Nipande ndege nikasome PhD au Nikomae na biashara yangu?

Ukiwa muongo jitahidi kutunza kumbukumbu na jitahidi kuepuka contradictions.

-Kwanza biashara ambayo unapata faida ya 45,000/= kwa siku sawa na 1,350,000/= kwa mwezi haiwezekani baada ya running costs zote ubakie na 200,000/= au 300,000/=??? Ni mjinga pekee anaweza ku squire nawe kwenye hili yaani running costs za biashara iwe around 85% ya profit? Are you serious dude?
-Pili unakumbuka wakati umeandika kuhusu maisha yako ya uyatima tr9/01 ulisemaje kuhusu uzao wako? Nitakukumbusha hapa


-Hapa ulisema una binti (mmoja-emphasis added)
-Mama yake aliolewa ukamwomba akuachie unamlea mwenyewe
-Leo unasema una mabinti 2 wote wanaishi na Mama zao?

Kijana try to be real and yourself! It’s immaturity to stand and tell lies in the midst of men and women.
 
Chukua huu ushauri
 
Liverpool VPN karibu ndugu .
Sasa kutokana na maelezo yako basi kuna vitu kadha wa kadha nivijue ili nikupe Ushauri Wangu vizuri

Mosi , unaacha utaratibu gani ikiwa una watoto naongelea malezi yao ?

pili ,itakuchukua muda gani Katika hiyo elimu yako ?

Sasa ikiwa majibu yako utayatoa naomba nikushauri kitu ila ambacho kitajihusisha na maswali yangu hapo juu

Ndugu Liverpool VPN najua hamna kitu kinaweza ishinda shauku hata iwe vipi , wewe una shauku kubwa ya kwenda kusoma hivyo ni dhahiri hata ukiacha kwenda kusoma bado nafsi yako haitatulia
Ndugu fanya kile nafsi na moyo wako unakutuma hasa nakushauri nenda kasome maana nafasi ushaipata na yawezekana inaweza kuchukua muda tena kuipata.

Nakuona unaniuliza vipi biashara yangu?
Kaka biashara ni muhimu ila sasa dunia imebadilika kwakuwa leo unasema inakulipa vizuri ila ya kesho huyajui na pia kumpa mtu uaminifu ni zero sasa ufanye nini ?
Hiko hivi najua ukienda huko ughaibuni na ukirejea kwenye mshahara hauwezi kuwa pale ulipokuwa awali hivyo nakupa machaguo mawili katika biashara

Mosi , tafuta mteja mpe hilo duka kwa bei ambayo utaridhia hili urudishe hela yako na ukaitunze utaikuta ukirejea

Pili, ni kweli dunia haina uaminifu ila yawezekana waaminifu wapo japo ni wachache sana sasa ikiwa unaye mtu ambaye unahisi ni mwaminifu kwako na unahisi anaweza kuendelea kuwa mwaminifu hata kama utakuwa huko mbali , ndugu mpe hiyo biashara kwa maandishi na pande mbili za mashahidi na kila kinachobidi katika biashara kifanyike

Fanya hivyo ikiwa siraha kuu ya mfanyabiashara yeyote ni kuwa yakubidi uwe ni RISK TAKER
Hivyo ukirudi ukalikuta duka mshukuru Mungu , ikiwa haujalikuta usihuzunike ni risk imeingia

Lingine ni kuhusu watoto wetu , usijiloge ukaondoka bila kuweka utaratibu mzuri wa kuwahudumia wanao ikiwa ni ada za mashuleni mpaka kuishi kwao .

Nakushauri hayo yote juu kwa kuzingatia ndoto zako za kusoma sasa ni muda wa kuzitimiza iwe hasi au chanya nenda kasome ndugu

Biashara zipo sio hiyo tu ila hata zingine hivyo hata kama biashara yako itasimama bado una nafasi ya kuanzisha nyingine pale ukirejea maana kwenye nia hapakosi njia .

Nimependa kukushauri uende huko uendako maana kama ni full scholarship basi haikugarimu chochote hivyo kapambane
Ila habari za mimi ni mtumishi huko Tanzania ziache huku Tanzania ukifika huko angalia ratiba ya masomo pata muda ujishughulishe na kazi yoyote upate hata vihela kadha wa kadha hivyo vinaweza kuja kuwa ni sehemu ya kulikuza duka lako au kuanzisha biashara mpya ikiwa yako haitakuwepo.

