Nini tafsiri ya Megawatts 2,115 za umeme wa bwawa la Mwalimu Nyerere (Stiegler's Gorge)?

Nini tafsiri ya Megawatts 2,115 za umeme wa bwawa la Mwalimu Nyerere (Stiegler's Gorge)?

Mkuuu hapo kwa Kinyerezi kuzalisha 1556MW ni typing error au na wewe haujui.?
Kinyerezi pale kuna plant mbili.
Kinyerezi 1 Gas power plant maarufu kama k1 na Kinyerezi 2 Thermal power plant/Combined Cycle power plant.
Hii K1 inazalisha 150MW .
Na k2 inazalisha 240MW.
Ambapo jumla yake inakuwa 390MW.
Sasa hyo 1556 umeitoa wapi.?
 
Kwanza kuingia kwa Serikali ya awamu ya 5 kulifungua ukurasa mpya wa utekelezaji wa maono ya Baba wa Taifa ya toka mwaka 1975 ya kutaka kuzalisha umeme kwenye bonde la Mto Rufiji kupitia mradi huo mkubwa kabisa namba 4 wa uzalishaji wa umeme barani Afrika unaoenda kuzalisha Megawatts 2115 kwa gharama ya Trillion 6.5 tena kwa fedha zetu za ndani.

Una hoja nzuri lakini hujui kabisa kuelezea!!
 
Mwegeso..umeongea vyema kabisa. Lakini reserve ya maji itategemea na uwepo wa feed up channels..labda kuwepo na chemichemi ya kudumu ambazo pia msimu wa kiangazi hupungua uwezo wake wa kutoa maji. Unakumbuka kukauka kwa mabwawa miaka ya 2007-2008 ikaletelezea Richmond saga? Waswasi wangu uko hapo Mwegeso. HEP easy and cheap but very unreliable kutokana na kutegemea single sources of water resources hasa kwa sisi Tanzania. Mabadiliko ya tabia nchi na yenyewe hayatabiriki sana kutokana na population. Tuombe kama unasema kusitokee majanga ya mazingira. Lets hope all factors are constant then bwawa la Stigler gorge litadumu milele.
Nakubaliana nawe kuhusu athari za mabadiliko ya tabia nchi kwenye uzalishaji umeme kwa njia ya maji (hydropower). Ripoti ya uchambuzi yakinifu kuhusu huo mradi umetoa mapendekezo ya kupunguza, kama siyo kudhibiti kabisa, athari za kimazingira kwa jamii, viumbe hai na ufuaji umeme (naambatanisha ripoti hiyo). Lakini mapendekezo hayo hayawezi kufanikiwa iwapo wahusika ambao ni mimi, wewe na kila mwananchi hatotimiza wajibu wetu.View attachment TECHNICAL REPORT FOR STIGLER'S HYDROPOWER.pdf
 
ALL in ALL... alternator au kinu kinachofua umeme kinahitaji mzunguko ili kizalishe umeme (Rotation). Mzunguko huo unaweza ukaupata kwenye upepo (windmill), mechanical engine (petrol ro diesel engine) maporomoko ya maji (water turbine - hapa akina Kidatu wanahusika), steam engine, GAS TURBINE ETC

Majenereta yaliyopo Mtwara mjini yote yanachoma gas kama inavyochomwa petroli au diesel ili kupata MZUNGUKO utakaozalisha umeme. Gas hiyo ikishachomwa, ndo mwisho wake, kama ambavyo diesel ikishachomwa ndo basi tena huwezi kuwa na diesel hiyo..

Kwenye turbines, ntaanza na water turbine... maji yanayoporomoka sehemu, kwa sababu ya HEAD (umbali toka mporomoko yanapoanza hadi maji yanapokwenda kutua) maji hupata na energy... sasa maji hayo yanayoporomoka, yakipelekwa kwenye gurudumu (turbine) yatalizungusha, and hence alternator iliyounganishwa na turbine hiyo itazalisha umeme. Kwa maji, yakishazungusha turbine, yanaweza yakatumika tena kwenye maisha ya kila siku ya binadamu mfano uvuvi, kilimo etc

Sasa kwa gas, gas yenyewe huwa inatoka huko ardhini ikiwa na high pressure. Pressure hiyo inaweza ikasukuma gurudumu linalohimili gas (gas turbine) na rotation ikapatikana na mwisho umeme kuzalishwa. Kama ilivyo kwenye maji, gas iliyokwisha tumika kuzalisha umeme, inaweza ikatumika tena kwenye shughuri za kibinadamu mfano viwandani (kama ilivyo kwa TBL, wazo cement etc), ingeweza kusambazwa majumbani kwa kupikia etc.

