Nipo Kariakoo muda huu: Kariakoo kumetakata, kusafi sana. Wahusika wapongezwe

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
40,153
Reaction score
93,069
Hamjambo!

Jua ni Kali sana hapa! Kupigana vikumbo ni hali iliyozoeleka maeneo haya. Kelele za watu na magari kama kawaida. Hakuna anayeshtushwa na hayo. Imezoeleka hivyo.

Lakini kuna jambo moja sio la kawaida macho yangu yanaliona. Na naamini sio mimi pekee bali wengi wanaona hali hii.

Maeneo mengi ni masafi kwa kiwango cha kuridhisha. Kama tukiweka kwenye asilimia basi tunasema ni 75% maeneo ni masafi.

Macho yangu yanaona kila Duka, kila meza ina dustbin la kuwekea takataka. Jambo ambalo halikuzoelekea kwa wafanyabiashara wengi eneo hili.

Njia ni nyeupe, kukuta mfuko au uchafu unazagaa ni nadra sana kitu ambacho wiki kadhaa zilizopita miguu ya watu ilikuw ikiogelea kwenye uchafu.

Nawapongeza wahusika wote waliofanya jitihada hizi. Mambo ni mazuri huo ndio ukweli.
Serikali na wadau kazi hizi ndio zinadhihirisha kuwa serikali ipo na inaviongozi wanaojitambua.

Sio watu wanatembelea juu ya mavi, mitaa inanuka, takataka kila sehemu alafu unajiita kiongozi, sijui Rais, sijui Mkuu wa Mkoa, sijui Waziri. Nope!
Haya ndio mambo yanayowatambulisha kama viongozi wa maana kabisa.

Kingine naona barabara ni nyeupe, machinga hawapangi tena bidhaa zao katikati ya njia. Hili ni zuri sana.
Leo nimepita bila bughuza za kukanyaga bidhaa za watu au kusukumwa kwenye bidhaa za watu.

Taarifa niliyonayo hapa ni kuwa Machinga kesho watakuwa kwenye kikao saa tatu. Na tarehe 24 mwezi huu hakutakuwa na machinga eneo hili la Kariakoo.

Mambo muhimu ambayo nayapendekeza;

1. Serikali iangalie ni namna gani inaweza kusaidia hao vijana watakaondolewa hapa.

2. Mawinga wote uundwe utaratibu wa kuwasajili.
Kila Duka liwe na winga Rasmi ambao watavaa sare za duka husika. Na wawe kwenye umoja au kikundi cha mawinga Kariakoo.

3. Ipigwe kampeni na propaganda Mteja atakayekutwa na bidhaa isiyo na risiti Rasmi atatozwa faini elfu 50 au kuwekwa mahabusu kwa wiki nzima.
Ukibana wateja umembana mfanyabiashara.

4. Serikali iandae portal mtandaoni ya Lists za bidhaa na bei zake(range ya bei) ili kuwarahisishia wananchi kutokupigwa na wafanyabiashara au mawinga.
Mfano;
Simu ya infinix hot 40. Bei 200k - 350k kulingana na eneo mtu analochukulia.

Kwa nini?
Wafanyabiashara wanatumia mwanya wa kutotoa risiti kutokana na watu kutokujua bei halisi ya bidhaa. Hivyo mtu anajua ameonewa huruma kununua bidhaa fulani. Hata risiti hana ujasiri wa kuomba.

Mfano. Jiko la pressure cooker mteja ataambiwa 200k.
Mteja ataomba wataenda mpaka 130k. Watakubaliana kuuziana.
Mteja akidai risiti. Mfanyabiashara atamuambia kama unataka risiti leta 200k.
Automatically mteja atachukua kwa bei pungufu na risiti hataihitaji.

Bei elekezi ni muhimu. Kama kwenye vyombo vya usafiri tuu.
Unajua kutoka Dsm mpaka Arusha nauli ina range 50k - 100k
Hivyo mtu anajipimia anavyotaka bila kuonewa huruma, kuomba omba, na ticketing lazima wampe ticketi halisi.

