Nionavyo mimi: Miaka kumi ya Rais Magufuli umasikini utaongezeka sana

Serikali imenyosha haswa makampuni na hizo kodi... nyingi zimefungwa...

Watu pesa hawana... hali ni ngumu haswa... Umasikini unazidi kutamalaki...



Cc: mahondaw
 

Lini watanzania wa kawaida walikuwa matajiri ? Kama sio wana siasa, na wale walioajiriwa kwenye ofisi za umma na kupiga deals? Rushwa ndio iliwabeba sana watu.
Ili umaskini uondoke, ni wajibu wa kila mtu kupambana ilivyo kuuepuka.
Kuiba fedha za walipa kodi kwa kisingizio cha kulipana posho au kupeana safari ili kuongezea kipato ni dhambi na uhalifu.
Turudi kwenye drawing board na kuamua kwa dhati kuchukua hatua za kweli kuutokomeza umaskini. Kumsingizia JPM sio sawa as if sisi ni malaika na hatuna mchango wa shida zinazotuzunguka
 
Kuwekeza Chato na dodoma kuna nufaisha vipi kizazi kijacho.Maisha ni Sasa na si kesho.Hao wakoloni awakujenga kwa ajili ya kesho walijenga kwa kuanza kufaidisha kizazi cha wakati ule Hadi Sasa tukinufaika na maendeleo waliotuachia wakoloni.
 
Umasikini unatengenezwa makusudi na watawala ili waweze kutawala watu.Leo kuimba kwaya Hadi na wasomi ndio cv ya kazi.
 
Hayo ni maoni yangu kama yalivyo yangu. Lakini Watanzania walio wengi "site" wanamkubali. Anataka kingine kipi zaidi ya hicho?
"Lakini Watanzania walio wengi "site" wanamkubali."

Uzuri ni kwamba haya nayo ni maoni yako tu..., na sio ukweli halisi.
 

Wastaafu kutolipwa mafao yao si haki, pesa ya mifuko imepelekwa kwenye miradi . Halafu mtu anakwambia serikali ni tajiri ina mapesa!!!
 
Na kikibaki mtandaoni mafao ya wastaafu yatakua yanawahi kulipwa huku tukiendelea kua super donor country.
Mafao yanalipwa vizuri tu. Ofisi ninayofanyia kazi kuna wastaafu wawili. Mmoja alistaafu mwezi Aprili, 2019 na mwingine Juni, 2019. Wote hao tangu mwaka jana walipokea fedha zao na wanaendelea vizuri tu maisha baada ya kustaafu. Nawashangaa ninyi wa mitandaoni.
 
"Lakini Watanzania walio wengi "site" wanamkubali."

Uzuri ni kwamba haya nayo ni maoni yako tu..., na sio ukweli halisi.
Nafikiri humu kila mtu anatoa maoni yake. Au wewe unaelekezwa cha kuandika? Ahahahahahah!
 
Hakika
 
Uzuri wewe peke yako hapa JF ndio unafanya kazi huko ofisini.
 
Profesa Rwekaza Sympho Mukandala anazungumzia kigezo muhimu cha uongozi, ambacho ni je wananchi wanafuraha?

Prof. Mukandala anasema haitoshi baba wa nyumba kuleta nyama, samaki na chakula kila siku nyumbani lakini familia yake inaishi bila furaha.


Kipimo cha kutengeneza miundombinu lukuki na kulazimisha watu waridhike wakati wananchi hawana furaha kutokana na ukata kuwepo ktk shughuli zao za kujiingizia kipato huku wakiwa hawana furaha kwa kukosa pesa na umasikini unaosababishwa na sera za kiuchumi za serikali kukazania Maendeleo ya Vitu na kusahau kabisa Maendeleo ya Watu.
Source :
25 Nov 2018
African Intellectuals
Hali ya Uchumi na Siasa Nchini Tanzania Miaka mitatu ya Serikali ya Awamu ya Tano: "Tunatoka wapi, Tuko wapi na Tunakwenda wapi"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…