Nipo Chato natafakari mengi, kwa hili pekee Katoliki na Usalama wangelisaidia Taifa kama wangeamua

Kwani lazima wamshangilie?

Kama wananchi wanashangilia ujinga kila siku, kwa nini unaona kushangilia kuna maana sana?
 
Kwani lazima wamshangilie?

Kama wananchi wanashangilia ujinga kila siku, kwa nini unaona kushangilia kuna maana sana?
Mzalendo wa kweli atalikisha information kwa local media hasa social media kama JF na kwingineko; ukiona mwandishi anapeleka siri au hicho unacho kisema wewe kama ubadhirifu nje ya nchi yake, huyo hana Nia nzuri na nchi yake, huyo ni mfanyabiashara, anaweza kuuza nchi yake, huyo ni kibaraka, hafai kabisa kua moja ya mwananchi mwenzio; tetea unavyo weza lakini popote duniani HAKUNAGA jambo la namna hiyo halafu na wenye akili wakaunga mkono, hakuna.
Mwanzoni nilidhani Magufuli alikua anaonea watu, baada ya kusoma the other side ya huyu mwandishi ambaye kupitia yeye umenituhumu kwamba nilikataa shule, nimejiridhisha, intelligence ya Magufuli was for this country na sio kwa maslahi yake binafsi. Kama kutokupenda makaratasi ya Kabendera ni kuchukia shule, let me stay ignorance kuliko kua msomi muuza nchi, shule inakua haina maana to me, period
 
Unalazimisha hoja kijinga.

Hoja ya muhimu ni ukweli na uwazi.

Hilo suala la mtu kupeleka habari vyombo vya nje ndiyo linaweza kuwa la mzalendo zaidi, kwa sababu vyombo vya ndani vyote viko compromised.

Kabendera kaongelea haya yote alivyofanya kazi vyombo vya habari vya Mengi Tanzania alivyoona madudu.

Tatizo hutaki kusoma, umejijengea dhana za kijinga kichwani mwako na hutaki hata kusoma ujielimishe.
 
Siwalaumu! Inawezekana wanaangalia route zitakazowalipa badala ya kujaribu kumridhisha kila mtu.
 
Huyo huyo aliyewaambia waandishi " hampo huru kuandika andika tu " au sio!? Unafikiri waandishi wa ndani wangeweza kuandika!? Wangeandikia wapi!? Magazeti yao yafungwe au kufutwa!?

JPM alikuwa Rais bora sana ila pia alikuwa na UPUMBAVU uliopitiliza upumbavu wa marais wengine wote waliomtangulia.
 
Chattle ni mfano mzuri sana wa yule mtu mpumbavu Biblia ilisema, aliyevuna mazao na kupata utajiri akasema sasa ngoja nikae nile nifurahishe nafsi yangu, Mungu akamwambia mpumbavu mkubwa wewe, leo hii nakuja kutwaa roho yako. wanadamu wengi huwa wanapata kiburi sana hasa wakipata kitu, wanajiona miungu watu, wanauwa watu,w anaonea na kunyanyasa nafsi za watu kwa sababu wana kitu. hawajui kuwa kuna mbabe mmoja tu ambaye akiamua kukunyoosha anakunyoosha tu. uwe Rais, uwe masikini uwe nani.

hii ilikuwa kwa mobutu seseseko pia, kwao alijenga uwanja wa ndege na ikulu ndogi, yakageuka kuwa magofu. kipindi cha jiwe, alijenga uwanja ule kwa bil.40 za watanzania, umebaki uwanja wa popo wa wachawi wa kisukuma, sijui kama kuna ndege yeyote inaenda kule. mabenki mengi yalikimbilia kule, yameondoka, watu walijenga mahoteli na lodge, sasaivi lodge zao wanalala panya na wachawi tu usiku na mapopo. ni kama mji uliolaaniwa vile. hakuna mtu anapenda kwenda kuishi chattle sasaivi.

nawashauri ninyi mnaoteka na kunyanyasa nafsi za watu, jueni hamtaishi milele. Mungu akutane na ninyi mmoja mmoja, jueni kama hamtabadili njia zenu, kuna siku tu mtavuna mnachopanda, hakika mtavuna.
 
HAta membe alijenga kanisa kwao likakataliwa na katoliki
 
Hapo USA, Edward Snowden wananchi wanamtazama kama mzalendo?
 
Hapo USA, Edward Snowden wananchi wanamtazama kama mzalendo?
Wengi sana.