Sasa kwa hali ilivyo sasa, tunachoma gas na hivyo ukitaka ya matumizi mengine lazima uichimbe upya...

ALL IN ALL, SHIDA KUBWA NI SIASA
Bwana mkubwa naona umejitahidi kuzunguka mbaaali lakini maswali yangu naona hujayapata vyema, hiyo gas turbine yako ambayo blade zake zinasukumwa na gas moja kwa moja zinaitwaje? kwa kukusaidia nenda,ubungo 2,kinyerezi 1 na kinyerezi 2 ukaone gas turbine inavyofanya kazi ili uondokane na dhana uliyonayo hiyo ambayo duniani hatuna katika upande wa gas. majenereta yalioko mtwara,ubungo 1 na tegeta zile ni reciprocating engine lakini mechanism za kupata expansion kubwa kwaajili ya kupata nguvu ni kuchoma gas. nakushauri rudi kwenye makaratasi yako ulikojifunzia hii kitu kuhusu gas na kayachane kabisa,halafu anza shule upya ya thermodynamics ili uelewe halafu ukishindwa kuelewa nitafute nikufundishe vyema ili uwe binadamu kwenye ulimwengu wa Energy
 
Jidanganye
Kwa nyongeza zaidi kitakwimu, kwa wale maTomaso, wanaobeza kuwa huo mradi ni maendeleo ya vitu, mimi natumia wastani wa unit 420 kwa mwezi wa gharama ~ 150,000/-.

Umeme wa Bwawa la Nyerere ukikamilika nitakuwa nalipa chini ya 20000/- kwa mwezi. Hii ina maana nitakuwa na salio la 130,000/- ambayo nitaitumia kwa maendeleo yangu (mtu).

Hiki ni kiasi cha 1,560,000/- kwa mwaka ambacho si haba maana kinatosheleza kwa elimu ya watoto/wajukuu wangu (maendeleo ya watu) au kulipia bima ya afya (maendeleo ya mtu), na kadhalika
 
Nikuongezee kanyama kengine,gas ikishachomwa sio kwamba matumizi yake yameisha, gas iliyochomwa hua inatumika tena kuzalisha umeme au kuchemsha maji kwa matumizi mengine itategemea na uhitaji wake, nenda tena pale kinyerezi 2 wanatumia gas turbine kufua umeme na hapo hapo gas iliyoungua inazalisha umeme wa mvuke (Stem turbine) tunaita combined cycle. Kijana punguza munkali wa siasa unapokuja kwenye utaalam na kama hujui jitahidi uchimbe kwanza na kuomba msaada kwa wajuvi wa haya mambo.
 
NINI TAFSIRI YA MEGAWATTS 2,115 ZA UMEME WA BWAWA LA MWALIMU NYERERE (Stiglers Gorge)?

Wengi tunaona na kusikia kuhusu habari ya utekelezaji wa mradi mkubwa wa uzalishaji umeme wa maji wa Megawatts 2115 kutoka kwenye Mto Rufiji, mradi uliobuniwa na Mwalimu Nyerere toka mwaka 1975 na sasa unatekelezwa na Rais wa awamu ya 5 Dkt John Pombe Magufuli.

Tumesikia habari ya ukubwa wake huo mradi, gharama ya utekelezaji wa mradi wenyewe, umeme unaoenda kuzalishwa na mambo mengine mengi sana kuuhusu mradi huo wa Stieglers Gorge (Bwawa la Mwalimu Nyerere). Sasa leo ngoja tuumulike kidogo mradi huu wa umeme, tujue idadi ya namba zilizoko za gharama na Megawatts zinazoenda kuzalishwa hapo na tafsili yake kwa Watanzania na uchumi wetu.

Kwanza kuingia kwa Serikali ya awamu ya 5 kulifungua ukurasa mpya wa utekelezaji wa maono ya Baba wa Taifa ya toka mwaka 1975 ya kutaka kuzalisha umeme kwenye bonde la Mto Rufiji kupitia mradi huo mkubwa kabisa namba 4 wa uzalishaji wa umeme barani Afrika unaoenda kuzalisha Megawatts 2115 kwa gharama ya Trillion 6.5 tena kwa fedha zetu za ndani.

