Mkuu, Labda mimi sielewi unachosema na mimi hunielewi ninachosema, nasema hivi mapepo au maruhani au majini yanayowashika hasa kina mama na kina dada ni ugonjwa unaoathiri ubongo, kwakuwa unathiri ubongo ni lazima tuuite kwa jina jingine "ugonjwa wa akili" (mental disease) na kwa kitaalamu unaitwa Hysteria, waarabu wanaita Ruhani au jinn, unaitwa hivyo kwasababu muathirika huwa anafanya mambo ya ajabu bila kujitambua au bila ridhaa yake, mfano anaweza kupagawa kwa kujirusha na kuongea maneno ya ajabu au akaongea lugha mpya na maneno yasiyokuwa na mpangilio (ravings) kiasi kwamba inaonekana kana kwamba kuna nguvu isiyoonekana imo ndani ya huyo muthirika ndiyo inayomsukuma kufanya hayo matendo na ndipo waarabu wakaita (Ruhani au jinn)---- Ruhani ni "Roho" yenye tamaa au tashwishwi na jinn ni kitu kisichoonekana kwa macho.
Mimi nilikuwa nasema dawa nilizoshuhudia zikitumika kuwatuliza wagonjwa hao kwamba ni kuwaliwaza kwa muziki au sauti nyororo kama jinsi dua zinavyosomwa na kuwashika sikio au kwenye paji la uso kwa kufanya hivyo mganga anafanya kazi ya kurejesha akili ya mgonjwa, sikio na paji ni mahali palipo karibu na ubongo ambao kwa muda huo ndiyo uliokuwa affected kwa maana hiyo inakuwa ni njia rahisi ya mawasiliano ya karibu kati ya ubongo na hivyo viungo, hii inafanana kwa kiasi fulani na "acupuncture" ya Wachina ambapo wao hutumia sindano kutoboatoboa sehemu yenye ugonjwa.
Wewe umezungumzia juu ya dawa ya kunusa, mimi naafiki na zipo nyingine zaidi ya hizo tulizozitaja.
Ugonjwa huo unajulikana kama Hysteria na unawapata wanawake zaidi duniani pote, Wazungu, waarabu, waswahili nk,.
HUO NI UGONJWA WA AKILI, KWA SABABU UNAATHIRI UBONGO TU KATIKA MWILI WA BINADAMU.