Nini tofauti kati ya Maruhani, Mapepo, Mashetani na Majini?

ruhani ni kama vile mshana jr,jini ni kama vile bashite na shetani ambaye ni mkuu wao ni kama jiwe
 
Inakuaje akiombewa ana pona
Na hapo imekaaje??
Kimsingi, majina yote kasoro moja yametokana na maneno ya kiarabu, maruhani (ruhani) kwa kiarabu ni روح حن yaani roho yenye tamaa kubwa ya kitu fulani ambayo ndiyo mapepo yanayowashika kina mama zaidi wengine huyaita kwa jina la majini (jinn) kwa kiarabu الجن ambalo ni neno lilitokana na kitenzi جن yaani kuficha/ kutoonekana kwa macho ya kawaida, kwakuwa akina mama wanaopatwa na hayo mapepo yasiyoonekana kwa macho ndipo waarabu wakayaita kwa jina "majini"-- lakini huo ni ugonjwa miongoni mwa magonjwa ya akili na kitaalamu ugonjwa huo unaitwa "Hysteria", wala hakuna kiumbe au viumbe vinavyotoka nje na vikamwingia mtu kichwani kama jinsi watu wengi wanavyoamini na kuaminishwa. Naam, katika lugha ya kiarabu inaruhusiwa bakteria wote (microscopic organism) kuitwa kwa kutumia jina "majini" kwa sababu tu ya sifa yao ya kutoonekana kirahisi, na baadhi ya maandiko ya kiarabu fasaha cha kale (clasic arabic) neno hilo limetumika kwa mnasaba huo.

Neno shetani kwa kiarabu ni شيطان (shaitwaan), ni kiumbe chochote kiovu chenye uhai.
 
Ruhani = spirits (roho) ambazo hazipo kwenye mwili, mwili umekufa na roho haijaingia kwenye umauti. Roho zinazotokana na binaadam na majinni.
Jinni = viumbe tusiowaona na wao wana "axis" yao na binaadam tuna "axis" yetu.

Axis = mhimili au "mihwar" Kiarabu.

Mapepo = ni mchanganyiko wa yote hayo juu.

Shetani = Ni sifa (mbaya) ya kiumbe chochote kile iwe binaadam, jinni au mnyama.
 
Na malaika mbona haelezwi humu naye yukoje maana anatajwa humu ama kuhusishwa na majini.
 
Kimsingi, majina yote kasoro moja yametokana na maneno ya kiarabu, maruhani (ruhani) kwa kiarabu ni روح حن yaani roho yenye tamaa kubwa ya kitu fulani ambayo ndiyo mapepo yanayowashika kina mama zaidi wengine huyaita kwa jina la majini (jinn) kwa kiarabu الجن ambalo ni neno lilitokana na kitenzi جن yaani kuficha/ kutoonekana kwa macho ya kawaida, kwakuwa akina mama wanaopatwa na hayo mapepo yasiyoonekana kwa macho ndipo waarabu wakayaita kwa jina "majini"-- lakini huo ni ugonjwa miongoni mwa magonjwa ya akili na kitaalamu ugonjwa huo unaitwa "Hysteria", wala hakuna kiumbe au viumbe vinavyotoka nje na vikamwingia mtu kichwani kama jinsi watu wengi wanavyoamini na kuaminishwa. Naam, katika lugha ya kiarabu inaruhusiwa bakteria wote (microscopic organism) kuitwa kwa kutumia jina "majini" kwa sababu tu ya sifa yao ya kutoonekana kirahisi, na baadhi ya maandiko ya kiarabu fasaha cha kale (clasic arabic) neno hilo limetumika kwa mnasaba huo.
Neno shetani kwa kiarabu ni شيطان (shaitwaan), ni kiumbe chochote kiovu chenye uhai.
Kwahiyo mkuu kipo kitengo maalumu cha kutibia hayo magonjwa ya akili ya aina hiyo? maana mara nyingi tunaona wenye hayo matatizo huenda kwa waganga,makanisani,masheikh na wengine hutibiana hapo hapo nyumbani.
 
Mkuu huo ni ugonjwa unaojulikana kitaalamu kwa jina la "Hysteria" ni miongoni mwa magonjwa ya akili na wataalamu wa magonjwa ya akili katika hospitali wanaujua ugonjwa huo na hasa huwapata akina mama/dada.