Adhima ya utekelezaji wa mradi huo inakuja wakati nchi ikiwa kwenye ujenzi wa uchumi wa viwanda ambao kwa kiwango kikubwa unategemea sana nishati umeme ya kuwezesha viwanda kupata nishati ya kutosha ili iweze kuzalisha vya kutosha na muhimu kwa gharama nafuu. Viwanda ni umeme na umeme ni viwanda.

Lakini licha ya yote ni wangapi tunaelewa tafsiri halisi ya Megawatts 2,115 za umeme zinazoenda kuzalishwa pale Mto Rufiji? kwa sisi watu wa kawaida ambao si wataalamu wala wahandisi tunaelewa nini kuhusu Megawatts 2115? twende sawa hapo chini.

Kuzielewa Megawatts 2115 na ukubwa wake ni rahisi ukipitia na kujua matumizi ya umeme na mahitaji ya umeme kwa taifa letu. Mfano mwepesi tu ni kwamba mahitaji halisi ya umeme kwa mikoa kama ya Mtwara na Lindi ili umeme usikatike hata sekunde ni Megawatts 22 hadi 30 tu, ina maana katika zile Megawatts 2,115 tunakuwa na chenji kama ya Megawatts 2,085.

Tanzania ina Mikoa 31, hivyo ukifanya kila mkoa upate Megawatts 50 tu kama makadirio ya juu kabisa hata kwa mikoa isiyozidi matumizi hayo maana yake ni sawa na kupeleka bahari ya umeme kila mkoa na bado matumizi tutaishia Megawatts 1,550 na bado zitabaki Megawatts 565 kama akiba ya umeme tuliyoiweka kibindoni. Bado hiyo Megawatts 50 kiwastani hata ukijumlisha mikoa yenye viwanda vingi na vikubwa kama Pwani, Dar es Salaam, Arusha, Tanga na Mwanza bado ni kubwa sana. Nimeweka kwa kiwango cha Juu saana usisahau matumizi ya Mtwara na Lindi ni Megawatts 22- 30 tu.

Ina maana hapo tunaenda kuua kabisa stori za mgao wa umeme na mambo ya umeme kukatikakatika. Hapo wenye viwanda vikubwa, vya kati na vidogo kabisa watazalisha bidhaa zao bila tatizo na zaidi kwa gharama nafuu kutegemea na urahisi wa gharama kwa umeme wa maji.

Umeme wa Kinyerezi ambao ndiyo tunaojivunia kwa sasa kuwa ni mradi mkubwa wa umeme kiwango chake cha mwisho cha kuzalisha umeme ni Megawatts 1,560 tu ina maana Bwawa la Mwalimu Nyerere pekee yake linaenda kutupa umeme wa uhakika tena wa maji ambao ni rahisi zaidi kuliko aina yoyote ile ya umeme duniani ukiachana na wa jua, upepo, nyuklia, makaa ya mawe, mafuta na gesi.

Tukumbuke umeme unaozalishwa na maji ndio umeme wa gharama nafuu na rahisi zaidi kuliko umeme wowote ule duniani. Kumbuka uniti 1 inayozalishwa na maji ni shilingi 36 tu wakati umeme wa nyuklia ni shilingi 65 kwa uniti, umeme wa jua shilingi 103.05, upepo 103.05, makaa ya mawe 118, gesi asilia 147 na mafuta ni 426. Hivyo tunaenda kushusha maradufu bei ya umeme kwa watumiaji hivyo kuhimili mfumuko wa bei wa bidhaa za viwandani.

Hii tafsili yake kukamilika tu kwa Bwawa la uzalishaji wa umeme la Mwalimu Nyerere kutashusha kwa kiwango kikubwa sana gharama ya umeme mpaka shilingi 36 tu kwa uniti hivyo kutoa nafasi kwa bidhaa zetu za viwanda nazo kushuka sana. Hapo mpaka kwenye matumizi ya kawaida nyumbani yatashuka na hata kwa watanzania watakaofungua viwanda vidogo kwa vikubwa watanufaika sana na gharama ndogo ya uzalishaji wa bidhaa itakayoleta neema na nafuu mpaka kwa sisi watu wa hali ya chini kabisa, machinga, mama nitilie, wajasiriamali na makundi mengine.

Unapokuwa na umeme wa uhakika, lakini sio wa uhakika tu tena na wa gharama nafuu ya bei tayali unavutia wawekezaji wengi zaidi kuja kujenga viwanda hapahapa. Suala la uhakika wa umeme na nafuu yake ni mambo ya msingi sana kwa mwekezaji anayefikiri kwenda kuwekeza sehemu yoyote ile kwasababu kiwanda ni nishati.