Nikweli bidhaa zipo nyingi. Lakini wapo watu wakufanya hiyo kazi. Waziingize zote kwenye portal moja.
Mtu akienda sokoni anajua fika anachoenda kununua ni bei fulani.

5. Hili la Winga wa kila duka kuvaa sare zao ni muhimu sana.
Ili kuwadhibiti kisaikolojia.
Mfano kuna mawinga ambao wanatabia ya kushika shika mikono au matako ya wateja wanawake.
Mtu aliyevaa sare ya duka fulani ni ngumu sana kufanya hivyo kwani ataona anaharibu kazi, Jina la biashara husika.

6. Pia, Winga kuvaa Sare ya duka fulani inamtambulisha kwamba huyu ni winga kutoka ofisi fulani.
Inaepusha utapeli ambao ungeweza kudhibitiwa.

7. Biashara ya mtandaoni.
Serikali ni muhimu kurahisisha na kuandaa mfumo ambao wafanyabiashara wa mtandaoni watajisajili hukohuko mtandaoni. Watalipia kodi mtandaoni. Kila kitu kitamalizwa mtandaoni.

8. Isiwe lazima mtu kuja kupanga mafoleni huko kwenye maofisi yenu. Kwanza baadhi ya maofisa ni wavivu. Kitu cha Lisaa limoja unafuatilia miezi mitatu. Sasa ndio nini.

Dunia imebadilika. Vijana wa Tehama wapo. Waandae mfumo mzuri na wenye ulinzi. Vijana wapate pesa na serikali ipate pesa.

Sasa serikali inasema oooh! Ukifanya Biashara mtandaoni weka Cheti cha Biashara, sijui TIN namba sijui leseni ya Biashara.
Mtu ambaye hana hata mtaji ataweka?

Ongeeni na META au hao wenye mitandao ya kijamii wawawekee mifumo ya wanaofanya online business kama sisi wenyewe kama nchi hatuwezi.

Acha nipumzike sasa.

TaikonMaster
Kwa sasa Kariakoo, Dar es Salaam.
 
Hayo ni maono na matamanio ya Rais Dr.Samia Suluhu Hassan yakatekelezwa kwa vitendo jijini Dar Es Salaam na majiji yote Tanzania.

In fact anastahili pongezi nyingi mno, na huo ni mwanzo tu gentleman.

Na maoni na mapendekezo yako huru yatachakatwa na wahusika kwa wakati muafaka.🐒
 
Bei elekezi ya pressure cooker 😁 na kuangalia receipt za watu, utaongeza matatizo badala ya kupunguza
 
Habari picha? Matomaso tukuaminije hapa?

Swala la risiti tuliache kwanza, uzalendo uanzie kwa sa100 na wasaidizi wake, sisi wala hatuna shida, ila kama tunasikia namna nchi inafujwa, watu wanaiba na kula kila mahali, unawezaje kutuhamasisha kuwa wazalendo sisi ambao tunaona mambo yakienda vibaya?
 
Hatukatai wafanyabiashara ndogondogo ila wawe sehemu maalum ,kufanya biashara kiholela hovyo hovyo ni kuchafua jiji ,mchana hawafanyi ila ikifika usiku wanarudi na kufanya ,ukipita asubuhi unaona mitakataka kibao kwenye barabara.
 
Hayo ni maono na matamanio ya Rais Dr.Samia Suluhu Hassan yakatekelezwa kwa vitendo jijini Dar Es Salaam na majiji yote Tanzania.

In fact anastahili pongezi nyingi mno, na huo ni mwanzo tu gentleman.

Na maoni na mapendekezo yako huru yatachakatwa na wahusika kwa wakati muafaka.🐒
Chawa kawaida yako, hata bwanako akikuridhisha unamshuru huyo muuaji
 
Gentleman,
makosa yangu ni yapi hapo na wakati sote ni mashahidi kwamba, alietoa maelekezo ya jiji la Dar Es Salaam kua safi wakati wote ni Rais Dr.Samia Suluhu Hassan?

