Nipeni Mbinu za kushinda vita za makazini, naona vita imekua kubwa

Nipeni Mbinu za kushinda vita za makazini, naona vita imekua kubwa

Technophilic Pool

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2024
Posts
3,104
Reaction score
4,574
Makazini kuna vita nyie?

Kila nako enda kufanya kazi vita inanizidia nipo sehemu ya tatu sasa kote vita hizi zimenishinda maadui zangu wananishinda.

Nadhani ni kwasababu ya personality yangu.

Mi si mtu wa kujipendekeza
Sina shobo

Nafanya kazi yangu naenda nyumbani.

Lakini game inaonekana ina mbinu nyingi na chafu zaidi.

Wakongwe mnipe mbinu.

NB: kama huna kazi au hujawai ajiriwa uwe msikilizaji
 
Acha mazoea na watu wa kazini utaishi kwa amani ,ishi kama bubu ..Ikipendeza achana na kukaa karibu kama kuangalia status zako na wao wasione zao ..Usiende kwenye mchanganyiko wa hafla nje ya kazi ; usiende kwenye harusi ya mfanyakazi mwezio au sherehe yake binafsi .

Ishi wasikujue ulivyo ,usipende kusambaza taarifa zako..Kama ni mwanaume usizoeane na mwanamke kwa namna yoyote ile wala kutongoza ...Walie buruzi hata kukuongelesha wanaone aibu.
 
Mimi ujuzi wangu ni kama MAJI usipo yaoga utayanywa usipo yanywa utajitawazia usipo jitawazia utafulia nguo usipo fulia nguo utayanawia mikono usipo yanywa yatakunyeshea na kuzalisha chakula utakila.

NB. Mimi sehemu zoteee nilizo pita huwa natokea KUAMINIKA/KUAMINIWA KATIKA UMRI MDOGO.. JIFUNZE KUISHI NA WATU, WAHESHIMU, USIPIGE MAJUNGU,USIJIPENDEKEZE, KUA MKWELI NA REAL, FANYA KAZI KWA BIDII ACHA KAZI NDIO IKUTANGAZE, WEKA FENCE WAKUOGOPE NA USIFANYE WAKUZOEE ZOEE OVYO OVYO.

MIMI KATIKA UMRI MDOGO NILIWEZA KUAMINIWA KUONGOZA WATU WENYE LIKA KAMA BABA KWANGU NA WENGINE WAKUBWA MIMI HUWA SICHONGEI MTU, NINA UMAGUFURI FULANI NDANI YANGU, PIA NINA MIPAKA YA MAZOEA, SICHEKI OVYO OVYO, HUWA NAPENDA ZAIDI KUCHUKIWA KWENYE KAZI.
 
Nilikaa siku mbili bila kulala vizuri usiku baada ya mkataba wangu kuisha na boss kukataa ku-recommend tu niongezewe
Lakini sasa naamini pengine pale sikuandikiwa...nilipewa ushauri wa kwenda Bagamoyo kwa mtaalam lkn nilikataa, wengine wakasema niende kwake boss nikamuombe, pia niligoma..sababu kazi nying nilifanya mimi na boss alkuwa kilaza tu
Mungu kanipa serikalini na malipo mazuri kweli
 
Nilikaa siku mbili bila kulala vizuri usiku baada ya mkataba wangu kuisha na boss kukataa ku-recommend tu niongezewe
Lakini sasa naamini pengine pale sikuandikiwa...nilipewa ushauri wa kwenda Bagamoyo kwa mtaalam lkn nilikataa, wengine wakasema niende kwake boss nikamuombe, pia niligoma..sababu kazi nying nilifanya mimi na boss alkuwa kilaza tu
Mungu kanipa serikalini na malipo mazuri kweli
Una MOYO NA ROHO YA KISOVIET (RUSSIAN)
 
Hapana sina kosa ila mara nyingi ni watu wanatengeneza maneno na skendo, watu wanaojipendekeza kwa maboss ndo wanatupaka matope
kama niivyo kuwa bize na mambo yako na usionyeshe kwamba unaathirika na vita vyao,wakigundua unaumia ndo watazidisha, wakiona unanawili na kupendeza wataachana na wewe? vita haviepukiki makazini mkuu chamsingi hakikisha vita hivyo havikuhalibii kazi yako kingine jalibu kujishusha uone hali itakuwaje ,kama vile kuwasalimu n.k...watu wapuuzi sana wanaweza kumchukia mtu bila sababu yoyote chamsingi ishi kwa akili nyingi
 
Back
Top Bottom