Inasemwa mtu anayepatwa na huo ugonjwa aghlabu anahitaji "kuliwazwa" tu mbali na kulishwa madawa, kuliwazwa kupo kwa aina nyingi na mojawapo ni; kumpigia muziki laini, kumuimbia nyimbo, kumsomea dua (kumbuka dua huwa ikisomwa katika mtindo wa wimbo), kumshika kichwani huku akikemewa kama wanavyofanya wachungaji, hii yote ni kujaribu kurudisha hali ya mgonjwa kujitambua.

Majini au mapepo au maruhani kama yanavyoitwa na wengi is nothing but Hysteria.
 
Kwa maana nyengine hili tatizo halina tiba ya kuliondoa kabisa na mtu akawa hana tena hilo tatizo bali kuna njia za kulituliza tu pale linapotokea? Na vp wengine tunaona wanabadili waganga,wachungaji na masheikh katika kutafuta tiba ya huo ugonjwa na huko kote unakuta mgonjwa amefanyiwa kama ulivyosema ila bado tatizo linakuwa palepale?
 
Mimi sio mjuzi nifikie hatua ya kusema kwamba hakuna dawa ya Hysteria, la hasha.

Ninachoweza kusema ni kwamba kuna hali fulani za kimaumbile na kitabia wanazo wanawake, hali hizo zikichangiwa na hali za kimazingira (environmental) hizo zinaweza kumfanya mwanamke/dada ashikwe na Hysteria, mfano mwanamke mwenye historia ya Hysteria anaweza kupandwa na Hysteria anapokumbana na harufi ya moshi wa baadhi ya mavumba yaliyochomwa, yaani yeye akinusa tu huo moshi basi akili yake mara moja inakuwa "Hysteric", na kuna vitu vingine kadhaa vikitokea huwafanya wawe na hali hiyo kulingana na kitu kipi humuathiri mgonjwa husika.

Na wapo wengine wakikaa muda mrefu bila kutimiziwa "haja" huwa ni taabu kubwa.🤣🤣.

Tabia nyingine ya akina mama/dada ni "emotional abd temperament" nayo huchangia pa kubwa katika hysteria.
 
Sasa kama sio mjuzi huoni kuwa hichi unachoeleza hapa kikawa tofauti uhalisia wa kilichopo huku mtaani mkuu? Kwani wewe binafsi ushawai kushuhudia haya matatizo katika uhalisia wake mbali na kusoma tu hizi habari?
 
Nimesema siyo mjuzi katika dawa, yaani siwezi kusema dawa ipo au haipo, unaposema dawa ipo maana yake mtu akipewa anapona kabisa na ugonjwa huo haurudi tena mimi katika hilo sijui ila ninachojua zipo dawa za kumtuliza yaani kumrudishia ufahamu wake kipindi ameshikwa na hayo mapepo (hysteria).

Kuna siku moja tukiwa kazini dada mmoja alishikwa na hali hiyo, wakatokea wanaume kama 4 hivi wakamdhibiti lakini alikuwa na nguvu za ajabu licha ya kudhibitiwa na njemba 4, ulikuwa ni mshikemshike hatari, mmoja wao akatoa wazo kumuona ustaadhi mmoja kutoka idara nyingine aende kutoa msaada na haraka akaenda kuitwa, yule ustaadhi alipofika tu kitu cha kwanza alimshika sikio na akaanza kumsomea surah Yasin, huku kadhibitiwa wakati watu wote wakiwa kimya wakati yule ustaadhi akiendelea kusoma, yule ustaadhi anasema ilimchukua kama dakika 3 hivi, yule mgonjwa akatulia na akili ikamrejea kitu cha kwanza akaomba maji na baadaye akapewa ruhusa kurudi nyumbani, kesho yake alipokuja kazini akamfuata yuke ustaadhi kutoa shukrani na akaenda mbali zaidi kuulizia dawa ya kumponyesha kabisa, yule ustaadhi akamwambia kuwa yeye hajui dawa zingine za kumponyesha kabisa mbali na dua za kuwasomea watu wenye matatizo kama yale mara tu yanapowatokea ila anaweza kwenda kwa wataalamu zaidi wa tiba.

Huyo ustaadhi alikuwa rafiki yangu na hichi kisa alinihadithia mwenyewe mchana kwasababu kilitokea katika shifti ya usiku. Mimi nikianza kumdadisi ili nijue yeye alikuwa anajua vipi juu ya hayo mapepo na ni kwa vipi ile dua iliweza kufanya kazi ya kumponesha yule dada kwa kipindi kile kwa sababu yule dada alikuwa anadai kwamba dalili za huo ugonjwa kumrudia bado alikuwa anazihisi.

