Mtaji wa 400k unatosha kabisa. Ila kabla ya yote unatakiwa uumize akili vya kutosha hata mwili pia. Biashara ya huo mtaji inabidi kujitoa mhanga na muda wote uwepo kimwili na kiakili. Ni mtaji ambao hauhitaji kabisa ule uswahili wa kusema "mwanzo mgumu", "binadamu sio wakamilifu tunafanya makosa", nk. Huo mtaji unahitaji discpline ya hatari maana kosa kidogo tu mtaji umefia mbali. Ungekuwa una subira na una mchina huko China ungeagiza 100pcs za viatu vya Tsh 2000 ambazo unaweza kuuza TZ kwa Tsh 10,000 hadi 15,000/=. Ni subira ya mwezi hadi mwezi na nusu.