Nipande ndege nikasome PhD au Nikomae na biashara yangu?

Ushauri wa kwenda shule au kuendelea na biashara, kuna wakati ili upewe ushauri mzuri wa nini cha kufanya ni vema pia kujua wewe una character gani.

Kuna watu huwa hawawezi kabisa hizi shughuli za ujasiriamali , watu wengi wa aina hii hupenda sana kuwa academician, na huona kusoma ndio njia mbadala ya kuongeza kipato.

Lakini pia kuna wale kutokana na exposure yao hata kwa elimu ndogo sana lakini hujikita kwenye ujasiriamali na hufanikiwa sana. Maana ujasiriamali pia unahitaji maarifa mengi japo unaweza pata through informal ways na bado ikakusaidia sana na kukupa mafanikio makubwa katika kipato.

Nb: jitafute katika hivyo vitu viwili , character yako, lipi unaliweza sana maana mwisho wa siku kipato kiongezeke. Hivyo nashindwa kutoa ushauri wa moja kwa moja kwasababu sijui character yako kwenye hivi vitu viwili, ila kwa maelezo yangu ya juu yanaweza kukusaidia kuchagua kipi cha kufanya.
 
3 - 5 Yrs.
Ila kama utaenda straight ni 3 Yrs tu unamaliza.

#YNWA
Mkuu nakushauri nenda kasome sababu zifuatazo

1: Utaongeza maarifa zaidi


2: Utafanya vitu viwili kwa wakati mmoja( unasoma na unafanya kazi (part time Jobs) na unapata pesa nyingi kwa nchi za wenzetu


3: Exposures (hii itakusaidia sana hata ukirudi home utafanya biashara zako kwa ufasaha zaidi na huenda ukafanikiwa zaidi kuliko utakavyotarajia.

Nakupa mfano ..MM nipo Kenya wenzetu wapo mbali sana kiupeo na kimtazamo tofauti na sisi watanzania wengi. Jamaa zangu wengi wanaenda ng'ambo tena wengine wanatumia fedha nyingi kwa kudanganya wanaenda kimasomo ili kupata VISA,wakifika huko wanapambana na part time Jobs baada ya miaka kadhaa mtu anarudi Nairobi anasimamisha ghorofa zake anakula maisha na familia yake. Wakenya wengi waliopo Australia wanafanya risk assessment hata ya kuoa mzungu ili apate papers akae kwa muda kidogo huko na wakati huohuo anapeleka familia yake kama "Students" anaendelea kukaa nayo huko kiujanja.


4: Yamkini ukarudi na ukapandishwa cheo zaidi.
 
Mkuu kama una Masters na hujui kuandika kiingereza utaaibika bora uendelee kuuza duka...eti wakufanyie represement""?
 
Ishu ya kuhamia Dar wakati huo ilipokuja kwangu ndo ingekua priority namba moja.Kwasasa kama hesabu za faida dukani ni hizo ulizoandika hapo bado hiyo biashara haijafikia hatua ya kuitegemea kama ukiacha kazi leo so nenda tu kasome ukirudi utaanza upya maana kwa aina ya biashara zetu wabongo usipokuwepo na lako halipo.
 
Kaka kama
Naomba
 
Nikiwa kama mtaaalam wa maswala wa human resources management ngoja nikushauri kitu.
elimu bongo ya kimuundo mwisho Masters ambapo ndio itakayokufanya ufike pahala kwenye cheo cha kimuundo,
Hakuna siku itahitajika PhD ili upande daraja,,pia kwa umri wako PhD haitakusaidia maana bado junior katika utumishi haitakuwa na maana kwa wakati huu zaidi ya kuongeza tu mzigo na kujiwekea ugumu wa maisha kwakuwa hakuna junior PhD unataka kuzidi elimu mabosi zako utapigwa pini nyingi sana za kiutumishi.
Tatizo la utoro kazini boss wako azalea upuuzi ila hiyo tabia ukihama nayo kwenye taasisi nje na local huko ulipo unafukuzwa kazi mapema sana
Kujiongezea kipato nje na kazi ni jambo bora kikubwa isiathiri ratiba za mwajiri wako. So kama taasisi unayotaka kuhamia ipo vizuri fanya hivyo mapema itakupa Fursa ya kujipanga
 
Hiyo PhD Sponsor ni wewe mwenyewe?,ungekuwa chuo kikuu hiyo PhD ndio ingekuwa na maana.Ungetumia huo muda wako kujjtafuta zaidi kuliko kwenye PhD.Kama ujuavyo PhD inaweza kuextend muda zaidi ya hiyo miaka 3 ambayo bila shaka wewe ndio unaipigia hesabu kuwa utasoma PhD.Achana
 
Mrejesho kipi uliona kinafaa
Mrejesho kipi uliona kinafaa
Niliona PhD mizinguo nikakomaa na biashara.
kwasasa biashara ina crate 800 za bia, 200 za coca na 235 za Pepsi.

Biashara hii imenifanya kufungua biashara nyengine 2.

na mwezi wa 2 nilifungua kampuni.
kwasasa naiendesha kwa staili ya limited company.

The future is promising japo MAPAMBANO BADO YANAENDELEA.

#YNWA
 
Mkuu kama una Masters na hujui kuandika kiingereza utaaibika bora uendelee kuuza duka...eti wakufanyie represement""?
Ushauri..
upokuwa unachangia hoja hebu epuka zile Pessimism words and Comments.

ukifanya hivyo UTAFANIKIWA SANAA.
Unajua hakuna faida ya ku-act elimu ya mtu, kipato cha mtu au chochote cha mtu ambae humjui?

#YNWA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…