Nipeni Mbinu za kushinda vita za makazini, naona vita imekua kubwa

Nipeni Mbinu za kushinda vita za makazini, naona vita imekua kubwa

Onaonekana ni kijana mdogo ambaye hujawa matured kisawasawa, kama sikosei uko kwenye 20’s mwishoni au kati au 30’s mwanzoni… huwezi kunielewa na madhara yake huyajui

Hata kuoa mtu mliye level sawa kazini ni makosa. Endelea yatakapokukuta utaelewa kijana wangu
Sipingi mawazo yako. Na nayaheshimu pia. Mimi namtom.ba yeyote tu hata wewe ukijichanganya napita na wewe tu
 
Pole sana mkuu na hakika vita ni karibia sehemu nyingi makazini ila jipe moyo. Binafsi nilipohitimu chuo nkapata kibarua mahali fulani kitengo kizuri tu na kuna mtu alinipisha yeye akapangiwa sehemu nyingine lakini ni ya chini,,,,aiseee vita ile ilichachamaa jamaa akawashawishi wafanyakazi wengi wakawa hawaniungi mkono.

Wakawa wanafanya hila kila positive changes nilizozianzisha kwa manufaa ya ofisi zikawa zinapingwa aisee. Mambo yalipozidi nilikaa chini na mkurugenzi nikamweleza nae akanitia moyo kuwa nifanye kazi, niliyashinda yote na baadae maadui zangu waligeuka marafiki lakini tayari me nilisha chukua tahadhari juu yao.
 
Acha mazoea na watu wa kazini utaishi kwa amani ,ishi kama bubu ..Ikipendeza achana na kukaa karibu kama kuangalia status zako na wao wasione zao ..Usiende kwenye mchanganyiko wa hafla nje ya kazi ; usiende kwenye harusi ya mfanyakazi mwezio au sherehe yake binafsi .

Ishi wasikujue ulivyo ,usipende kusambaza taarifa zako..Kama ni mwanaume usizoeane na mwanamke kwa namna yoyote ile wala kutongoza ...Walie buruzi hata kukuongelesha wanaone aibu.
Well said. Hizo ndio kanuni kuu kazini.
 
Scenario km ninayopitia mm
Mtu anakuchukia hujamkosea chochote kibaya n mwanamke msimbe sina tyme naye always yeye ananipaka matope na kuniongelea vibaya vibaya mbele za watu.
Wanawake usiwaamini sana mkuu, uskute mwenzio anakuelewa na anaona wewe huna time nae so kamaind.

Au anaona hiyo ndio njia pekee ya kupata attention yako.
 
Vita hiyo ni

1.Wafanyakazi vs You au
2.Wafanyakazi + Boss vs You

Kama ni Vita no 2. Hutoboi Ondoka/Hama kituo cha kazi hapo utakuja Ufe au ujisababishie mabalaa tu.

Huwezi shindana na Kundi Lote hilo.

Kama ni VITA NO.2

Fanya Mashauri wanakushauri watu hapa kwenye huu uzi yale utakayoona yanakufaa yachukue yote yafanyie kazi.

Ila hapo kwenye NO.1 No maongezi ukilazimisha sana kitakukuta zaidi ya hizo figisu mwisho usingiziwe kubwa zaidi ujikute JELA au HOSPITAL au MOCHWARI kbisa.
💯
 
umeajiriwa au umejiajiri, usiombe ukutane nao.
Siwezi babaishwa na work mates hata siku 1, sio hivyo yaan ktk maisha yangu, mie binafsi siendeshwi na mtu, natimiza majukumu yanipasayo, mengineyo hayanihusu kabisaa. Lol
 
Siwezi babaishwa na work mates hata siku 1, sio hivyo yaan ktk maisha yangu, mie binafsi siendeshwi na mtu, natimiza majukumu yanipasayo, mengineyo hayanihusu kabisaa. Lol
hujakutana na waja kwa maana ya waja, hutajua hujui nakuapia,

usishawai pelekwa kwa balozi kisa jogoo wako amemkimbiza mtetea wa jirani wewe? (yaani anataka mechi)
 
Pole sana mkuu na hakika vita ni karibia sehemu nyingi makazini ila jipe moyo. Binafsi nilipohitimu chuo nkapata kibarua mahali fulani kitengo kizuri tu na kuna mtu alinipisha yeye akapangiwa sehemu nyingine lakini ni ya chini,,,,aiseee vita ile ilichachamaa jamaa akawashawishi wafanyakazi wengi wakawa hawaniungi mkono.

Wakawa wanafanya hila kila positive changes nilizozianzisha kwa manufaa ya ofisi zikawa zinapingwa aisee. Mambo yalipozidi nilikaa chini na mkurugenzi nikamweleza nae akanitia moyo kuwa nifanye kazi, niliyashinda yote na baadae maadui zangu waligeuka marafiki lakini tayari me nilisha chukua tahadhari juu yao.
Ulichukua tahadhari gan
 
Back
Top Bottom