Nini umuhimu wa ziara ya Rais Samia Ufaransa?

Nini umuhimu wa ziara ya Rais Samia Ufaransa?

Kwani safari zingine alizofanya zina faida gani 🤔🤔 ni muendelezo wa kuzurula tuu, bandari na ardhi vimeuzwa ujombani uarabuni sasa hivi ni bata kwa kwenda mbele hadi kuku waone wivu, lakini vina mwanzo na mwisho
 
Hii ziara ni yakutizama kwa jicho kavu, hawa wafaransa sio watu wema, mama wakiuliza una uraniam kataa katakata waambie haipo, wakisema una lithiam waambie sidhani, waambie tunao simba nyati twiga swala na ile great nyumbu migration wanaweza kuja kutalii ila sio kuondoka nao, waambie kipo kisiwa cha chumbe pale panafaa sana kwa vacation, wakiuliza wale jamaa zetu wa lgbt waambie wana kajiuchaguzi kao ka ndani kanawatia hofu, ngoja wamalize,
 
Mikutano kama hii bila M7 na paka ni makongamano tu
 
Rais Samia huyoo?
Sasa hivi kaenda Ufaransa!

Ufaransa, chini ya Macron, sasa hivi kimataifa haivumi upepo mzuri. Matukio ya uhusiano wa Ufaransa na nchi za Afrika Magharibi, kama Niger, Mali, Burkina Faso na nchi nyingine siyo mzuri kabisa.

Nchi hizo za wenzetu zime experience ushenzi wa ukoloni mamboleo wa dola la kifaransa. Uchumi wa nchi hizo ulidhibitiwa na ufaransa kiasi kwamba walikuwa wakinyonywa mchana kweupe. Sasa wamewafukuza physically wafaransa wote toka nchini mwao.

Katika mazingira hayo lazima tujiulize, Mama Samia anafuata nini huko Ufaransa, na atatendewa nini tofauti na nchi za Afrika Magharibi?

Anatafuta wateja.

Nadhani Mlima Kilimanjaro bado haujapata mteja.
 
Back
Top Bottom