Kwa maelezo yako unataka kutuaminisha kua hata virusi wa UKIMWI, maleria, nk wanaweza kuitwa (jin) kwasababu hawaonekani..?
Sawa kabisa, matumizi ya neno jinn katika kiarabu kwa ajili ya hivyo viumbe inaruhusiwa kabisa.
Kuna simulizi moja kutoka kwa mtukufu mtume Muhammad (saw), alipata kuwaonya waarabu katika zama zake waache kutumia vinyesi vikavu vya ngamia na mifupa ya wanyama kujichambia baada ya kwenda haja kama jinsi leo watu wanavyotumia toilet paper, mtume (saw) aliwaambia vitu hivyo ni vyakula vya majinni, ikumbukwe katika zama hizo Mtume (saw) aliwakuta warabu katika lindi la ushenzi mkubwa hivyo ilibidi kwanza awafundishe "ustaarabu/ adabu" (civilization/manners ) kulingana na mafundisho ya kiislamu na hivyo akawaambia badala yake watumei maji.
Katika zama hizo (takriban miaka 1400) iliyopita Waarabu hawakujua kwamba vinyesi na mifupa ya wanyama inaweza kuwa ni chakula cha Bakteria hivyo kuvitumia kujichambia wangeweza kujisababshia maambukizi katika sehemu za siri, lakini Mungu alimjulisha mtume wake juu ya jambo hilo na mtume (saw) akawatahadharisha wafuasi wake.
Leo kutokana na maendeleo ya elimu ya sayansi inawezekana kuwaona hao bakteria katika vinyesi kwa kutumia vifaa, bakteria hao wanakula kwa njia ya kuozesha (decaying).
Hivyo hao majinni aliowataja mtume (saw) ndiyo hao majinn.
Kuna simulizi lingine mtume (saw) alituasa tusome dua tunapoingia chooni ili kujikinga na majinni wanaoishi humo, majinn wanaoishi humo chooni sio viumbe wengine bali ni wadudu wadowadogo wa maradhi (microbes) wanaopatikana katika vinyesi vyetu sisi binadamu, mfano, wadudu wa kipindupindu, kuhara damu, wadudu wa kichocho nk, hao ndio majinn waishio chooni na wala hakuna eti jinn makata wala jinn Subiani au jinn mahaba tunaoaminishwa tuwakubali, huo i ujinga mtu na hakuna mtu mwenye akili timamu anaweza kukubali hadithi hizo za uongo.