Nipo kiwandani Mtibwa, Turiani; umeme umekatika mara kumi toka saa kumi na mbili mpaka muda huu

Nipo kiwandani Mtibwa, Turiani; umeme umekatika mara kumi toka saa kumi na mbili mpaka muda huu

Umeme sio Siasa mzee kama Mitambo na Miundo Mbinu ni chakavu huwezi kuzuia izo Outages, tofauti na kipindi Cha mwendezake kwa sasa outages zikitokea public inakuwa informed

Lakini amini kuwa Tanesco linaenda kuwa shirika bora miongoni mwa mashirika ya Umma its matter of time ila Statergic na plan tayari zimeanza kuwa implemented
Siasa hadi kwenye uneme duuuh
 
Nipo songosongo umeme una mwezi mzima hauwaki mji mzima ni sola na jenereta tu
 
Nina experience ya kuishi maeneo hayo hadi Dakawa na Mkindo kwa kina Amos Makalla huko ni hakufai upepo kidogo tu umeme umeenda alafu unakaa dakika 5 unarudi tena kukatika mara 10 ni kawaida ndugu😂😂
 
Lawama ni nyingi sana Kwa shirika hili lakini ukweli lazima niseme kwa upande wangu, TANESCO WANAJITAHIDI HASWAA kumbukeni kuwa ili ni shirika la umma ambalo hupata bajeti toka serikalini lakini naamini kuwa bajeti hiyo haitoshi ama hawapewi kwa muda muafaka.Tulipe muda nina imani serikali itariboresha shirika hili na kuwa moja ya mashirika bora kabisa ya kutoa huduma hapa nchini
 
Bado nipo turiani mpaka leo muda huu na saa hii 11:38 asubuhi umeme hakuna toka asubuhi.
Kati ya mimi,wewe ambae Samia ni Rais wako mpendwa na Samia ambae aliahidi mwezi March 2021 kuwa ni mwisho wa umeme kukatika nchini halafu leo huko Turiani umeme umeshakatika mara kumi ni nani ambae hayupo sawa?
 
Hapa moshi mjini umeme unawaka kama traffic light, kama fedha hazijatosha kumalizia mradi waongeze tozo tu mateso yapungue
 
Shida ya umeme wa Tanzania ni nini? Je, ni

Siasa?
Tanesco?
Maji?
Gesi?
Mitambo chakavu?
Hujuma?

Au nini? Mimi nilijua shida hii ipo maeneo ya mjini tu kukatikakatika kwa umeme ila sasa nimekuja huku Turiani, Mtibwa leo tu jioni mpaka muda huu umeme umekatika mara kumi sasa shida ni nini?

Mbaya zaidi watu wanasema angekuwepo Magufuli umeme usingekatika! Sasa mama Samia Suluhu Hassan Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kazi kwako.

D8096B81-49B8-4903-B242-BD50DD9702FF.jpeg
 
Umeme sio Siasa mzee kama Mitambo na Miundo Mbinu ni chakavu huwezi kuzuia izo Outages, tofauti na kipindi Cha mwendezake kwa sasa outages zikitokea public inakuwa informed

Lakini amini kuwa Tanesco linaenda kuwa shirika bora miongoni mwa mashirika ya Umma its matter of time ila Statergic na plan tayari zimeanza kuwa implemented
Unataka kusema miaka yote aliyoongoza dictator kulikua hamna outages zimeanza kutokea baada ya yeye kufa !?
How come yeye alimaintain kipindi chote hicho upande wa maji na umeme na bei za vitu [emoji854]
Pure propaganda.
 
Back
Top Bottom