Pre GE2025 Nipo kwenye hatua za mwisho za kusajili chama kipya cha siasa kitakachoing'oa CCM kabla 2025. Nahitaji vijana 10 tu kutoka kila mkoa

Pre GE2025 Nipo kwenye hatua za mwisho za kusajili chama kipya cha siasa kitakachoing'oa CCM kabla 2025. Nahitaji vijana 10 tu kutoka kila mkoa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Bila backup ya kiulinzi na usalama ni ngumu.
Kingine unahitaji vyombo vya habari kama radio,tv na magazeti kwa sababu kaa mkao wa hotuba zenu kupigwa marufuku kwenye vyombo vya habari.
Tafuta wanasheria nondo watakaoweza kukupambania hasa pale unapobablmbikwa kesi za kutunga.
Ndugu yangu ni vile hatujuani lakini karibu ofisini kwangu utaona maandalizi ya kutosha tuliyonayo ! Kuhusu vyombo vya habari Kila kitu kipo sawa ,tunategemea kwenda kwa msajili jumatatu kuwasilisha ombi letu ,tukitoka hapo tutajua namna ya kukutana na kuzungumza kulingana na taratibu za kisheria
 
IMG-20240414-WA0013(1).jpg

tunaweza sanaaa vijana sasa kesho niyamungu
 
Jina la chama na sera za chama hazitaundwa na mtu mmoja Bali zitatokana na mawazo ya wadau
Bwana mganguzi songa mbele, jikite zaidi kwenye sera za kuikwamua nchi ni sio sera za kulalama kila uchwao na kutukana watu, "Chama cha kisoshalisti cha jamuhuri ya watu wa Tanzania"
Jina hili litakipa nguvu chetu kipya. Maana ccm ni chama cha mapinduzi, kwa jina lake hakiishiki Tanzania kikamilifu.
 
Sina utani kabisa kwenye hili jambo nimedhamilia , kama vijana wa nchi hii ,tuliweka Imani kubwa sana kwa vyama vya siasa vilivyopo ,tangu mwaka 1995 mpaka sasa ,hakuna chama hata kimoja ambacho kimethubutu kuiondoa ccm na kushika Dola! Zaidi tu tunaona ni vyama vyenye malengo ya kujikimu kimaisha kupitia ruzuku wanayopata !! Hakuna kipya Cha kujifunza kwenye vyama vilivyopo kwa sasa ,kwa sababu vimetawaliwa na uoga ,ubinafsi na ukanda 😭vyama vilivyopo sasa haviwezi kushika Dola abadani! Sera za vyama vyetu vya siasa vilivyopo ni ama kujipatia kipato na kung'ang'ana ili kulinda maslahi binafsi ,ndio maana ni wale wale hakuna rotation ya kimfumo ,nenda uendako Kila ukirudi utawakuta ni wale wale ! Tunahitaji chama kipya kitakachotatua mtanzuko huu holela wa vyama siasa! Marehemu sengondo mvungi aliwahi kuonya umajumui wa vyama vyetu hasa uchaguzi ukikaribia kufeli kwa mikakati na usaliti . Sisi ni vijana na hii ni nchi yetu twendeni kifua mbele tuibebe Tanzania kuipeleka nchi ya ahadi ! Mimi naamini Kila mkoa wapo vijana wanaotamani mageuzi na nafasi ya kuonyesha karama zao katika siasa ! Majukwaa ya kisiasa yaliyopo sasa Yana wenyewe ! Ni yao na watoto wao ! Tuundeni chama kipya kama alivyofanya mwanamziki bobi wine pale Uganda! Ni kijana mdogo lakini amefanikiwa kuunganisha vijana nchi nzima na sasa chama chake Cha NUP ,kinaelekea kushika Dola! Tunao vijana bukoba ! Mbeya ,rukwa ,tabora ,ruvuma ,lindi ,mwanza na mikoa mingine yote ambao kwa pamoja tunaweza kuunda chama chenye nguvu sana na kikawashangaza watu! Tuache kukesha mitandaoni tukisubili eti vyama vilivyopo kwamba vinaweza kutuletea mabadiliko yoyote ! Tutakuwa wafu tunaosubili kuangua embe kwa miti ya michongoma ! Tuamke ,tuliamshe taifa letu !kama ni hivyo basi kwa mujibu wa Sheria na kanuni tunaanza kuelekea 2025 tukiwa na chama kipya Cha kisiasa!
= nimedhamiria

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
 
Back
Top Bottom