Ninunue bajaji iniingizie pesa au ninunue gari nami nionekane mtu ila linitese?

Aisee . Okk .
 
Mimi nakuambia hivi; kama gari itakuwa lazima, labda kutokana na nature ya shughuli zako za kika siku, kama vile kuwahi kazini, biashara, nk, hapo nunua gari ya kiwango chochote kile. Lakini endapo unataka kununua gari kwa ajili ya show off, achana nayo, ni bora ukaiwekeza hiyo hela ili ujiingizie faida kuliko kununua gari ambayo itahitaji kuihudumia! Kulingana na maelezo yako, inaonekana hela yenyewe haizidi shs 8000000/=, ni bora ukaiingiza kwenye mzunguko ili baadae mambo yakikaa vizuri, uje ununue chombo ya uhakika; kama Harrier, Vanguard, X-Trail (SVU cars), nk, kuliko sasa ukiamua kununua, hautakuwa na option zaidi ya kununua Vitz!
 
Mnhh .. mkuu.
Pata potea sio poa.

Mzunguko ndo huo.
 
Nilinunua IST kuifanya Uber/Bolt nilichokutana nacho mwaka wa nne huu naiendesha Mwenyewe kwenye shughuli zangu. Biashara ya transport madereva ni pasua kichwa inatakiwa mmiliki uwe pasua kichwa zaidi yao ndiyo utatoboa
 
Hata iyo bajaji labda kama utaendesha mwenyewe ila ukijichanganya kuwapa hawa vijana wanaovaa jinsi za kubana kama dada zao utakula hasara tu. Ushauri wangu kama una muda fanya biashara utakayoweza kuismamia mwenyewe mguu kwa mguu angalao kwa hatua za mwanzo
 
Duh.. !
Hapo kwa mguu kwa mguu ndo ishu..
 
Duh.. !
Hapo kwa mguu kwa mguu ndo ishu..
Kwa hatua za mwanzo ni hatari sana kukaa mbali na biashara hata umpe rafiki au ndugu atakupiga tu. Ushauri wangu tafuta chimbo fungua car wash ya kijanja janja kidogo magari, bajaji, pikipiki, kirikuu vyote vinaoshwa alafu usicheze mbali ukishajua mzunguko upoje unaweza kuwapangia hesabu vijana alafu we unapita kuchukua hesabu jioni au kwa muda mliokubaliana
 
Au Suzuki swift
 
Maana yake asilale?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…