Vipi umefikilia hizo Megawatts zingine zaidi ya 565 ambazo tunakuwa tumezitia kibindoni baada kujihakikishia uhakika wa umeme nchi nzima? hapo tunaweza kuamua kuuza kwa majirani zetu hapo Kenya, Malawi, Uganda au Msumbiji ambako tunajua bado hawana uhakika wa umeme. Hapo unazungumza kuhusu umeme wa Rufiji tu, hujaenda Kinyerezi, Kidatu, Mtera, Nyumba ya Mungu na kwingine ambako umeme unaendelea kuzalishwa.

Rais Magufuli na Serikali yake baada ya kugundua hatuna umeme wa kutosha na wenye bei nafuu kwa wananchi wake ndiyo ikaja na suluhisho hilo la Bwawa la Mwalimu Nyerere. Nini tena sasa? Tusiposema sisi kwa haya yanayofanyika basi hata mawe yatapiga kelele siku moja.View attachment 1597580

Kabla hamjarukia kuwahadaa Watanzania mtuambie ufanisi wa hiyo miradi kabambe mlokwishaifanya. Tuanze na BOMBADIA.
 
Anza hata leo gesi asilia kwenye gari lako
Mkuu, asante sana kwa udadavuzi wa hiyo mada.

1. Kama sijakosea, hiyo 2115 MW ni installed capacity, je umeisha fanya hesabu kujua Capacity factor tarajiwa ya hiyo Hydropower Plant itakuwa kiasi gani?

2. Na mmejipangaje kukabiliana na "generation na load balancing" wakati wa peak load au matumizi ya umeme ya kipungua kwa masaa kadhaa kwa siku.?

3.Mkuu, gharama ulizotoa za ununuaji wa unit ya umeme ni Levellized Cost of Energy ama ni tariffs za umeme kutokana mamlaka husika? Naomba chanzo cha Takwimu zako hizi.

Natanguliza Shukrani kwa majibu ya maswali na ombi la chanzo cha Takwimu.
 
Shida ya kwenye gas, ni kwamba badala ya kuweka gas turbines sehemu zote zenye majenereta, wao wameweka mashine zinazochoma gas kama unavyochoma petroli. Gharama ingekuwa rahisi kidogo kwa turbines kuliko ilivyo sasa. Kama kwenye maji, baada ya turnine, tungekuwa bado tuna gas kwa matumizi mengine
Na gesi ya kupikia (LNG) ambayo tuliambiwa mtungi wa elfu 50 tutanunua kwa elfu 10 imekuwaje???
 
Kwa nyongeza zaidi kitakwimu, kwa wale maTomaso, wanaobeza kuwa huo mradi ni maendeleo ya vitu, mimi natumia wastani wa unit 420 kwa mwezi wa gharama ~ 150,000/-.

Umeme wa Bwawa la Nyerere ukikamilika nitakuwa nalipa chini ya 20000/- kwa mwezi. Hii ina maana nitakuwa na salio la 130,000/- ambayo nitaitumia kwa maendeleo yangu (mtu).

Hiki ni kiasi cha 1,560,000/- kwa mwaka ambacho si haba maana kinatosheleza kwa elimu ya watoto/wajukuu wangu (maendeleo ya watu) au kulipia bima ya afya (maendeleo ya mtu), na kadhalika
Nitajie kitu ambacho kimeshuka bei angalau kwa 30 - 40 % since 2015? Mbwembwe za gesi ziliishia wapi? Hatusikii tena habari za uchumi wa gesi mbona?
 
Bwana mkubwa naona umejitahidi kuzunguka mbaaali lakini maswali yangu naona hujayapata vyema, hiyo gas turbine yako ambayo blade zake zinasukumwa na gas moja kwa moja zinaitwaje? kwa kukusaidia nenda,ubungo 2,kinyerezi 1 na kinyerezi 2 ukaone gas turbine inavyofanya kazi ili uondokane na dhana uliyonayo hiyo ambayo duniani hatuna katika upande wa gas. majenereta yalioko mtwara,ubungo 1 na tegeta zile ni reciprocating engine lakini mechanism za kupata expansion kubwa kwaajili ya kupata nguvu ni kuchoma gas. nakushauri rudi kwenye makaratasi yako ulikojifunzia hii kitu kuhusu gas na kayachane kabisa,halafu anza shule upya ya thermodynamics ili uelewe halafu ukishindwa kuelewa nitafute nikufundishe vyema ili uwe binadamu kwenye ulimwengu wa Energy
Nilistuka aliposema gesi inatoka moja kwa moja "ardhini" na kuzungusha Turbine!! Ila nadhani atakuwa amechanganya "materials" ya geothermal hasa aina ile ya Dry steam geothermal power plant!!!
 
