Nioe mke mwingine?

Nioe mke mwingine?

mulama jahazi limezama kaka huna chako,sio wewe tu uliyepatwa na maswahiba kama haja wapo wengi saaana wamepata na wanaendelea kupata. Nakushauri anza maisha mapya .kuna watu wanakushauri eti mmekaa miaka kumi na moja ni mingi ,let me tell you something........ huyo dada ni kama atom ambayo mwanzo ilikuwa stable na kwa bahati mbaya amekuwa subjected kwenye external (other energy) ambayo imemfanya abadilike .hawezi rudi hali ya zamani kaka........fafuta maisha mengine..........zaidi zaidi subiri ukimwi ndani sasa
kukubali kushindwa wakati mwingine ni ushujaa kaka
 
Ni kweli usemayo lakini jamani hivi kweli mimi sina haki ya kuliwazwa katika magumu haya?!, mwenzangu ana ponda life yaani kanisahau kabisa, pia kuna suala la kimwili ambalo sijalisema hapa namimi ni mtu mzima niliyekamilika sana kijinsia navumilia kutopata haki hii kwa muda mrefu wakati nahisi mwenzangu anapata ndio maana hana tena shida na mimi.Nakula kwa kufanya vibarua vya kazi ndogo ndogo si kama mimi na mtoto tunamtegemea yeye keshatubwaga kabisa! hasa ukizingatia kuwa wa kwake yuko boarding.Pia tusisahau kuwa ajira zenyewe ni taabu siku hizi hata kwa wasomi wenye shahada zao kwangu nikisubiri kujijenga si nitazeeka manake inabidi nirudi shule ili nipate kazi.uamuzi wa kutafuta mwingine nimeufanya kwa mpangilio kwa mfano nilipojiunga na jf ilikuwa njia mojawapo ya kutafuta faraja kwa kubadilishana mawazo kama hivi, ndio maana utaona sikulisema hili mwanzo mpaka nilipoelewa utaratibu wa mada zinavyowasilishwa.kwa hiyo nitakayempata atajua nimekosa nini huko kwa awari na tutazungumzia uwezekano wa mapenzi ya dhati kabla ya kupiga hatua zaidi.
Well uamuzi ni wako kaka...sisi tunakupa ushauri vile tunavyoona inafaa wewe uchukue alafu changanya na zako.Ila angalia kesho kutwa usije ukarudi unalia umekamatika sehemu maana akili yako haikua huru kuchagua kwa uangalifu...angalia tu usije ukaruka majivu na kukanyaga moto!!!
 
tatizo la dada zetu most of them ...........most of them.............wakiwa na kipato zaidi ya mume ndoa matatizo kila siku........hawakumbuki nyuma ambako labda mume alikuwa anafanya viiiitu vyooooote
sasa hiyo ya kusema hajanioa bali tumeoana mnaitaka ya nini?..................kuoana means everybody owes everything,,,,,,,,,,,,,
 
Kuna mada ulikuja nayo hapa ukisema kama nakumbuka vizuri uamini ndoa. Kuna siku nikakushauri umtokee yule mheshimiwa wa kawe kwani yeye ataka mtoto tu si kuolewa. Kuna nyingine ulisema nyie medical doctors mna ethics. Sasa hii unasema wewe ni std seven. Anyway michango ni muhimu kwa wale wenye situation kama hiyo.

Nakushukuru kwa umakini wako mkuu ila sasa nakushauri upitie upya "the art of the representations" utapata majibu yote. unajua nyie wasomi mnajua mengi kunizidi nisiyesoma inawezekana ukashindwa ku premise hoja zangu kwa sababu zina miss comprehensiveness component!
 
Pole sana Mulama, mi nakusisitiza usikimbilie kumuacha mkeo,naomba utafute kazi au namna ya kujiendeleza. Ni rahisi sana watu kumuona huyo mwanamke mbaya lakini nikuhakikishie wanawake wengi hawatakuwa tofauti na huyo mama. Kama baba wa familia jitahidi nawe uingize kipato hata kama ni kidogo na pia kwenda kazini itakupunguzia stress unazopata sasa,atleast kule uta interact na watu,utakuwa na marafiki ambao kwa namna moja au nyingine watakuwa msaada kwako hata kama ni wa kisaikolojia. Nakutakia kila la kheri.

