Nipande ndege nikasome PhD au Nikomae na biashara yangu?

Nipande ndege nikasome PhD au Nikomae na biashara yangu?

Ukiwa muongo jitahidi kutunza kumbukumbu na jitahidi kuepuka contradictions.

-Kwanza biashara ambayo unapata faida ya 45,000/= kwa siku sawa na 1,350,000/= kwa mwezi haiwezekani baada ya running costs zote ubakie na 200,000/= au 300,000/=??? Ni mjinga pekee anaweza ku squire nawe kwenye hili yaani running costs za biashara iwe around 85% ya profit? Are you serious dude?
-Pili unakumbuka wakati umeandika kuhusu maisha yako ya uyatima tr9/01 ulisemaje kuhusu uzao wako? Nitakukumbusha hapa

IMG_6357.png

-Hapa ulisema una binti (mmoja-emphasis added)
-Mama yake aliolewa ukamwomba akuachie unamlea mwenyewe
-Leo unasema una mabinti 2 wote wanaishi na Mama zao?

Kijana try to be real and yourself! It’s immaturity to stand and tell lies in the midst of men and women.
 
Chukua huu ushauri
Chukua ushauri huu na utanishukuru baadae.
KWANZA jua faida ya kupata elimu ya juu
1: unaweza pata PHD na ukaja ukafanya part time kufundisha vyuo vikuu ambavyo mara nyingi saa moja kufundisha huwa ni laki moja unusu Hadi laki mbili.

2: unaweza acha Kazi au kuomba uhamishwe ufundishe vyuo na mshahara mara dufu.

3: wakati upo masomoni,full salary inaingia hivyo kama kwa mwezi kwenye duka lako ulikuwa unapata laki mbili, Sasa tegemea mshahara wako wote kwa mwezi.

4: huko nje unaweza fanya Kazi maana elimu yetu ni kusoma hasubuhi Hadi jioni wakati wenzetu ni masaa machache tu hivyo kujiongezea kipato hasa dollar.

5: kwa kuwa umesema full sponsorship unayo,huweki chochote kama hela hivyo unaweza kuja kukuta mishahara yako ya miaka yote uliokuwa nje.

6: exposure

7: unaweza pata bahati hata ya kupata Kazi huko huko na usirudi bingo na ukapiga hela ndefu.

8: unaweza pata mtu wa kike na mkaanza maisha ukaachana na maisha ya kutungisha mimba na kuongeza watoto unnecessary, na bila mipangilio na kufanya single mother kuwa wengi.

9: ukirudi dar unaweza kaa muda mfupi na kupandishwa cheo na kukaa headquarter kama dar au Dom na wewe ukawa boss.

10: unaweza fanya biashara kwa kuwekeza hela yako unayofanya Kazi bongo na majuu na pia ukatumia fursa uko nje ya nchi baada ya kumaliza shule ukaleta container la vitu used na ukaja kufungua hapa hapa nchini na ukawa mfanyabiashara mwenye PHD nchini Tanzania na ndo utakuwa msomi wa kiwango cha juu kufanya biashara.

11: HATA ukiamua kufanya biashara na kuacha Kazi, NSSF yako itakuwa imenona hela

Ukiona ushauri wangu mzuri ufanyie Kazi ukiona haufai chagua unachoona kinafaa.
 
Liverpool VPN karibu ndugu .
Sasa kutokana na maelezo yako basi kuna vitu kadha wa kadha nivijue ili nikupe Ushauri Wangu vizuri

Mosi , unaacha utaratibu gani ikiwa una watoto naongelea malezi yao ?

pili ,itakuchukua muda gani Katika hiyo elimu yako ?

Sasa ikiwa majibu yako utayatoa naomba nikushauri kitu ila ambacho kitajihusisha na maswali yangu hapo juu

Ndugu Liverpool VPN najua hamna kitu kinaweza ishinda shauku hata iwe vipi , wewe una shauku kubwa ya kwenda kusoma hivyo ni dhahiri hata ukiacha kwenda kusoma bado nafsi yako haitatulia
Ndugu fanya kile nafsi na moyo wako unakutuma hasa nakushauri nenda kasome maana nafasi ushaipata na yawezekana inaweza kuchukua muda tena kuipata.

