Nipo Mtwara, serikali ni kama imeususa kabisa huu mkoa. Nimepamiss Dar Es Salaam!

Safi sana mkipata ,nyie watu wa dat mkipata hizo tabu ndio Raha yangu.

Mara nyingi nimekuwa nazungumzia wajibu na ulazima wa Serikali kuweka uwiano wa maendeleo mikoani badala ya kujaza Kila kitu Dar.

Wakati huko hakuna miundombinu yeyote ya maana kulinganisha Wilaya na Wilaya Kwa kiwango kikubwa ,hapo Dar pekee wanajenga Barabara za mitaani km 250.

Na ikumbukwe Hela zao za Bandari,Korosho na gesi zinaenda kujenga Dar,Arusha na Dodoma.

Kwa kuwa umeenda kikazi Sasa utakoma
 
Dogo, mbona unakuwa muongo hivi, ni Mtwara gani uliyoenda wewe?
Bahati nzuri kwa sasa huko mikoa ya Lindi na Mtwara wanakunywa mpaka chai ya maziwa baada ya Wasukuma kuingia na makundi makubwa ya ng'ombe, sasa hivi hawali tena ngozi ya ng'ombe bali wanakula nyama yenyewe..
 
Haha na ntakoma kweli
 
Dar unakotoa pesa kwa wakala saa 7 usiku ni wapi kwa huku mitaani?
Yaani watu wa Dar tunapenda kilishana ujinga sana!
Hata mimi nashangaa hiyo saa saba mitaani Dar es Salaam unapataje huduma ya laki saba na mawakala wa Dar keshi tiatia maji!
 
Yaani watu wa Dar tunapenda kilishana ujinga sana!
Hata mimi nashangaa hiyo saa saba mitaani Dar es Salaam unapataje huduma ya laki saba na mawakala wa Dar keshi tiatia maji!
Sio kulishana ujinga !binafsi nastaajabu mkoa kama huu kuwa na huduma mbovu hasa maeneo ya mjini ...ukilinganisha na mikoa mingine ,,maeneo ya mjinj huwa yamechangamka ...kwa dsm huwezi zijua sehemu kwa sababu hujawahi patwa na shida ya namna hiyo usiku..siku ukipatwa na shida ya nmana hiyo ndo utajua kuwa watu dar hawalali
Na siyo dsm hata hapo moro na na sehemu nyingine za mjini ambazo nimebahatika kufika,huduma za kifedha zinapatikana masaa yote
Mtwara huku pharmacy anafunga saa 12 amezidi sana saa 2 na hapo ni mjini
 
Dar Wanalala bhana acha maneno yako! Ni sehemu chache sana hata Sinza utazikuta ziko wazi usiku mzima!
Sema mnapenda kukuza mambo tu!
Nikuulize huduma gani ambayo ipo Dar peke ake tu usiikute mkoani kama Mtwara! Huyo mtoa mada ni mhuni tu na hana maana.
Mkoa kama Mwanza mimi sioni tofauti na Dar es Salaam lakini mnapenda kudanganya na kuuufanya mji huu uchafu na usio nampangilio kama Dubai!
 
Huna akili ,ndo maana huelewi ..bye
 
S

Shooters patamu haswaa ijumaa nitarudi tena hapo
 
Bado upo, tena lately ni biashara ambayo ipo almost kila mtaa.
 
Ila waTanzania wengi wetu ni watu wa ajabu kweli kweli! Mtu anakupa experience yake. Bila mshipa wa aibu unasema ni muongo.

Kwa nini unaamini wewe ndo mkweli? Kwa nini. wasomaji wakuamini wewe? Na siyo mleta mada? Mhusika anakwambia kiwanja alichokielewa ni shooters. Wewe unampa viwanja standards zako..huku ukimwambia hana pesa! Aiseeee!
 
Hahaha! Wonders shall never end!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…