Mfano mmoja muhimu.

Mtu aliyeteuliwa na Trump kuwa Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa (Director of National Intelligence) Tulsi Gabbard amesema anakataa kumuita Snowden msaliti na anafurahia Snowden alivyoanika madudu mengi ya uvunjwaji wa katiba katika program za serikali ya Marekani.

Huyu si Mmarekani wa kawaida tu, huyu ni Mmarekani anayeenda bungeni kuwa confirmed kama Director of National Intelligence.

Ameyasema hayo huku anajua anaenda bungeni kuulizwa maswali magumu kuhusu confirmation yake kuwa Director of National Intelligence.

Sasa kama huyu kasema hivi, jiulize Wamarekani wa kawaida wangapi wanamkubali Snowden kama mzalendo.


 
Wewe sifi leo wewe!!wewe ndio wale watafiti uchwara!

Kujenga kanisa na kukabidhi taasisi kwanini aonekane kichaa wakati ni kitu Cha kawaida!!?

SEMA wakatoliki wanajenga makanisa Yao kimkakati zaidi Kwa malengo makubwa huku chini ya maeneo hayo Kuna utajiri ndani yake!!

Mwamba hakukusoea,Mama janet unafukuzaje walokole hapo!!?Marehem atakua anawalaumu sana !watu wa Mungu Huwa hawafikuzwi kwenye kanisa!wamekaribisha vita kuu ya kiroho pasipo kujua!!

Jpm alikua ni mwamba na hizo dosari ni dosari za malezi na makuzi ndio zilimchnaganya!kina jpm wapo wengi sana na wanapitia magumu sana Sasa Hadi wapate ukubwa ndio tutawajua kwamba tulikosea kuwalea!!
 
😃 ndo akaamua kuliita kabisa Mtakatifu Joseph.
Alikua anaijua hatma yake mapema!kwasasa huwezi kuwa namba moja wa nchi bila kujua fate yako,lazima utachungulia kwanza Toka kwa jamii zile ndio wakupe kijiti!!

We huoni alipewa ubunge wa vipindi vinne kipindi Cha tano ndio akawa was muhula mmoja!!?unafikiri alipata pata tu!!?

Mchoro unapewa mapema ndio unasaini halafu unaanza kutumikia Duniani Kwa muda Fulani wanakuchukua ukamalizie na upande wa pili ndio unaenda rasmi sasa ukisubiri hukumu kuu!!

Labda utaelewa!
 
Kwanini nisiseme umetumia hisia kufikia hitimisho hili?

Umetoa mfano wa mtu mmoja hapo.
Nimetoa mfano si wa mtu mmoja tu.

Huyo mtu ni mteuliwa wa rais anayeenda kuwa confirmed bungeni.

Maana yake ni kwamba anawakilisha mawazo yaliyokubalika na rais Trump na watu wengi sana waliomchagua. Anaenda kuwakilisha ajenda ya watu wengi sana wa Marekani. Ingekuwa si hivyo asingeteuliwa.

Hii poll inaonesha %56 ya millennials wa US wanamuona Snowden ni mzalendo.


Hapa YouGov survey inaonesha %55 ya Wamarekani wanaona Snowden yuko sawa. Kuna polls nyingi zinazoonesha kuwa kuna sehemu kubwa tu ya Wamarekani wanam support Snowden.



Haya, hizi polls zote nazo ni mtu mmoja huyu?
 
Ok tufanye uko sahihi...

Kwanini Snowden aongee ukweli halafu akimbie wakati USA ni nchi ya kidemokrasia?
 
Ok tufanye uko sahihi...

Kwanini Snowden aongee ukweli halafu akimbie wakati USA ni nchi ya kidemokrasia?
Demokrasia ni jambo relative na dynamic. This is not something that is fixed and written in stone. There is no perfect democracy on earth. Watu wanaoujua uhuru wao wanazikataa sheria dhalimu, hata kama si kwa kasi wanayotaka wao.

Ndiyo maana kuna mabunge ya kubadili sheria zilizopitwa na wakati. Ndiyo maana kuna whistleblower protection laws.

Inawezekana Snowden ni mzalendo zaidi ya sheria za sasa za Marekani zinavyoruhusu.

Umekubali hoja ya msingi kwamba mtu mzalendo anaweza kuianika nchi yake kwenye vyombo vya kimataifa na kwamba mfano wako wa Snowden umetuonesha hilo na Wamarekani wengi sana wameelewa hilo jambo na wanamuona Snowden kama mzalendo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…