Nakuona unaniuliza vipi biashara yangu?
Kaka biashara ni muhimu ila sasa dunia imebadilika kwakuwa leo unasema inakulipa vizuri ila ya kesho huyajui na pia kumpa mtu uaminifu ni zero sasa ufanye nini ?
Hiko hivi najua ukienda huko ughaibuni na ukirejea kwenye mshahara hauwezi kuwa pale ulipokuwa awali hivyo nakupa machaguo mawili katika biashara

Mosi , tafuta mteja mpe hilo duka kwa bei ambayo utaridhia hili urudishe hela yako na ukaitunze utaikuta ukirejea

Pili, ni kweli dunia haina uaminifu ila yawezekana waaminifu wapo japo ni wachache sana sasa ikiwa unaye mtu ambaye unahisi ni mwaminifu kwako na unahisi anaweza kuendelea kuwa mwaminifu hata kama utakuwa huko mbali , ndugu mpe hiyo biashara kwa maandishi na pande mbili za mashahidi na kila kinachobidi katika biashara kifanyike

Fanya hivyo ikiwa siraha kuu ya mfanyabiashara yeyote ni kuwa yakubidi uwe ni RISK TAKER
Hivyo ukirudi ukalikuta duka mshukuru Mungu , ikiwa haujalikuta usihuzunike ni risk imeingia

Lingine ni kuhusu watoto wetu , usijiloge ukaondoka bila kuweka utaratibu mzuri wa kuwahudumia wanao ikiwa ni ada za mashuleni mpaka kuishi kwao .

Nakushauri hayo yote juu kwa kuzingatia ndoto zako za kusoma sasa ni muda wa kuzitimiza iwe hasi au chanya nenda kasome ndugu

Biashara zipo sio hiyo tu ila hata zingine hivyo hata kama biashara yako itasimama bado una nafasi ya kuanzisha nyingine pale ukirejea maana kwenye nia hapakosi njia .

Nimependa kukushauri uende huko uendako maana kama ni full scholarship basi haikugarimu chochote hivyo kapambane
Ila habari za mimi ni mtumishi huko Tanzania ziache huku Tanzania ukifika huko angalia ratiba ya masomo pata muda ujishughulishe na kazi yoyote upate hata vihela kadha wa kadha hivyo vinaweza kuja kuwa ni sehemu ya kulikuza duka lako au kuanzisha biashara mpya ikiwa yako haitakuwepo.

Ndugu nenda kasome , nenda kasome , nenda kasome , biashara huwa muda mwingine ni pata potea yaani leo kipo kesho kinakutaka ujiongeze zaidi ili kiendelee kuwepo ila Elimu ni hazina ujanani mpaka uzeeni ndugu.

NENDA KASOME NENDA KASOME.
Ushauri tu [emoji120][emoji120]

TEKERI.
 
Haloo is me "Mr. Liverpool" again.
Baada ya salamu, hebu tuingie kwenye hoja..

INTRODUCTION
Mimi ni kijana mwenye miaka 32.
Elimu yangu ni Masters ya mambo ya biashara.
Ni mwajiriwa wa Halmashauri moja wapo hapa nchini.

Mimi ni baba wa watoto wawili (kila mmoja na mama ake).
Wanangu huishi na mama zao ila kila likizo lazima waje kwa baba.

Mimi ni kijana ambaye SINA MPANGO WA KUOA japo nahitaji watoto wa5...!!

SCENARIO
Kiukweli kuanzia 2021 moyoni iliingia hali ya kuchoka sanaa kufanya kazi halmashauri.
Huu uchovu ulitengeneza sanaa hasira ya kuhama local government.

Hivyo hali hii ilisababisha nikawa natuma sanaa maombi ya kuhamia Taasisi mbalimbali huku na-apply sanaa scholarship za kwenda kusoma PhD ili mradi tu NIONDOKE HALMASHAURI.

Mwaka jana (2021) Wizara ya Utumishi ilitangaza nafasi ya ku-apply scholarship kwenda kusomea nje huko kwa level za post graduate.

Wakati huo nilikua nina hamu sanaa ya kusoma na kuhama halmashari.

Yaani akili ilikua inawaza ""Niondoke halmashauri au nikasome PhD nipumzike""

Mara nikapata scholarship ya PhD (Full Scholarship).