Ndugu Mulama, kwa kaumri nilikonako, asikudanganye mtu hakuna mwanamke anayetaka mwanaume goalkeeper! Kama Michelle alivyoshauri, tafuta kazi uwe na kipato. Ukikurupuka kuoa mke wakati huna kipato utakuwa umeruka majivu umekanyaka moto. Tafuta kazi uwe na kipato ulee mwanao na kama kuoa ije baada ya kuwa una msimamo.
 
mkuu pole kama ni kweli
ningependa kujua hiyo nyumba mmepanga au ni yenu
vyovyote vile hama muage vizuri mtoto mhamishie kwa wazazi au nduguzo
hamia mkoa mwingine katafute kazi au anza biashara
kama ana chembe ya mapenzi atakutafuta
kama hana atajuta kumkosa houseboy na hiyo utaiona wakati mkiwasiliana
kwa yeye kukaa mwenyewe na wewe kuwa mwenyewe utaweza kuwa free thinking
usikimbilie kuoa kwanza tafuta pesa si unajua "ukitafuta wanawake utapoteza pesa ukitafuta pesa wanawake watakufuata"
ukikaa mwenyewe kwa miezi mitatu mpaka sita utajua ukweli ingawa hilo suala la kutoa mimba ina maana hapo future hakuna ila kaa mwenyewe kwa muda pata kazi wakati hujamuacha officially then ukitulia utakuwa na maamuzi ya busara


Ndio mkuu nyumba ni ya kupanga. Pia ahsante kwa ushauri
 
Nashukuru sana kwa michango yenu, imekuwa ya manufaa sana kwangu. Nimeamua kusubiri sitakurupuka kuoa tena nitajitahidi kutafuta kazi japokuwa si kazi rahisi kupata kazi, kuhusu yeye nadhani aendelee na maisha yake nami niwe peke yangu na mwnangu, pengine itanisaidia kupunguza mawazo yanayosababishwa na kumuona akiwa katika hali ya kunikataa na masimango pia.

Ahsanteni sana na Mungu awabariki awazidishie hekima, akili, maharifa na busara ili muweze kuwasaidia na wengine, tuzingatie kuwa haya ni matatizo ya kijamii katika ulimwengu wa sasa tunaouishi, hivyo ni vyema tukapeana ushauri, mwongozo na maelekezi bora ya kuyatatua.

Na kwa kufanya hivi tutapunguza uwezekano wa e.t.c, yaani end of thinking capacity ambayo upelekea mtu kuamua kujinyonga!
 
Kuna mada ulikuja nayo hapa ukisema kama nakumbuka vizuri uamini ndoa. Kuna siku nikakushauri umtokee yule mheshimiwa wa kawe kwani yeye ataka mtoto tu si kuolewa. Kuna nyingine ulisema nyie medical doctors mna ethics. Sasa hii unasema wewe ni std seven. Anyway michango ni muhimu kwa wale wenye situation kama hiyo.

Yawezekana anawakilisha matatizo ya wengine toka kwa ndugu,jamaa,marafiki na jamii kwa ujumla ,cha msingi hapa nafikiri ni ushauri
 
wanawake wakiwezeshwa ,kweli wanaweza.......................................
The Boss malizia sentensi yako naona kama haijakamika.
Vipi nikimalizia hivi?
Wanawake wakiwezeshwa,kweli wanaweza nyanyasa wanaume😛eep:
 
Duh kweli hii ndio inaitwa maskini akipata ****** hulia mbwata!!!! yaani kama mie hapa alivohangaika na mie mpaka hapa nilipo alinioa niko form four tu maskini, leo hii nifanye visa hata Mungu atanichapa bao la uso... watu huwa tunasahau sana tulikotoka na kujiona wa maana ila jitahidi na wewe kusoma elimu haina mwisho utapata tu kazi
 
halafu mwanamke kama huyu baadae mambo yako yanakuwa super ndio anaanza oohh mume wangu oohh cjui kitu gani na gani, bibadamu wengine utu hawana kabisa aise.
 
halafu mwanamke kama huyu baadae mambo yako yanakuwa super ndio anaanza oohh mume wangu oohh cjui kitu gani na gani, bibadamu wengine utu hawana kabisa aise.
Yaaaaani kaniudhi kweli huyu mama ambiliki, hata uso wa haya amekosa eee
 
Fikia muafaka kwanza na huyo bibie,then ndo unaweza kufikiria issue zingine.Maana akina mama wakifanikiwa kidogo tu mabega juu.
 
Mulama hapo ishakula kwako. Kwa ujumla ni kuwa mkeo kashapata mahala pengine pa kujihifadhi. Mungu mwema atakuponya na maumivu hayo
 
That's not a wife pal! Find yourself another woman. She possible agreed to mary you just because you were helping her!
 