Mh Rais Dr. John Pombe Magufuli leo akiwa Kinyerezi, Dar es salaam amesemasualala ajira kwa vijana awamu ijayo litatatuliwa tu. Lakini pia hii miradi itaajiri sana ndiyo maana kwa sasa serikali inapambana kutengeneza miradi mikubwa ya kudumu yenye kutoa ajira za kudumu
Namkumbuka yule dogo aliimba songi moja hivi 'Bongo bahati mbaya [emoji445] [emoji445] [emoji445]' ngoja tusubiri ajira kwa madogo itatuliwe [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Hakuna Jengo lolote ambalo linaweza likatumia hata Megawatt moja duniani usitufanye sie wajinga . Kwenye jengo hilo na Mkapa kuna furnace za kuyeyushia dhahabu au chuma punguzeni uongo wewe unaonekana umesomea siasa tu na kukaa kwenye keyboard kuleta uongo huku ukibadili ID zako.
Hata wewe ni muongo tuu maana haujatoa any proof to backup your argument.
 
Halafu huu wa kinyerezi na vyanzo vingine vya maji tunaupeleka wapi?kama tunauza uhakika wa soko upo? Je wataumaliza wote au?...vyanzo vingine kama mtera,nyumba ya mungu nk vingeboreshwa je tusingeweza fikia megawatt hizo za stigler?..kama zingefikiwa hudhani kwamba ingekua busara kiuchumi hii hela ya stigler zingejengwa skimu za umwagiliaji vijana wangepata ajira huko?..ukiweka na viwanda vyepesi vya kuchakata hayo mazao yatokanayo na skimu huoni tungekua tumeyagusa maisha ya raia moja kwa moja na serikali ingepata kodi chapu?
Real great thinker [emoji106][emoji106][emoji120][emoji120]
 
Labda hukunisoma vizuri. Kushuka kwa bei ya umeme inaweza kuwa motisha kwa wanaotaka kuanzisha hizo scheme. Mimi ninayo micro scheme, gharama za umeme kuvuta maji toka kisima kirefu zinafanya mapato ya mradi kuwa kidogo sana hasa mikoa ya kanda ya kati yenye ukame mkubwa.

Umeme ukipunguzwa bei tukalipa kwa mfano sh 100/unit, itawavutia wengi ku-invest kwenye schemes ndogondogo za umwagiliaji kwakuwa zitalipa.
Watu wavivu utawajua tuu, hivi huna habari kwamba watu tayari wana several schemes za irrigation kwa kutumia majenereta? Unadhani vitunguu, nyanya, hoho etc zinalimwaje kama siyo irrigation za kutumia water pumps??
 
Ita supply continuously kwa sababu hakuna limit ya water flow and it will depend na ENVIRONMENTAL CONSERVATION itakavyokuwa.
Are aware of ongoing climate change crisis? Kama kidatu ilikauka hali ikawa Mbaya nini kutasababisha hili lisikauke wakati tatizo la climate change ndiyo linazidi? Angalia mlima Kilimanjaro unavyoteketea kwa moto [emoji91] [emoji91] jambo ambalo si la kawaida.
 
I remember to have read similar arguments kama hii, ambayo pia Lissu na mabeberu wengi wamekuwa wakizitumia kupinga mradi huo wa Rufiji ikiwa ni pamoja na uharibifu wa mazingira na kutumia vibaya Mbuga ya Selous! What a joke!
Mkishindwa kupangua hoja za Watanzania wenzenu kwa hoja mnakimbilia kuwaita mabeberu, ni ujuha tuu huo, pangua hoja kwa hoja siyo kurusha rungu, hoja haifi kwa kupigwa rungu (alisema JK).Mtu na akili zako unashindwa kuzima hoja kwa kujenga hoja nzito badala yake unakimbilia kumuita mara beberu, ooh siyo mzalendo, mara ooh shoga... Halafu unataka sisi wengine eti kutumaini na kukuona umeongea la maana kumbe pumba tupu.
 
Back
Top Bottom