Mihemko, makasiriko na Matusi yanini haswa dhidi ya ukweli mtupu mtupu dhidi ya jambo hilo muhimu na la msingi sana kwa ustawi wa jiji la Dar Es Salaam?

Kulikoni hujamtukana mtoa hoja aliepongeza kazi kubwa na nzuri sana iliyofanywa na wahusika wanaotekeleza maagizo na maelekezo ya Rais Dr Samia Suluhu Hassan?

au kwako matusi jukwaani ndio furaha yako?🐒
 
Suala la bei elekezi naunga mkono, bidhaa mpja haiwezekani mwongine auziwe 15,000 mwongine auziwe 30,000 huu ni wizi wa wazi
 
Hamjambo!

Jua ni Kali sana hapa! Kupigana vikumbo ni hali iliyozoeleka maeneo haya. Kelele za watu na magari kama kawaida. Hakuna anayeshtushwa na hayo. Imezoeleka hivyo.

Lakini kuna jambo moja sio la kawaida macho yangu yanaliona. Na naamini sio mimi pekee bali wengi wanaona hali hii.

Maeneo mengi ni masafi kwa kiwango cha kuridhisha. Kama tukiweka kwenye asilimia basi tunasema ni 75% maeneo ni masafi.

Macho yangu yanaona kila Duka, kila meza ina dustbin la kuwekea takataka. Jambo ambalo halikuzoelekea kwa wafanyabiashara wengi eneo hili.

Njia ni nyeupe, kukuta mfuko au uchafu unazagaa ni nadra sana kitu ambacho wiki kadhaa zilizopita miguu ya watu ilikuw ikiogelea kwenye uchafu.

Nawapongeza wahusika wote waliofanya jitihada hizi. Mambo ni mazuri huo ndio ukweli.
Serikali na wadau kazi hizi ndio zinadhihirisha kuwa serikali ipo na inaviongozi wanaojitambua.

Sio watu wanatembelea juu ya mavi, mitaa inanuka, takataka kila sehemu alafu unajiita kiongozi, sijui Rais, sijui Mkuu wa Mkoa, sijui Waziri. Nope!
Haya ndio mambo yanayowatambulisha kama viongozi wa maana kabisa.

Kingine naona barabara ni nyeupe, machinga hawapangi tena bidhaa zao katikati ya njia. Hili ni zuri sana.
Leo nimepita bila bughuza za kukanyaga bidhaa za watu au kusukumwa kwenye bidhaa za watu.

Taarifa niliyonayo hapa ni kuwa Machinga kesho watakuwa kwenye kikao saa tatu. Na tarehe 24 mwezi huu hakutakuwa na machinga eneo hili la Kariakoo.

Mambo muhimu ambayo nayapendekeza;

1. Serikali iangalie ni namna gani inaweza kusaidia hao vijana watakaondolewa hapa.

2. Mawinga wote uundwe utaratibu wa kuwasajili.
Kila Duka liwe na winga Rasmi ambao watavaa sare za duka husika. Na wawe kwenye umoja au kikundi cha mawinga Kariakoo.

3. Ipigwe kampeni na propaganda Mteja atakayekutwa na bidhaa isiyo na risiti Rasmi atatozwa faini elfu 50 au kuwekwa mahabusu kwa wiki nzima.
Ukibana wateja umembana mfanyabiashara.

4. Serikali iandae portal mtandaoni ya Lists za bidhaa na bei zake(range ya bei) ili kuwarahisishia wananchi kutokupigwa na wafanyabiashara au mawinga.
Mfano;
Simu ya infinix hot 40. Bei 200k - 350k kulingana na eneo mtu analochukulia.