Katika kujibu maswali yangu, ustaadhi aliniambia kwamba ni kwa uwezo wa Mungu tu ndipo akiweza kumsaidia yule dada.

Sasa angalia, mimi nilisema kwamba ugonjwa wa hysteria (mapepo/majini) ni miongoni mwa magonjwa ya akili kwa sababu mgonjwa anafanya mambo bila kujitambua na tiba yake kwa wakati huo ni kumliwaza ama kwa kumuimbia mziki laini au sauti yeyote inayoendelea kulia kwa kuliwaza huku ukiwa umemshika sikio au sehemu ya paji la uso kwa sababu sehemu iliyoathirika ni ndani ya kichwa/ubongo ambapo sikio au paji ni sehemu ya kichwa, yule ustaadhi alikuwa anasoma aya za Qur'an kwa kuimba huku ameshika sikio la yule mgonjwa na ndipo "senses" zikamrudia kwa muda mfupi. Njia hii pia hutumiwa na wachungaji wanapokemea pepo kwa sauti kali huku wakishika kichwa cha muathirika.

Kifupi ninasema sijui dawa ya kumponyesha kabisa mtu mwenye mapepo ila dawa ya kumtuliza na kumrejeshea utambuzi wake kipindi kapandisha mapepo njia ni kama hizo nilizokueleza zilizotumiwa na huyo ustaadhi au wachungaji.

Mshike mgonjwa kichwani tafuta mwimbo laini na umpigie au kama unaweza kuimba basi fanya hivyo, utaona matokeo yake kwa kipindi hicho.
 
Mkuu basi ni vizuri pengine ungefanya kauchunguzi kujionea zaidi kuhusu huo ugonjwa,sababu wengine wanapopata huo ugonjwa hawapigi kelele wala kufanya fujo unaweza huwa wanajitambua na mnaweza mkaongea na kuelewana na baadaye hiyo hali ikatoka bila kufanyiwa chochote(kumliwaza wala kumkalipia kwa kukemea) hili jambo nimelishuhudia mwenyewe. Lakini pia huu ugonjwa watu hupona kabisa ila hao wenye kutibu hawaiti huu kama ni ugonjwa wa akili bali hutambua ni jini/pepo limemuingia mtu na hivyo hufanya kulitoa au kuondoa hiyo hali yenye kufanya wapige kelele au hizo fujo.

Chengine unaweza kutuliza huo ugonjwa pale unapompata mtu kwa kumnusisha aina fulani ya mafuta huyo mgonjwa na hali ikatulia bila kumliwaza na haya mafuta ndio hutumika sana makanisani huko,sasa ndio najaribu kupima kati ya kinachosemwa na wataalamu wetu kuwa huo ni ugonjwa tu wa akili na si kwamba kuna kiumbe kimemuingia mtu Na wanaosema kuwa ni majini.
 
Huo ni ugonjwa wa akili unaoitwa Hysteria, na kuna hatua zake na athari tofauti kati ya mtu na mtu, ni ugonjwa wa akili kwa sababu unaathiri ubongo moja kwa moja.

Mgonjwa anaponusishwa dawa hiyo maana yake athari za dawa huenda kwenye ubongo kupitia puani kwa njia ya kunusa (olifactory sense ??), kwa sababu pua ni kiungo ambacho kazi yake imeungana moja kwa moja na ubongo kwa muktadha huo nakubaliana nawe kwamba zipo dawa za kunusa kwa ajili ya huo ugonjwa.

Yote kwa yote huwezi pinga kwamba huo si ugonjwa wa akili.
 
Mkuu mie sitaki kukupinga ila najaribu kupambanisha kati ya unachoeleza na kinachotokea kwenye uhalisia,huko mwanzo ulikuwa unasema njia ya kutuliza hiyo hali inapompata mgonjwa ni mkuliwaza kama kumuimbia(japo tunaona makanisani wanakemea) sasa hapa nimekutajia hiyo njia ya kumnusisha mafuta umekubaliana hiyo dawa kisa tu unasema inapita puani na kuingia kwenye ubongo ila hujari hayo mafuta yametengenezwa kwa kutumia nini hadi ikawa dawa yenye kuhusika na huo ugonjwa wa akili.

Binafsi sitaka matatizo mengine kama haya ni magonjwa ya akili tu ila kusema yote haya ni magonjwa tu ya akili na si vinginevyo hapo ndio palipo na tatizo.
 
Back
Top Bottom