Mokaze
JF-Expert Member
- Aug 3, 2018
- 14,370
- 14,929
Kichwa kinajieleza. Mwenye ulewa afafanue. Utasikia mtu ana maruhani au ana mapepo au ana mashetani au ana majini. Tofauti yake ni nini?
Maruhani ndiyo mapepo ndiyo yale yanayowashika sana akina mama, utasikia watu wakisema; mama fulani kapandisha maruhani wake na kwakuwa ni athari zinazowashika watu hasa kina mama na huwashika kichwani bila watu wa nje kuziona hizo athari na hata muathirika naye hufanya matendo fulani bila kujitambua basi watu wakayaita kwa jina la "majini" --- jini ni umoja wa neno majini, maana yake ya moja kwa moja ni kitu chochote kisichoonekana kwa macho ya kawaida (naked eyes), jini au jinn ni neno la kiarabu lenye maana hiyo ya asili.--- shetani ni kitu chochote kiovu chenye uhai, awe mtu, mnyama, nyoka nk, anapokuwavni muovu au mtenda uhalifu huyo anabeba jina la shetani.