Nionesheni bodaboda aliyeagiza gari Japan au China kwa kipato cha bodaboda niache kazi ya utumishi wa umma ndani ya saa 24

Turudi kwenye Socialism nadhan tatzo ni system ya gvt na utawala ,lack of equal access of resources to all people
 
Shenzi taipu! Huu uzi wako ndo uzi bora wa mwaka.

Naomba waambie hao bodaboda tuliowaajiri kuwa wawe na adabu. Nipo nafanya mikakati ya kuagiza premio kali kabisa toka Japan

Form za mkopo walipitisha tayari?
 

Ukimuona bodaboda ana maendeleo basi huyo alikuwa kwenye transition tu ,alipita hapo wakati akisubiria michongo itiki ,nilishwahi kumuona jamaa sehemu alikuwa amechoka sana ,alihamia kwake nyumba bati kaezeka nusu ,akaanza bodaboda alikuwa anaifanyia sehemu tofauti na kwake.

Baada ya muda akaikarabati nyumba yake fresh,akamalizia bati nyumba nzima ,akaipiga rangi,akaweka PVC ,akanunua na gari ila bodaboda wenzake wakimuona ili wajifariji ndiyo utasikia jamaa alikuwa bodaboda lakini alikuwa anasikilizia mchongo na ulivyotick akaachana nayo.
 
Ni ujinga kuwaza kuwa gari ndo maisha ya juu wakati pikipiki pia ni chombo cha usafiri. Waziri mkuu wa uingereza hana gari wala bodaboda hutumia baiskeli tu. Unamzidi nini wewe mwenye ist ya mkopo
 
Sasa nyinyi ambao hamtaki wafanye bodaboda mtawapa kazi gani za kufanya?....

Siasa bwana [emoji16]
 
Ukweli kuhusu Bodaboda ni hivi Bodaboda Mabosi zao ni Walimu karibu VIJIWE vingi unavyoviona huku katika Jamii wale waendeshaji Wamepewa Mikataba na Waalimu .Na Mara nyingi Mikataba inawashinda Kabisa Mwalimu anachukua boda yake. Hivyo msipende kufananisha kwa shangwe la kipuuzi .Mwalimu akienda bank kukopa Pesa anapewa Pesa ya kununua Pikipiki 6 hadi 10 .Leo hii ukafananishe Bodaboda ambaye hata akiumwa hela haiingii anaweza kufa hata Njaa.
Mwalimu yule anayeanza kazi tu anao uwezo wa kununua Pikipiki 6 na kutoa Ajira Hadi za Bodaboda 6 kwa Mwaka .

Usifananishe Laana na kazi za Utumishi wa Umma .Nenda katembelee Walimu nyumbani kwao halafu katembelee Bodaboda kwao ndiyo utarudi kusema Bodaboda ni Laana.

Kuna Mtu kasema boda anaingiza 35,000/= tukio Kama Hilo ndani ya Mwaka linaweza kutokea kwa Mwaka Mara Moja au mbili tu na hapo umejiumiza hasa bila hata kulala .

Bodaboda baada tu ya Kupeleka hesabu kwa Bosi anabaki na 7000 au 5000 kumbuka anayo familia na anayo Matumizi binafsi kumbuka anatakiwa kununua Mafuta ya hiyo Boda .

Kwakua hakuna Ajira ndiyo maana tunafanya Ila HAKUNA Maisha kwenye Bodaboda.

HAKUNA kijana anayeweza nunua Bodaboda kwa Pesa yake maana Lazima Pesa ya kununua Boda ni kuanzia 2,000,000/= na 2,700,000/= kijana hapa kitaa anaitoa wapi?.

Hakika nawaambieni Karibu Bodaboda zote unazoziona ni Mali za Watumishi wa Umma Kama unabisha waulize wenyewe Bodaboda
 
Waache upuuzi, hao boda boda wananipeleka job daily
Zamani watu walikuwa wanatumia baiskeli kama daladala, in fact Tabora mpaka leo baiskeli bado zinabeba watu, lakini hiyo hawafanyi wasiwe masikini...
 
Ni kweli mkuu Ila umetumia maneno magumu sana😃
 
Hawa boda ambao tunawapa mikataba ndio unaowaongelea?
 
Bi mkubwa wangu ticha somewhere anazo hizo Bodaboda 4 kawapa mikataba ndio mbishe zake na harakati zake zingine za hapa na pale.
 
Nilichogundua kwa madereva bodaboda ni kua, hawafikirii juu ya kupanua biashara yao, ndio wanapata pesa nyingi sana kwa siku, lakini ile akili ya kua watumwa tu wa maboss ndio inawakost. utakuta mtu akimaliza mkataba anauza na kuenda kutafuta nyingine ya mkataba. Yaani hawezi miliki pikipiki yake binafsi
 
Sure.

Wote kipato ni kidogo.
 
Kama unachangamoto ya kibima na unahitaji ushauri na msaada zaidi tafadhali tunaweza kuwasiliana katika number hizi. 0765 827 355 kupata msaada na ushauri.
 
Mkuu wakikujibu nistue niandike barua chap nikanunue boda
 
Acheni kudharau boda boda, unaweza kuta mkeo ndo yanamkula[emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…