Kwa nini?
Wafanyabiashara wanatumia mwanya wa kutotoa risiti kutokana na watu kutokujua bei halisi ya bidhaa. Hivyo mtu anajua ameonewa huruma kununua bidhaa fulani. Hata risiti hana ujasiri wa kuomba.

Mfano. Jiko la pressure cooker mteja ataambiwa 200k.
Mteja ataomba wataenda mpaka 130k. Watakubaliana kuuziana.
Mteja akidai risiti. Mfanyabiashara atamuambia kama unataka risiti leta 200k.
Automatically mteja atachukua kwa bei pungufu na risiti hataihitaji.

Bei elekezi ni muhimu. Kama kwenye vyombo vya usafiri tuu.
Unajua kutoka Dsm mpaka Arusha nauli ina range 50k - 100k
Hivyo mtu anajipimia anavyotaka bila kuonewa huruma, kuomba omba, na ticketing lazima wampe ticketi halisi.

Nikweli bidhaa zipo nyingi. Lakini wapo watu wakufanya hiyo kazi. Waziingize zote kwenye portal moja.
Mtu akienda sokoni anajua fika anachoenda kununua ni bei fulani.

5. Hili la Winga wa kila duka kuvaa sare zao ni muhimu sana.
Ili kuwadhibiti kisaikolojia.
Mfano kuna mawinga ambao wanatabia ya kushika shika mikono au matako ya wateja wanawake.
Mtu aliyevaa sare ya duka fulani ni ngumu sana kufanya hivyo kwani ataona anaharibu kazi, Jina la biashara husika.

6. Pia, Winga kuvaa Sare ya duka fulani inamtambulisha kwamba huyu ni winga kutoka ofisi fulani.
Inaepusha utapeli ambao ungeweza kudhibitiwa.

7. Biashara ya mtandaoni.
Serikali ni muhimu kurahisisha na kuandaa mfumo ambao wafanyabiashara wa mtandaoni watajisajili hukohuko mtandaoni. Watalipia kodi mtandaoni. Kila kitu kitamalizwa mtandaoni.

8. Isiwe lazima mtu kuja kupanga mafoleni huko kwenye maofisi yenu. Kwanza baadhi ya maofisa ni wavivu. Kitu cha Lisaa limoja unafuatilia miezi mitatu. Sasa ndio nini.

Dunia imebadilika. Vijana wa Tehama wapo. Waandae mfumo mzuri na wenye ulinzi. Vijana wapate pesa na serikali ipate pesa.

Sasa serikali inasema oooh! Ukifanya Biashara mtandaoni weka Cheti cha Biashara, sijui TIN namba sijui leseni ya Biashara.
Mtu ambaye hana hata mtaji ataweka?

Ongeeni na META au hao wenye mitandao ya kijamii wawawekee mifumo ya wanaofanya online business kama sisi wenyewe kama nchi hatuwezi.

Acha nipumzike sasa.

TaikonMaster
Kwa sasa Kariakoo, Dar es Salaam.

Ndiyo hivyo mnavyozitafuta posho za Makonda. Ongeza bidii atakuona.
 
Ni mawazo mazuri ila mawinga kuwa na Duka moja tu ni uongo hawatapata faida, winga anakuwa na maduka kibao kulingana na mahitaji ya mteja ndio wanavyoishi
 
Suala la bei elekezi naunga mkono, bidhaa mpja haiwezekani mwongine auziwe 15,000 mwongine auziwe 30,000 huu ni wizi wa wazi

Hakuna sehemu utapata kitu cha namna hiyo duniani ambapo biashara ni huria.

Kuna sababu nyingi zinazoamua bei ya soko.

Ndio maana hata katika nchi zilizoendelea kuna supermarkets zinauza vitu kwa bei rahisi kuliko mahali pengine hivyo watu wataamua waende wapi na utakuta huko kwenye bei rahisi kuna watu na kwenye bei ya kati wapo kadhalika pia katika maeneo yenye bei kubwa.
 
Back
Top Bottom