...mke mbogo, anajidai, anakunyanyasa wewe na mtoto wako, nyumba ya kupanga, huna kazi...
Yote hayo ni magumu kwa kweli. Baada ya kupitia michango yote, ninaweza kufupisha yafuatayo:
1. Usitende ihsani kwa kungoja shukurani: umemsomesha kama wajibu au mapezi yako, huna haki ya kudai kulipwa kwa hili.
2. Hakuna ushauri, dawa, shetani wala mizizi itayomfanya ageuke nyuma na kutafakari mlikotoka, kwa hivyo msahau kama mke.
3. Usijione mnyonge kwa kufanya kazi za ndani, kama wewe ungekuwa na kazi yeye hana, yeye angefanya kazi hizo.
4. Tafuta ajira yoyote, hata umachinga wa kuuza pipi na maji ya kunywa ili uweze kujisaidia na kumsaidia mtoto wako. Mtoto wa mkewako kusoma international isikupe joto. Mara nyengine kusoma kwa shida ni changamoto kwa mtoto kuifahamu hiyo hali na kukaza kamba.
5. Hakuna hata mmoja aliyekushauri kuoa mke mwengine,kwa hiyo hilo lisahau kabisa vyengine utakuja kuruka maji na kukanyaga tope. Mada yako na sehemu fulani ya majibu yako ilionesha kama tayari hilo la kuoa mke mwengine lilikuwa wazo ulilonalo kabla na ushauri wowote usingesaidia, lakini baadaye umefahamu na ninakupongeza kwa hilo.
6. Kwa kuwa mmo katika nyumba ya kupanga, inawezekana yeye ndiye analipia kodi, vumilia hapo hapo na gawa wakati wako vizuri baina ya kufanyakazi za nyumba na kazi za kukupatia riziki. Huwezi hivyo, fuata ushauri uliopewa wa kumpeleka mtoto wako kwa wazazi wako ili uwe na muda mwingi wa kutafuta/kufanya kazi.
Pole sana mkuu.