Nini yatakuwa matokeo kwa mtu ambae atakunywa maziwa ambayo ndani yake yametiliwa sumu?

Hakuna lolote litalalompata huyo atakayekunywa hayo maziwa
Mbona hauwi specific? Yani sumu iwekwe kwenye maziwa kisha hiyo sumu isimdhuru?

Kwani unaongelea sumu aina ipi? Coz kuna sumu hata unywe debe la maziwa lazima ikuondoe.
 
Habari za wakati huu ndugu zangu wana jamii, naomba kuuliza ni nini kitatokea endapo mtu atakunywa maziwa ambayo ndani yake yametiliwa sumu, ukizingatia maziwa huwa tunayatumia kumpa mtu aliye kula sumu kabla ya kumpeleka hospitali kwa matibabu zaidi
Inategemea ni sumu ya aina gani na maziwa ya aina gani...
 
Hii kitu sijui wabongo waliitolea wapi yani? Haipo kwenye literature yoyote duniani na wanaoamini ni watz tu hadi karne hii ya information at your fingertips, kwamba sumu inamalizwa na maziwa 😅😅
 
Habari za wakati huu ndugu zangu wana jamii, naomba kuuliza ni nini kitatokea endapo mtu atakunywa maziwa ambayo ndani yake yametiliwa sumu, ukizingatia maziwa huwa tunayatumia kumpa mtu aliye kula sumu kabla ya kumpeleka hospitali kwa matibabu zaidi
Like charges repel while unlike charges attract,
 
Habari za wakati huu ndugu zangu wana jamii, naomba kuuliza ni nini kitatokea endapo mtu atakunywa maziwa ambayo ndani yake yametiliwa sumu, ukizingatia maziwa huwa tunayatumia kumpa mtu aliye kula sumu kabla ya kumpeleka hospitali kwa matibabu zaidi
Kunywa maziwa ambayo tayari yametiliwa sumu ni hatari sana kwa afya. Ingawa maziwa mara nyingine hutumika kama njia ya dharura kusaidia kupunguza athari za sumu fulani, si kila aina ya sumu itazuiliwa au kufyonzwa na maziwa. Ikiwa maziwa yenyewe yamechafuliwa na sumu, basi:
  1. Sumu itapenya mwilini: Mtu atakunywa sumu moja kwa moja, ambayo inaweza kusababisha madhara ya kiafya kulingana na aina na kiasi cha sumu hiyo.
  2. Hakuna kinga dhidi ya sumu hiyo: Maziwa yatakayoingia mwilini yamechafuliwa, hivyo hayatasaidia kufyonza wala kupunguza athari za sumu hiyo.
  3. Madhara ya kiafya: Madhara yanaweza kuwa makubwa na haraka, kama vile kichefuchefu, kutapika, kuhara, au hata sumu kufika viungo muhimu kama ini, figo, au mfumo wa neva.

Hatua za kuchukua:​

  • Epuka kunywa maziwa au chakula chochote ambacho huna uhakika wa usalama wake.
  • Ikiwa mtu amekunywa maziwa yenye sumu kwa bahati mbaya, peleka haraka hospitali kwa matibabu ya dharura.
  • Usitumie maziwa kama njia ya kinga bila ushauri wa kitaalamu, hasa kama haijulikani sumu iliyotumiwa.
Maziwa ni msaada kwa sumu maalum kama asidi au vitu vyenye ukali, lakini kwa sumu fulani (kama zile za kemikali au dawa za kuulia wadudu), yanaweza hata kuongeza madhara. Daima tafuta msaada wa kitaalamu haraka.
 
Inaishiwa nguvu, kama uhamini changanya maziwa na konyagi then kunywa na flajero sijui ndio inavoandikwa,uone.
 
Habari,
Hatari ya kudhurika iko pale pale kutegemeana na aina ya sumu na kiwango cha maziwa.

Maziwa yanatumika kupunguza kwa muda sumu kufyonzwa na mwili. Katika jitihada za kupunguza athari ya sumu mwilini, mtu aliyekunywa sumu anaweza kunyweshwa maziwa, ama aina zingine za dawa ambazo zinashikana na sumu hivyo kupunguza sumu kuingia kwenye damu na kuleta madhara. Lakini, hiyo sio njia inayotosheleza kuepusha madhara ya sumu, Bali inatumika kupunguza.

Hivyo, ukinywa maziwa yenye sumu utadhurika kama kawaida.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…