Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 15,819
- 33,255
Nitafanya mambo matano muhimu.
1. Kuufanya Arusha kuwa Mji wa Taasisi za Kimataifa Afrika ambapo Taasisi zote za kimataifa zitapewa maeneo ya kujenga Ofisi zao na Makazi ya Wafanyakazi wao Arusha- Kupitia hili nina uhakika wa kuingiza fedha nyingi sana za kigeni pamoja na kutengeneza ajira za uhakika kwa Watanzania wengi sana.
2. Kuifanya Dar es Salaam kuwa Mji wa Biashara kweli na Dodoma Ofisi na Makazi ya Serikali tu. Kwenye hili kila kitu cha Kibiashara na maeneo makubwa mazuri ya starehe yatajengwa Dar.
Dodoma kutakuwa na Ofisi za Wizara, Ikulu, Bunge na Mahakama tu. Hakuna taasisi itakuwa na Ofisi Dodoma bali Ofisi za Taasisi zitagawanywa mikoa mbalimbali ikiwemo Dar, Mwanza, Mbeya, Kigoma, Lindi, Iringa, Kilimanjaro, Tanga na Njombe ili kuleta uwiano katika vichocheo vya maendeleo sehemu mbalimbali.
3. Kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha usafirishaji kuelekea kusini, katikati na kaskazini mwa Afrika kupitia Bandari zake na reli. Hapa nitaweka miondombinu ya uhakika ya reli za umeme na barabara za uhakika kwenye njia zote za mipaka ya kuingia na kutoka Tanzania.
4. Kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha Utalii na Uwekezaji Afrika. Kila kivutio cha utalii kinachopaswa kuwepo Tanzania kitawekwa.
Mwisho nitaivunja Wizara ya Ardhi na kuajiri vijana wapya ambao watafanya zoezi na kuipima na kuipanga nchi nzima.
Kabla ya yote haya nitaanza na Katiba Mpya.
Mungu nisaidie!