Hapohapo moja wapo ya maombi yangu ya kuhamia Taasisi moja yakatiki (Taasisi ipo Dar).
Hii Taasisi ilitangaza transfer nikaomba nikapata.

Nikiwa nawaza nihame au nikasome PhD nikashirikisha watu wakubwa wakanishauri ""Niende kwanza chuo/PhD maana hawadhani kama Taasisi inaweza kumruhusu mtumishi waliyompokea miezi kadhaa hata mwaka bado aende kusoma, huku wao walitangaza nafasi za transfer ili wafanye represement""

Hivyo kuhama nikaacha na kutamani sanaaa kusomaaaa.

Hamu ya PhD ikapambaa motooo.
Hivyo nikawa nasubiri tarehe ifike nishughulikie VISA nisepe, kuhama nikatupa kuleee.

PROBLEM
Sababu hasaa ya kutaka kuhama ilikuwa ni kufata mishahara mikubwa, maana niliona kadiri siku zinavyokwenda majukumu yanaongezeka na mshahara wa local government unakua mdogo.

Ila Kuna siku nilikaa nikajishauri nikaona ""nilikuwa nataka kuhama kwasababu ya mshahara mdogo na kuchoka Kazi, hivyo ni bora nifungue biashara ili niwe bizee nisiwe bored na niongeze kipato""

Ila upande mwengine biashara ni jambo nililokuwa napenda na kulitamani kulifanya tokea nikiwa diploma ila ni ukosefu wa mtaji ndio ulinizuia kufanya biashara.

Nikaanzisha biashara ya jumla na rejareja kwenye moja ya mji wa huku mkoani.

Hii biashara imenifanya niwe bizee hasaa na hata siku nyengine kazini siendi (mfano Kuna wiki yoteee sikwenda kazini).

DED aliniita siku moja nikamwambia najiandaa na safari, hivyo alinionyaa basi ikaishia hapo.

Ila tokea anionyee NIMEBADILISHA STAILI, nachofanya naenda kazini nasaini halafu napoteaa kazini kwenda dukani.

Duka langu linaenda vizuri ""ashukuriwe Mungu"".
Duka lilianza kwa faida ya elfu 5 kwa siku (baada ya kutoa matumizi yotee ya siku) na sasa linatoa faida ya 45,000 kwa siku.

Kuna kipindi huwa nafikiria niache tu Kazi niwe free na duka, ila kwenye faida nikipiga hesabu zotee za matumizi ya mwezi dukani (mshahara wa vijana, kodi ya fremu, umeme, usafi n.k) unakuta inabaki faida ya 200,000 mpaka 300,000 naona hii bado haiwezi kunilea ikalipa ada za watoto na kodi ya nyumba na mambo mengine hivyo moyo wa kuacha Kazi unaingia kusita.

Kwa upande mwengine, muda wa kupanda ndege umefika ili nikasome PhD na dip down my heart nahitaji kusoma ila pia hii biashara nahitaji.

Sasa je nifanyaje mwana JF, DED kashasaini barua zotee alizotumiwa na kupelekewa ili Mimi nisepe ila nikiliangalia duka langu naona HAPANA HAPA NDIO NIMEFIKA, nikiwa mwenyewe kitandani huwa NATAMANI SHULE...

Niko DILEMMA ya MAAMUZI.

USHAURI WAKO MUHIMU.

#YNWA
Nenda shule ila nahofia Shem huku nyuma watamshikisha ukuta kama sio michongoma na alivyo mrembo
 
My advice, fanya biashara yako na uisimamie mwenyewe.. hiyo phd haina maana kwako. Haya ukimaliza kusoma urudi kuajiriwa tena sio! Hivi kuna binadamu gani asiependa kujiajiri mwenyewe badala ya kuajiriwa! Labda wachache sana.

Sikulazimishi kamanda,
 
Ukiwa muongo jitahidi kutunza kumbukumbu na jitahidi kuepuka contradictions.