Ndugu nenda kasome , nenda kasome , nenda kasome , biashara huwa muda mwingine ni pata potea yaani leo kipo kesho kinakutaka ujiongeze zaidi ili kiendelee kuwepo ila Elimu ni hazina ujanani mpaka uzeeni ndugu.

NENDA KASOME NENDA KASOME.
Ushauri tu [emoji120][emoji120]

TEKERI.
 
Nenda shule ila nahofia Shem huku nyuma watamshikisha ukuta kama sio michongoma na alivyo mrembo
 
My advice, fanya biashara yako na uisimamie mwenyewe.. hiyo phd haina maana kwako. Haya ukimaliza kusoma urudi kuajiriwa tena sio! Hivi kuna binadamu gani asiependa kujiajiri mwenyewe badala ya kuajiriwa! Labda wachache sana.

Sikulazimishi kamanda,
 

KUHUSU WATOTO

1. Binti wa pili alizaliwa mwaka jana, kulikuwa na ubishi kati yangu na mama ake kuwa "Mtoto si wangu" ila tulipima DNA ikathibitisha ni wangu hivyo Nilimpokea na namlea.

2. Baada ya kuona sishindi sanaa nyumbani (nazurura kutafuta hela) na mtoto anateseka (binti wa kwanza) niliongea na mama ake tukaelewana amchukue akae kwake.
Na nashukuru mumewe aliridhia ila huwa nahikikisha likizo yake yoyote lazima ni settle ili nipate muda kuwa nae.

3. Na infact mwakani au 2024 nataka mtoto mwengine.
Nahitaji kuwa na watoto wa5 tuuu.!!!

KUHUSU BIASHARA

1. Biashara yangu ni Monopolistic kwenye hili eneo hivyo wateja ni wakugombania.
Faida huwa Kati ya 20,000 mpaka 45,000 per day in different days.
Nakumbuka biashara kama hii faida ni 200, 50, 100 kwa bidhaa, hivyo huwezi pata constant faida siku zoteeee.

Mi ni mgeni hili eneo na ni mgeni wa hii biashara.
Nilichokifanya nimeajiri mpaka mdada (marketing) Kazi yake ni kuzunguka kunitafutia wateja na kunitangaza.

2. Lakini pia Nina vyombo vya Usafiri ambavyo lengo lake ni kufanya bidhaa imfikie mteja shapu pale tu aki order through phone.

Nina vijana 2 wa duka
Mdada mmoja wa marketing
Dereva mmoja wa guta na bodaboda/pikipiki.

Hivyo biashara yangu ina high running cost sanaa.

Ila najua SIKU ZA MBELE ZITARUDI TU.

NB:-
Kwa ushauri usiwe una attack mtu ghafla tuuu.
Uliza kwanza then ndio u comment.

#YNWA
 
nendq kasome huku mshahara unaingia.. achana na hizo biashara za uchuuzi.

Biashara ya uchuuzi ni pata potea haina sustainability. Ni kikubwa kwa sababu hujaoa hilo pia ni jambo zuri.. no stress life.. ki kukubwa uhakikishe unarudi na phd tu maana nayo kuipata is not a walk in the park.. ipo shughuli pevu..

by the way, hii phd ni ya nchi gani? usikute ni ya hiv vyuo msen.ge huko malaysia???
 
Umeathirika kisaikolojia ujue 😃😃, you need help

Kwasababu tu SITAKI KUOA.
Nina shangazi yangu hataki kabisaa kusikia "Kununua gari" ila Kuna watu wanapenda Sana magari.

Unadhani shangazi yangu "NEED HELP"???

#YNWA
 
Kwasababu tu SITAKI KUOA.
Nina shangazi yangu hataki kabisaa kusikia "Kununua gari" ila Kuna watu wanapenda Sana magari.

Unadhani shangazi yangu "NEED HELP"???

#YNWA
Kama uwezo wa nunua gari anao yes anahitaji msaada. Naamini sababu anayoitoa lazima ni ya ajabu.

Kutokua/kutokuolewa sio tatizo. Tatizo ni sababu zinazokufanya usioe seems matukio ya watu wengine yamekuharibu akili
 
Kama uwezo wa nunua gari anao yes anahitaji msaada. Naamini sababu anayoitoa lazima ni ya ajabu.

Kutokua/kutokuolewa sio tatizo. Tatizo ni sababu zinazokufanya usioe seems matukio ya watu wengine yamekuharibu akili

Ndoa zinazeesha sanaaa 👇👇👇

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…