Nipo kiwandani Mtibwa, Turiani; umeme umekatika mara kumi toka saa kumi na mbili mpaka muda huu

Idara ya usalama wa taifa anzeni kuchambua ubora wa huduma za tanesco kwa watanzania vinginevyo mtamfanya mama alaumiwe bure.
 
Mpaka muda huu nipo turiani kwasasa umeme unawaka si ajabu haya majinga yamesoma uzi wangu. Mkifanya hivi hamumsaidii rais ila mnamuhujumu. Kama hamtaki tuamini ni hujuma mseme shida yenu ninini?

Mvua zisiponyesha mnasingizia ukame zikinyesha mnasingizia ninini?
 
Hujaeleweka....
 
....Uko TANESCO?....
 
Sawa, wakati wa Mwenfa zake John ulikuwa pia unakatika, lakini sio kwa Spidi hii!!
 
Ili uweze kusaidiwa andika kitu kinachoeleweka, siku moja huwa na saa kumi na mbili asubuhi na saa kumi na mbili jioni, sasa wewe ni saa kumi na mbili ipi mpaka muda huu ambao sisi hatuuoni! Acha ghadhabu uandikapo, tulia andika kitu sahihi kitakachoeleweka.
 
Umeme haukatiki wenyewe

Unakatwa

Weka record sawa
 
Hizi porojo na huu ujinga ulikuwepo awamu ya nne
 
Informed wapi mzee wakati huku mwanza tuna Mgao wa kimya kimya toka ijumatatu mpaka leo. Ni mgao wa kuanzia saa mbili asubui mpaka saa moja kasoro ndo wanarudisha umeme TANESCO shida nini mbona hamtuambii
 
Upo sawa lakini mkuu?
Kati ya mimi,wewe ambae Samia ni Rais wako mpendwa na Samia ambae aliahidi mwezi March 2021 kuwa ni mwisho wa umeme kukatika nchini halafu leo huko Turiani umeme umeshakatika mara kumi ni nani ambae hayupo sawa?
 
Nani kakudanganya kuwa kipindi cha Magu umeme haukuwa unakatika?
Hivi uliisikia kauli ya Makamba? Makamba alisema kwa kinywa chake "zamani umeme ulikuwa haukatiki mara kwa mara sababu walikuwa hawafanyi schedule maintenance..........".

Wabunge wakamwomba atoe, sheet yenye maelezo ya maintenance miaka mitano iliyopita hajatoa, labda may be mitambo ilikuwa ina muogopa Magu.
 
Kati ya mimi,wewe ambae Samia ni Rais wako mpendwa na Samia ambae aliahidi mwezi March 2021 kuwa ni mwisho wa umeme kukatika nchini halafu leo huko Turiani umeme umeshakatika mara kumi ni nani ambae hayupo sawa?
Samia anaendelea na mambo yake ila wewe bado unaendelea kupost kitu kile kile kila siku na zaidi ya mara moja, ndio maana nakuuliza upo sawa? kwa mtu mwenye akili ya sawa sawa angekwisha choka kufanya hicho unachofanya wewe au hizo likes unazopata ndio burudani kwako?

Nimeona muda mrefu sana haipiti siku bila kurudia kupost hako kapicha.
 
na umeme usipokatika kwa muda mrefu pia msifie serikali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…