Highlander
JF-Expert Member
- Feb 12, 2012
- 3,093
- 1,075
Nimeota mimi mwenyewe na niliwahi kuiota pia, hii ni kama mara ya 2 au 3,iko hivi;
inatokea magari wawili ya kubebea pesa yanapinduka(ni katika mji ambao sijawa kuuona ila mazingira na matukio kati ya ndoto hii na zilizopita yanafanana), watu wengi wanaenda kuokota pesa ambazo ni dollar lakini mimi siendi naendaelea kutembea, baadae wenzangu wawili niliokuwa nao lakini walienda kuokota dollar wanarudi nazo na wananipa nyingine niwashikie wao wananipa dollar 250 zote walizokuwa nazo na wanabaki na dollar ambazo ni dollar 20, 10 na nyingine lakini hakuna kubwa kufikia note za dollar 250 aliyenipa hela nishike ni mtu niliyesoma nae chuo kikuuna huyu mwingine ni ndugu yangu na inaoneka walikubaliana wagawane baadae, mtende inaonekana anataka kama baadadhi ya note za dollar 250 anataka kumdhulumu ndugu yangu,natambua hilo kwa kumwangalia machoni na mm nakuwa kama nimekubaliana nae.
Mimi naelekea mahali pengine na wao pengine kwa miadi ya kukutana baadae, mimi naangaika na kutafuta bar hili nile ghafla rafiki yangu ananipigia simu kuwa niende kuongea na simu kwenye jengo alimokuwa ambalo ni kama benki kuu hivi ananitajia jina la mtu anayetaka kuongea na mimi, ni mtu ambaye nimemfaham kupitia ndoto niliyoota before ndoto hii kwa maana ndoto zilipandana na siikumbuki hiyo ndoto ila nakumbuka kuwa namfahamu huyo jamaa, namwambia rafiki yangu a-transfer call kwenye simu yangu ya kiganjani lakini anakataa na mimi namuona kwa kuwa jengo lilikuwa mbele yangu, wakati naenda kuwaona nilitereza nikaingia kwenye dimbwi dogo la matope machafu sana na kunauwezekano tope likawa limechanyika na mavi. Sandles zangu zinapotelea humo, natoka humo nafika ili kuongea na simu kumbe ni mtego wale wenzangu walikuwa wameshikwa na walitumika ili na mimi nishikwe,wakati nashuka na watu wa benki kwenda ukaguzi na dollar ninazo mfuko nafkria nifanye nn mara ndugu yangu ananipa 12,000 ni niwape wakaguzi wasinifunge, wakati nafikiria udogo wa 12,000 huku nazipokea nikawa najaribu kutoa hizo dollar nimpe ndugu yangu ili nisikutwe nazo ikawa inaniwia viggumu na ndoto ikaisha.
Naombeni tafsiri wana jamvi,si mara ya kwanza kuiota, si kila mtu ana kipawa cha kutafsiri ndoto na ipo mpaka kwenye vitabu vitakatifu, mimi nimeshindwa kuielewa naomba mwenye kuielewa anisaidie
ndoto zote ni mwili unajiongelesha. mwili huwa unajiongelesha kuhusu mafikirio yake katika ngazi ya roho, katika ngazi ya akili, na katika ngazi ya hali halisi. Haya mambo yanapoanza kutafakariwa kwenye sub-consious ndo unaona ndoto. Kwenye sub-consious ni eneo la mawazo ambalo halina utashi kama uliopo katika mafikirio ya hali halisi. Ni mafikirio katika hurka ya mwanadamu iliyojificha. Ukitaka kujua hilo lalia mkono wako uwe unaumia katika uzingizi. Hapa mwili utaanza kujiongelesha kuhusu tatizo hilo na utapata ndoto ya jinamizi.
Wewe una tamaa ya utajiri kupindukia lakini hujatangaza tamaa hiyo kwa uwazi kama vile wanvyofanya wabunge kule Dodoma. Tamaa yako imejificha inazungumzwa tu kwenye sub-consious. Nakushauri tafufa kazi ya kufanya inayokupa kipato fulani na ridhika na unachokipata. Bila hivyo kuna siku utafanya ujambazi au wizi wa aina nyingine. Mwili wako unajiongelesha kitu ambacho kama kisipopatikana unaweza ufanye lolote kukipata.