duniani inayotumia umeme mkubwa kiasi hicho.
 
Na gesi ya kupikia (LNG) ambayo tuliambiwa mtungi wa elfu 50 tutanunua kwa elfu 10 imekuwaje???
Kama nilivyosema, kwa gas inachomwa kwenye majenereta, hivyo ikishachomwa ndo imeisha. Kupata gas kwa ajili ya LNG plant inatakiwa uwe na gas nyingine ujenge plant... Hiyo ya kujenga plant ndo haijafanyika hadi leo
 
Hayo nayajuwa... nilitaka kuelezea kwamba huwezi ipata tena gas kama gas...
 
Muongo leta ushahidi, train zinatumia Motor mzee na hakuna motor duniani inayotumia umeme mkubwa kiasi hicho.
Ukiwa na motor nyingi unaweza fikisha power hiyo... Ingawa kwa treni hatutegemei hilo
 
Ngoja nikuulize!

Assume kiasi ambacho mtu anatakiwa kula ni 1kg ya mchele na 1 kg ya nyama, ambazo total ni TSh 10K! Lakini kwa kuwa hana uwezo wa Sh.10K, anaamua kula 1/2 kg ya mchele na 1/kg ya nyama ambayo total ni TShs. 5K

Je, unaweza kusema mahitaji ya huyo mtu ni TSh. 5K?!
Hapa napo unatakiwa kujiuliza suali la hapo juu!!!!

Anyway, wacha nikujuze!!!

Mahitaji ya Lindi na Mtwara sio hizo 22MW to 30MW ulizotaja bali umaskini ndio unakufanya udhani mahitaji yao ni 22-30MW!!

Bei kubwa ya umeme inawafanya watu wasiwe wanatumia vifaa vya umeme vinavyotumia umeme mwingi kama vile majiko na pasi!

Umaskini unawafanya watu wa Lindi na Tanzania kwa ujumla wasiwe na uwezo wa kununua vifaa vya nyumbani vinavyotumia umeme kama vile majiko, majokofu, mashine za kufulia nguo, redio n.k!!!

Kwahiyo hicho unachoona kama matumizi yetu Tanzania ni 1550 MW inatokana na watu ku-opt kula mchele 1/2 kilo na nyama 1/2 kilo wakati mahitaji yao ni 1kg ya nyama na 1kg ya mchele kwa sababu hawana uwezo wa kununua 1kg ya nyama na mchele!!!

Leo hii ikitokea situation kwamba 50% TU ya watu wanaoishi Dar es salaam peke yake wawe na uwezo wa kununua na kutumia majiko ya umeme, pasi, majokofu, mashine za kufulia nguo; hata bila ya kungalia mikoa mingine, hapo hapo utagundua hizo 2114MW si lolote si chochote!!

And remember, hivyo vifaa nilivyotaja hapo juu ni basic home appliances!!

That's one but two, umeonesha mapungufu makubwa ya kiuchambuzi pale unapodai:-
Hapo umedanganya, ama kwa makusudi au kwa kutojua!!!

Kiwango chake cha mwisho kinachoweza kuzalishwa pale Kinyerezi kitategemeana na kiwango cha gesi kitakacholetwa pale relative to capacity ya bomba linalosafirisha gas husika!

Hapo kabla iliwahi kutangazwa kwamba Bomba la Gesi linaloenda Kinyerezi linasafirisha ONLY 6% ya uwezo wake!! Kwa sasa labda itakuwa imefikia 15-20%, au kama imezidi sana labda 25%!!!

Hii maana yake ni kwamba si kweli eti uwezo wake wa kuzalisha pale Kinyerezi ni Megawatts 1560 tu bali hizo Megawatts 1560 zinatokana na gas ambayo inaenda pale!!! Kwa maana nyingine, hata bila ya kujenga bomba lingine, pale Kinyerezi tunaweza kuzalisha zaidi 6000MW za umeme!!

Na hata bomba likielemewa, bado unaweza kujenga bomba lingine na terminal kuwa at the same Kinyerezi Power Plant or elsewhere provided gas bado ipo!!

Lakini kwa upande mwingine, labda kwa sababu umeamua kuleta ushabiki wa kisiasa au kwa kutojua, umeshindwa kuelezea multiplier effect inayoweza kupatikana kwenye uwekezaji kupitia gas as compared na umeme wa maji!

Wakati kinachoweza kupatikana kwenye uwekezaji wa Bwawa la Nyerere ni umeme pekee (na faida zake), uwekezaji kwenye gas ungeleta huo umeme ambao utapatikana kupitia Bwawa la Nyerere, na pia ingepatikana nishati mbadala ambayo ni gas yenyewe!!

On top of that, unapofanya gas processing kunakuwa na byproducts zinazoweza kuchochea uanzishwaji wa viwanda vya mbolea na plastic, na ndio maana Dangote alitaka kuanzisha kiwanda kikubwa sana cha mbolea kule Mtwara!!!

Kwa kujiongeza zaidi, pitia hapa chini:
Multiplier effect (economic multiplier effect) nyingine ambayo ni kubwa sana ni ile ya kwenye ajira zinazokuwa generated kutoka kwenye gas extraction, gas processing, gas distribution and transportation, and many more!!

Yote hayo hayawezi kupatikana kwenye mradi wenu mnaotuaminisha kwamba ndo mwisho wa matatizo!!!
 
Ahsante sana for ceteris paribus manake hata hizo 2115MW anazodai ni nyingi kweli kweli, zitaendelea kuwa nyingi endapo tu kiwango cha uchumi wa Tanzania kitabaki kama kilivyo, lakini leo hii ikitokea 5% ya Watanzania wakanunua majiko ya umeme na kuyatumia, in no time atajua 2115MW ni umeme kidogo sana!!!
 
Kinyerezi I inatoa MW185 na Kinyerezi II inatoa MW 240 umeme mwingine unatoka katika vyanzo vingine mzee usidanganye na kujitia unajua sana angalia document hiyo
 

Attachments

Kwa nini 2,115? Kwani ukitoa 3,000 shida iko wapi? Yaani ikifika 2,200 au 2,120 kuna shida gani? Si maji yapo?
 
Niambie kwa sasa nchi nzima Tanzania tunatumia MW ngapi kwa matumizi ya ndani,.. na MW ngapi kwa matumizi ya viwandani.

I rest my case here.

Kabla hauja restisha your case, hivi umemwelewa vizuru huyu mkuu renamaizo?
Ni mbaya sana kuelezea jambo gumu ambalo huna taaluma nalo!
 
Kinyerezi I inatoa MW185 na Kinyerezi II inatoa MW 240 umeme mwingine unatoka katika vyanzo vingine mzee usidanganye na kujitia unajua sana angalia document hiyo
We Juha kweli!!

Mimi na wewe nani anayejifanya kujua au anayedanganya watu?!

Wapi nimesema Kinyerezi inazalisha kiwango fulani cha umeme zaidi ya maelezo yangu kuegemea na kile kilichoandikwa na mleta mada kwamba:-
Nyie Misukule ya Lumumba kichwani bure kabisa ndo maana mmebaki kushangilia mambo ya kijinga!
 
Mwenye ufahamu kuhusu uzalishaji wa umeme kupitia gas yetu na malengo yake ya baadae atusaidie pls
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…