-Kwanza biashara ambayo unapata faida ya 45,000/= kwa siku sawa na 1,350,000/= kwa mwezi haiwezekani baada ya running costs zote ubakie na 200,000/= au 300,000/=??? Ni mjinga pekee anaweza ku squire nawe kwenye hili yaani running costs za biashara iwe around 85% ya profit? Are you serious dude?
-Pili unakumbuka wakati umeandika kuhusu maisha yako ya uyatima tr9/01 ulisemaje kuhusu uzao wako? Nitakukumbusha hapa

View attachment 2302984
-Hapa ulisema una binti (mmoja-emphasis added)
-Mama yake aliolewa ukamwomba akuachie unamlea mwenyewe
-Leo unasema una mabinti 2 wote wanaishi na Mama zao?

Kijana try to be real and yourself! It’s immaturity to stand and tell lies in the midst of men and women.

KUHUSU WATOTO

1. Binti wa pili alizaliwa mwaka jana, kulikuwa na ubishi kati yangu na mama ake kuwa "Mtoto si wangu" ila tulipima DNA ikathibitisha ni wangu hivyo Nilimpokea na namlea.

2. Baada ya kuona sishindi sanaa nyumbani (nazurura kutafuta hela) na mtoto anateseka (binti wa kwanza) niliongea na mama ake tukaelewana amchukue akae kwake.
Na nashukuru mumewe aliridhia ila huwa nahikikisha likizo yake yoyote lazima ni settle ili nipate muda kuwa nae.

3. Na infact mwakani au 2024 nataka mtoto mwengine.
Nahitaji kuwa na watoto wa5 tuuu.!!!

KUHUSU BIASHARA

1. Biashara yangu ni Monopolistic kwenye hili eneo hivyo wateja ni wakugombania.
Faida huwa Kati ya 20,000 mpaka 45,000 per day in different days.
Nakumbuka biashara kama hii faida ni 200, 50, 100 kwa bidhaa, hivyo huwezi pata constant faida siku zoteeee.

Mi ni mgeni hili eneo na ni mgeni wa hii biashara.
Nilichokifanya nimeajiri mpaka mdada (marketing) Kazi yake ni kuzunguka kunitafutia wateja na kunitangaza.

2. Lakini pia Nina vyombo vya Usafiri ambavyo lengo lake ni kufanya bidhaa imfikie mteja shapu pale tu aki order through phone.

Nina vijana 2 wa duka
Mdada mmoja wa marketing
Dereva mmoja wa guta na bodaboda/pikipiki.

Hivyo biashara yangu ina high running cost sanaa.

Ila najua SIKU ZA MBELE ZITARUDI TU.

NB:-
Kwa ushauri usiwe una attack mtu ghafla tuuu.
Uliza kwanza then ndio u comment.

#YNWA
 
nendq kasome huku mshahara unaingia.. achana na hizo biashara za uchuuzi.

Biashara ya uchuuzi ni pata potea haina sustainability. Ni kikubwa kwa sababu hujaoa hilo pia ni jambo zuri.. no stress life.. ki kukubwa uhakikishe unarudi na phd tu maana nayo kuipata is not a walk in the park.. ipo shughuli pevu..

by the way, hii phd ni ya nchi gani? usikute ni ya hiv vyuo msen.ge huko malaysia???
 
Umeathirika kisaikolojia ujue 😃😃, you need help

Kwasababu tu SITAKI KUOA.
Nina shangazi yangu hataki kabisaa kusikia "Kununua gari" ila Kuna watu wanapenda Sana magari.

Unadhani shangazi yangu "NEED HELP"???

#YNWA
 
Kwasababu tu SITAKI KUOA.
Nina shangazi yangu hataki kabisaa kusikia "Kununua gari" ila Kuna watu wanapenda Sana magari.

Unadhani shangazi yangu "NEED HELP"???

#YNWA
Kama uwezo wa nunua gari anao yes anahitaji msaada. Naamini sababu anayoitoa lazima ni ya ajabu.

Kutokua/kutokuolewa sio tatizo. Tatizo ni sababu zinazokufanya usioe seems matukio ya watu wengine yamekuharibu akili
 
Kama uwezo wa nunua gari anao yes anahitaji msaada. Naamini sababu anayoitoa lazima ni ya ajabu.

Kutokua/kutokuolewa sio tatizo. Tatizo ni sababu zinazokufanya usioe seems matukio ya watu wengine yamekuharibu akili

Ndoa zinazeesha sanaaa 👇👇👇

 
Back
Top Bottom