Nipeni ushauri kuhusu huyu mwanamke maana sielewi

Candela

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2021
Posts
817
Reaction score
2,180
Nanukuu kama ilivyosimuliwa na muhusika, " Niliingia katika mahusiano na binti mmoja alikuwa akiishi na wazazi wake. Tulikuwa vizuri mpaka ikafikia nikawa namhudumia kama mke vile, kuanzia kula yake, kuvaa na hata akiumwa nahusika na kila kitu. Ikafikia wakati akahama kwao, akaenda kupanga na hapo ndio shida ilipoanzia. Nilimsaidia vitu baadhi vya kuanzia maisha na kodi nikamuongezea robo. Alipohamia kwake tukaenda vizuri tu mpaka siku nilipotaka kujua anapoishi nikaona anaanza kunikwepa.

Badae nikamkazania nataka nipajue , akanielekeza nikaenda nilipofika akaanza kusema nishapajua hategemei kunioma tena pale, kwani yeye ashasema akipanga hataki mwanaume aingie katika chumba chake. Kengere ililia kichwani mwangu lakini sikutaka kubishana nae nikaondoka.

Baada ya hapo kama nilivyosema, nilikuwa namuhudumia na kila wiki nilikuwa nampa nauli na hela ya kutumia akiwa kazini, so nilipotoka hapo kesho yake sikumpa pesa kama ilivyo ada, akanipigia kuomba nikamwambia sina. Wiki ikapita analalamika hana hela hata ya nauli mie sikujali.

Week iliyofuata akadai gesi imekata, nikamwambia sawa badae akaona kimya, akanicheki akauliza nilikwambia gesi hamna, mpaka sasa hujatuma hela unataka niishije, nikamjibu sina pesa, basi akaanza lawama kuwa nimebadilika simjali na vitu kibao. Nikampigia nikamweleza kama yeye hataki niende kwake mie namuhudumia ili iweje sasa. Nikafilia mbali nikamwambia tena ukiona kama sieleweki achana na mie tafuta mwanaume anaeeleweka."

Kilichonileta hapa ni kuwa, licha ya kuwa nimeamua ku move on sina tena time na huyu mwanamke, lakini bado anaendelea kunitafuta na kuwasiliana na mie kama wapenzi ambao hawana tofauti, yaani ana act kama hamna kilichotokea na ananieleza shida zake akitaka nimsaidie, lakini binafsi moyo huo sina, yaani somo la huruma nilimpiga mwalimu sikuingia hata kipindi kimoja.

Nimemwambia tuachane lakini bado anadumisha mawasiliano na mie na hana dalili kukubaliana na matokeo ya alichosema." Sada sielewi nifanyeje ili aache kunitafuta, maana maisha yake magumu kuna mda naumia anavyoniambia shida zake, lakini ndio hivyo siwezi kutoa hata senti yangu kwa mwanamke dizaini yake kwa hapo tulipofikia.

Mrejesho:

 
Najitakia usiku mwema...[emoji3590]
Na kwangu pia ..[emoji3590]

I love me [emoji3590]
Ilove me too[emoji3590]

Me nalala..
Mbona nalala mapema..?
Ndio ..nalala mapema maana simu haina chaji na umeme hamna.

Ok sawa kesho hiyo..
Ok pw pw.
 
Nilitaka nimdharau mshikaji waio ila kwa huu uamzi kama atausimamia atakuwa ni mwanaume wa shoka na kamwe hatosumbuliiwa na malaya tena
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…