Ndugu zangu naombeni msaada kwenye kisa hiki cha kweli . nina mke tuliyefunga ndoa yapata miaka 11 iliyopita, mke wangu tulikutana kazini kwenye kiwanda cha kutengeneza biscuits ambapo yeye alikuwa teller mimi ni mwendesha mashine.
Baada ya kuoana nilimwendeleza kimasomo kwakuwa yeye alikuwa wa form IV nami ni darasa la saba, kwakuwa alifanya vizuri katika kozi zake alifanikiwa kupata kazi kwenye shirika moja la kimataifa kama administrative secretary.
Sisi huku kiwanda kilifungwa kutokana na biscuits kukosa masoko kutokana na ushindani uliopo hivyo nikalazimika kukaa nyumbani huku nikijitahidi kutafuta vibarua vya hapa na pale.
Issue ni kwamba mke wangu sasa amekuwa mbogo hataki kusaidia kitu chochote hapa nyumbani na ikitokea akatoa hela basi masimango yanatisha, tutaitwa majina ya kila aina mara poyoyo, mara Mario nk.
Wakati tunaoana kila mmoja alikuwa na mtoto na wote tulikuwa tunawalea kwa mapenzi bila ubaguzi, cha kushangaza yeye mtoto wake kampeleka international school wa kwangu amemwacha aendelee na hizi za kayumba!
Kinachonipa taabu sana ni kurudi usiku wa manane wakati mwingine akiwa amelewa nikimuuliza anasema walikuwa na kazi nyingi na mikutano inayoambatana na vinywaji, pia ana safari nyingi za kikazi na akifika huko huwa hataki nimpigie simu eti namsumbua!
Sasa je huyu bado anastahili kuwa mke wangu? Si kawa wa mataifa sasa niachane naye nikaoe mwingine?
Vikao vya wazee vimeshindwa kutoa ufumbuzi wanamuogopa au sijui ni kwamba anawakatia mkwanja mrefu?!
Nawasilisha

Ni tafakuri jadidi katika mkutadha huu, je wadau nyakati hizi tulizo nazo kuna haja ya kuoana? Ikiwa tendo la kuzaa na kuijaza dunia tuliloagizwa na maulana tunalitimiza kikamilifu nje ya utaratibu huu wa kuoana na imefikia mahala hata wengine hatutaki tena kujaza dunia tuna abort au kuua vi offspring vyetu kinyume na mpango wa mola!
Mimi naona mpaka hapo kuoana ni uchoyo tu wa kutaka mtu mmoja kushikilia mwenzie na kuwanyima fursa wengine kuongeza dunia hapohapo!
Mnasemaje wadau?

Najaribu kuconect dot....nitarudi
 
...mke mbogo, anajidai, anakunyanyasa wewe na mtoto wako, nyumba ya kupanga, huna kazi...
Yote hayo ni magumu kwa kweli. Baada ya kupitia michango yote, ninaweza kufupisha yafuatayo:
1. Usitende ihsani kwa kungoja shukurani: umemsomesha kama wajibu au mapezi yako, huna haki ya kudai kulipwa kwa hili.
2. Hakuna ushauri, dawa, shetani wala mizizi itayomfanya ageuke nyuma na kutafakari mlikotoka, kwa hivyo msahau kama mke.
3. Usijione mnyonge kwa kufanya kazi za ndani, kama wewe ungekuwa na kazi yeye hana, yeye angefanya kazi hizo.
4. Tafuta ajira yoyote, hata umachinga wa kuuza pipi na maji ya kunywa ili uweze kujisaidia na kumsaidia mtoto wako. Mtoto wa mkewako kusoma international isikupe joto. Mara nyengine kusoma kwa shida ni changamoto kwa mtoto kuifahamu hiyo hali na kukaza kamba.
5. Hakuna hata mmoja aliyekushauri kuoa mke mwengine,kwa hiyo hilo lisahau kabisa vyengine utakuja kuruka maji na kukanyaga tope. Mada yako na sehemu fulani ya majibu yako ilionesha kama tayari hilo la kuoa mke mwengine lilikuwa wazo ulilonalo kabla na ushauri wowote usingesaidia, lakini baadaye umefahamu na ninakupongeza kwa hilo.
6. Kwa kuwa mmo katika nyumba ya kupanga, inawezekana yeye ndiye analipia kodi, vumilia hapo hapo na gawa wakati wako vizuri baina ya kufanyakazi za nyumba na kazi za kukupatia riziki. Huwezi hivyo, fuata ushauri uliopewa wa kumpeleka mtoto wako kwa wazazi wako ili uwe na muda mwingi wa kutafuta/kufanya kazi.

Pole sana mkuu.
 
Back
Top Bottom