Nioe mke mwingine?

mulama jahazi limezama kaka huna chako,sio wewe tu uliyepatwa na maswahiba kama haja wapo wengi saaana wamepata na wanaendelea kupata. Nakushauri anza maisha mapya .kuna watu wanakushauri eti mmekaa miaka kumi na moja ni mingi ,let me tell you something........ huyo dada ni kama atom ambayo mwanzo ilikuwa stable na kwa bahati mbaya amekuwa subjected kwenye external (other energy) ambayo imemfanya abadilike .hawezi rudi hali ya zamani kaka........fafuta maisha mengine..........zaidi zaidi subiri ukimwi ndani sasa
kukubali kushindwa wakati mwingine ni ushujaa kaka
 
Well uamuzi ni wako kaka...sisi tunakupa ushauri vile tunavyoona inafaa wewe uchukue alafu changanya na zako.Ila angalia kesho kutwa usije ukarudi unalia umekamatika sehemu maana akili yako haikua huru kuchagua kwa uangalifu...angalia tu usije ukaruka majivu na kukanyaga moto!!!
 
tatizo la dada zetu most of them ...........most of them.............wakiwa na kipato zaidi ya mume ndoa matatizo kila siku........hawakumbuki nyuma ambako labda mume alikuwa anafanya viiiitu vyooooote
sasa hiyo ya kusema hajanioa bali tumeoana mnaitaka ya nini?..................kuoana means everybody owes everything,,,,,,,,,,,,,
 

Nakushukuru kwa umakini wako mkuu ila sasa nakushauri upitie upya "the art of the representations" utapata majibu yote. unajua nyie wasomi mnajua mengi kunizidi nisiyesoma inawezekana ukashindwa ku premise hoja zangu kwa sababu zina miss comprehensiveness component!
 

Ndugu Mulama, kwa kaumri nilikonako, asikudanganye mtu hakuna mwanamke anayetaka mwanaume goalkeeper! Kama Michelle alivyoshauri, tafuta kazi uwe na kipato. Ukikurupuka kuoa mke wakati huna kipato utakuwa umeruka majivu umekanyaka moto. Tafuta kazi uwe na kipato ulee mwanao na kama kuoa ije baada ya kuwa una msimamo.
 


Ndio mkuu nyumba ni ya kupanga. Pia ahsante kwa ushauri
 
Nashukuru sana kwa michango yenu, imekuwa ya manufaa sana kwangu. Nimeamua kusubiri sitakurupuka kuoa tena nitajitahidi kutafuta kazi japokuwa si kazi rahisi kupata kazi, kuhusu yeye nadhani aendelee na maisha yake nami niwe peke yangu na mwnangu, pengine itanisaidia kupunguza mawazo yanayosababishwa na kumuona akiwa katika hali ya kunikataa na masimango pia.

Ahsanteni sana na Mungu awabariki awazidishie hekima, akili, maharifa na busara ili muweze kuwasaidia na wengine, tuzingatie kuwa haya ni matatizo ya kijamii katika ulimwengu wa sasa tunaouishi, hivyo ni vyema tukapeana ushauri, mwongozo na maelekezi bora ya kuyatatua.

Na kwa kufanya hivi tutapunguza uwezekano wa e.t.c, yaani end of thinking capacity ambayo upelekea mtu kuamua kujinyonga!
 

Yawezekana anawakilisha matatizo ya wengine toka kwa ndugu,jamaa,marafiki na jamii kwa ujumla ,cha msingi hapa nafikiri ni ushauri
 
wanawake wakiwezeshwa ,kweli wanaweza.......................................
The Boss malizia sentensi yako naona kama haijakamika.
Vipi nikimalizia hivi?
Wanawake wakiwezeshwa,kweli wanaweza nyanyasa wanaume😛eep:
 
Duh kweli hii ndio inaitwa maskini akipata ****** hulia mbwata!!!! yaani kama mie hapa alivohangaika na mie mpaka hapa nilipo alinioa niko form four tu maskini, leo hii nifanye visa hata Mungu atanichapa bao la uso... watu huwa tunasahau sana tulikotoka na kujiona wa maana ila jitahidi na wewe kusoma elimu haina mwisho utapata tu kazi
 
halafu mwanamke kama huyu baadae mambo yako yanakuwa super ndio anaanza oohh mume wangu oohh cjui kitu gani na gani, bibadamu wengine utu hawana kabisa aise.
 
halafu mwanamke kama huyu baadae mambo yako yanakuwa super ndio anaanza oohh mume wangu oohh cjui kitu gani na gani, bibadamu wengine utu hawana kabisa aise.
Yaaaaani kaniudhi kweli huyu mama ambiliki, hata uso wa haya amekosa eee
 
Fikia muafaka kwanza na huyo bibie,then ndo unaweza kufikiria issue zingine.Maana akina mama wakifanikiwa kidogo tu mabega juu.
 
Mulama hapo ishakula kwako. Kwa ujumla ni kuwa mkeo kashapata mahala pengine pa kujihifadhi. Mungu mwema atakuponya na maumivu hayo
 
That's not a wife pal! Find yourself another woman. She possible agreed to mary you just because you were helping her!
 


Najaribu kuconect dot....nitarudi
 
...mke mbogo, anajidai, anakunyanyasa wewe na mtoto wako, nyumba ya kupanga, huna kazi...
Yote hayo ni magumu kwa kweli. Baada ya kupitia michango yote, ninaweza kufupisha yafuatayo:
1. Usitende ihsani kwa kungoja shukurani: umemsomesha kama wajibu au mapezi yako, huna haki ya kudai kulipwa kwa hili.
2. Hakuna ushauri, dawa, shetani wala mizizi itayomfanya ageuke nyuma na kutafakari mlikotoka, kwa hivyo msahau kama mke.
3. Usijione mnyonge kwa kufanya kazi za ndani, kama wewe ungekuwa na kazi yeye hana, yeye angefanya kazi hizo.
4. Tafuta ajira yoyote, hata umachinga wa kuuza pipi na maji ya kunywa ili uweze kujisaidia na kumsaidia mtoto wako. Mtoto wa mkewako kusoma international isikupe joto. Mara nyengine kusoma kwa shida ni changamoto kwa mtoto kuifahamu hiyo hali na kukaza kamba.
5. Hakuna hata mmoja aliyekushauri kuoa mke mwengine,kwa hiyo hilo lisahau kabisa vyengine utakuja kuruka maji na kukanyaga tope. Mada yako na sehemu fulani ya majibu yako ilionesha kama tayari hilo la kuoa mke mwengine lilikuwa wazo ulilonalo kabla na ushauri wowote usingesaidia, lakini baadaye umefahamu na ninakupongeza kwa hilo.
6. Kwa kuwa mmo katika nyumba ya kupanga, inawezekana yeye ndiye analipia kodi, vumilia hapo hapo na gawa wakati wako vizuri baina ya kufanyakazi za nyumba na kazi za kukupatia riziki. Huwezi hivyo, fuata ushauri uliopewa wa kumpeleka mtoto wako kwa wazazi wako ili uwe na muda mwingi wa kutafuta/kufanya kazi.

Pole sana mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…